Namsimulia Rafiki yangu wa Kijani (Part TWO)

Mwafrika mmoja

Senior Member
Joined
Mar 15, 2019
Posts
104
Reaction score
234
PART TWO

Basi bwana, katikati ya mwaka wa 2023 nilipata pigo ambalo lilibadilisha kabisa ndoto zangu za kusonga mbele na nilifikia hatua ya kuwaza nirudi zangu Kijijini nikaanze upya na maisha.

Mwezi Juni, mimi na sehemu yangu niliyokuwa nafanya kazi tulifikia mwisho. Niliumia kwasababu sikutarajia na sikujipanga kukabiliana na hali hiyo.

Mpaka hapo rafiki yangu wa kijani nilikuwa simuwazi tena kwasababu nilikuwa simuelewi, nikawaza nitafute kwanza pesa za haraka za kuendesha maisha yangu. Katika kujitafuta nikafikia hatua hadi ya kufanya kazi za nguvu za mikono kupata hela ya kula. Ndani ya mwaka 2023 wote nao ukapita 0 bila ya chochote kutoka kwa rafiki yangu wa kijani.

Mwaka 2024 nikiwa sina hali, siku moja nilipigiwa simu na rafiki yangu niliyewahi kufanya naye kazi, akanipa mchongo wa kazi ya kupata angalau hela ya kula akili itulie MUNGU AMBARIKI SANA. Hapa kuna somo kubwa unalipata kwamba popote pale unapoaminiwa kufanya kazi, ifanye kazi kwa uaminifu kwasababu utiifu wako na uaminifu ndiyo CV yako huko mbele.

Kipindi chote hicho sikuwahi kumsahau rafiki yangu wa kijani, ndani ya mwaka 2024 nikamrejea tena, safari hii nilikuwa na hasira sana, nikaingia chimbo kujifunza zaidi kuhusu yeye na namna anavyotoa pesa kwa watu wanaomtumia. Nikarudi kuboresha profile yangu na kazi ninazofanya, MUNGU si Mangungu ..... ndani ya miezi miwili baada ya kufanya maboresho nikapokea oda yangu ya kwanza ya $15.

Kwangu ilikuwa ni muujiza mkubwa sana sikuamini kama ni mimi nimefanikiwa kuingiza hela yangu ya kwanza mtandaoni. Japokuwa ilikuwa pesa ndogo lakini ndiyo ulikuwa mwanzo wa safari yangu mimi ya upendo na rafiki yangu wa kijani.

Mpaka leo kupitia rafiki wa kijani, nimefanikiwa kuingiza pesa ya kutosha (nitaleta screenshot). Ninampenda rafiki yangu wa kijani na kamwe siwezi kumuacha mpaka afilisike au afunge kampuni 😀😀.

Lengo langu ni kukuonesha kuwa mtandaoni kuna fursa nyingi sana. Tumia skill uliyonayo kuiuza na watu wakupe pesa, wewe kama mwalimu, daktari, dalali, IT, sales, mpiga picha.... unaweza kuuza ujuzi wako na ukapata pesa.

#Freelancing #Fiverr #WorkFromHome #MakeMoneyOnline #DigitalSkills
 
Tumjue rafiki wa kijani mkuu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom