Sikupi pesa ila nakupa mchongo, amua wewe

Sikupi pesa ila nakupa mchongo, amua wewe

Mwafrika mmoja

Senior Member
Joined
Mar 15, 2019
Posts
104
Reaction score
234
Siku chache zilizopita niliwapa stori ya rafiki yangu wa kijani ambaye amenisaidia kuona upande mwingine wa dunia ya freelancing. Wengi mliuliza:

"Huyo rafiki ni nani?"

Leo nimeamua kumleta rasmi.
Jina lake ni FIVERR.
Usichanganyikiwe na kizungu, ngoja nikuelezee kwa lugha rahisi.

Fikiria una ujuzi wowote unaoweza kumsaidia mtu mwingine. Inaweza kuwa kuandika, kutengeneza logo, kuhariri video, kufundisha Kiswahili, kupanga safari za watalii, kupiga picha, kutengeneza content za mitandao ya kijamii au hata kurekodi sauti tu.

Tatizo huwa moja.
Unajuaje wateja wanaokuhitaji?
Hapo ndipo rafiki yangu wa kijani anapoingia.

FIVERR ni kama dalali wa mtandaoni, lakini tofauti na baadhi ya madalali tunaowafahamu, huyu hakimbii na pesa za watu. 😄

Yeye anakupa sehemu ya kutangaza ujuzi wako kwa dunia nzima.
Mteja akiona huduma yako na akaipenda, anakupa kazi.
Lakini kabla hujaanza kazi, mteja analipa kwanza pesa kwa Fiverr.

Fiverr ndiyo inashikilia pesa hizo kwa usalama.
Wewe unafanya kazi.
Mteja anathibitisha kuwa ameridhika.
Kisha Fiverr anakutumia pesa zako.

Rahisi hivyo.

Jambo ambalo watu wengi hawalijui ni kwamba hapa si lazima uwe na PhD, Master's wala Bachelor's ndiyo upate kazi.

La hasha.

Kama una ujuzi ambao unaweza kumsaidia mtu kutatua tatizo, tayari una nafasi.

Unaweza kuwa:
✅ Mwongoza watalii
✅ Mwalimu wa Kiswahili kwa wageni
✅ Mpiga picha
✅ Content Creator
✅ Graphic Designer
✅ Video Editor
✅ Virtual Assistant
✅ Voice Over Artist

Kitu kingine kinachonivutia kuhusu Fiverr ni tofauti yake na platform nyingi za freelancing.
Kwenye platform nyingi, wewe ndiye unatakiwa kutafuta kazi.
Unaandika maombi.
Unaomba nafasi.
Unashindana na mamia ya watu.
Wakati mwingine unakosa kazi hata baada ya kutuma maombi mengi.
Lakini Fiverr mara nyingi mteja ndiye anayekutafuta.
Anaona profile yako.
Anaona kazi zako.
Anakutumia ujumbe moja kwa moja.
Mnakubaliana bei.
Analipa.
Unafanya kazi.
Unalipwa.

Ndiyo maana hata mtu aliyeanza leo anaweza kupata nafasi ya kupata oda yake ya kwanza ikiwa amejipanga vizuri.

Hatua za kufuata ni rahisi sana, kwanza unaingi kwenye platform kwa kusearch google, halafu unajiunga kwa kutumia email yako ya Gmail, halafu unajaza taarifa zako za profile ikiwemo ujuzi wako, uzoefu wako, potfolio na vyeti vyako kama unavyo (siyo lazima sana kwa kuanzia) halafu hatua inayofuata baada ya hapo ni kutengeneza GIG (tangazo la kuitangaza huduma unayotoa) kwa wateja. Ukishamaliza, kinachofuata wewe ni kusubiri upate message za wateja wanaohitaji uwafanyie kazi kisha wakulipe.

Pesa za kukupa sina, nashare haya ili nawe uweze kujitengenezea kipato mtandaoni.
Fursa mtandoni zipo
Watu wanalipwa kila siku
Swali ni:
Je, wewe uko tayari kujifunza na kujaribu?

KAZI NI KWAKO, ingia ujaribu ukikwama nipo kukusaidia!
CHAO 🟢
 
Yaan uwongo uwongo tuu..
Hiyo fivver sijui mdudu gani an ukianza process zao ndo utajua ujui kuna sehemu unafika watahitaji taarifa zako za bank na hapo ndo utajua ujui unaanza kuambiwa mambo ya kulipia

Faken
Fursa Fursana 😀

Taarifa za bank ili wajue pa kukuwekea pesa zako, usiopoge. Utajiri unahitaji risk 😂😂😂
 
Back
Top Bottom