Kasomi
JF-Expert Member
- Sep 3, 2014
- 11,036
- 20,337
SAFARI YA KUTAFUTA PESA.
TUMIA NGUVU ZAKO KUPATA PESA.
Mtaji wa maskini ni nguvu zake mwenyewe, walisema wahenga.
Kubagua kazi ni kauli za wasio na maono.
Kuishi bila kazi na kuridhika kuwa duniani bila kujishughulisha na chochote wakati Mungu amekupa Uhai, akili, na afya njema UNAKUWA MZIGO KWA TAIFA.
Katika sehemu ya tano tuliona jinsi ya kutumia akili kuzalisha mawazo makubwa yanayoweza kumpa mtu pesa.
Katika sehemu ya sita nakukumbusha kwamba
Kuna siraha kuu 3 zinazoweza kukupatia pesa
1.Akili 2.Mikono 3.Mazingira.
Katika kipengele cha mikono nataka leo ujiulize swali hili
Je unaweza kufanya nini?
Kama unaweza kulima, LIMA upate pesa
Kama unaweza kubeba mizigo BEBA upate pesa
Kama unaweza kubeba tofali kwa mafundi au kuchanganya zege CHANGANYA upate pesa.
Kama unaweza kuchimba mitaro CHIMBA upate pesa.
Kwenye kitabu cha THE SCHOOL OF MONEY Mwandishi anasema kwamba Pesa zimejificha kwenye matatizo.
Hivyo basi ili upate pesa kwa kutumia nguvu zako ni muhimu kujiuliza kwamba
Je unaweza kutatua tatizo gani ili upate pesa?
Jijini Dar es salaam mvua ikinyesha daraja likabomoka kwenye mtaro au kijito fulani
Watu wanajitolea kutengeneza daraja la muda mfupi, au wakati mwingine wanapanga tofali kisha wanaweka kitambaa kwa mbele kidogo
Ukitaka kupita kwenye matofali waliyopanga kwa kuwa hutaki kulowa, ni LAZIMA utoe pesa.
Hivyo ndivyo maisha yalivyo, ukitatua matatizo ya watu, HAKIKA watakupatia pesa.
Tumia nguvu ulizonazo, kama mtaji wa kupata unachokitafuta.