Masokotz
JF-Expert Member
- Nov 26, 2018
- 3,878
- 6,548
Nimuda mrefu Tangu niweke andiko katika jamvi na jukwaa hili.Hii ni kutokana na changamoto na Purukushani za Maisha.Najua umekuja kwenye huu uzi haraka kwa sababu ya Kichwa cha Uzi.
Lengo la UZI huu ni kujadili kauli ya 'Njoo Upige Pesa' kauli ambayo huwa inasisimua,inahamasisha na kuwapa watu wengi sana mawenge.Katika maisha yangu huwa naongozwa na kanuni.Kanunu yangu muhimu inasema kwamba Ukiona unaitwa Fursa huenda wewe ndio FURSA.Hivyo basi ni muhimu sana unaposikia hii kauli basi hisia yako ya sita iwake na Taa nyekundu iwe angavu kwamba unaweza kuwa wewe ndio FURSA.
Hata hivyo kabla sijawadisappoint watu ni wajulisha tu kwamba sasa TIN zinazoanza na 2 zimetoka.Hii inamaana kwamba idadi ya walipa kodi imeongezeka.Idadi ya Biashara imeongezeka na idadi ya makampuni pia imeongezeka.Wakati ninaanza biashara ilikuwa ukitaka kusajili kampuni au jina la biashara ilikuwa inakulazimu usasifi km mia nyingi ili ufike Dar es Salaam,Pale Ushirika OFISI za Brela Ukabidhi Makaratsi kisha uanze na nenda rudi mpaka upati usajili wa kampuni.Sasa hivi unaweza sajili Kampuni ukiwa Sebuleni kwako na kama unapata shida unaweza kuwasiliana nasi ili tusaidiane.
Maendeleo ya teknolojia yameongezeka kwa kasi sana.Kwa sasa unaweza kuanzisha biashara ya kimataifa na kuiendesha ukiwa Sebuleni kwako na Ukapiga Pesa.Huu ni wakati wa Kupiga PESA.Swali la kujiuliza ni Je ninawezaje kupiga PESA.Hizi hapa ni baadhi ya Mbinu unaweza tumia:
NJOO TUPIGE PESA

- Anza kwa kutafuta Niche(Aina ya soko,biashara au huduma ambayo unaweza kuifanya na ukalipwa kwa kuifanya)Hapa kuwa Makini,Usikimbilie tu kufanya ile kitu wanasema inalipa,Vizia kitu ambacho watu wanahitaji ila hawajui kama wanahitaji au wanajua wanahitaji ila hawajapata.Viko Vingi sana kwa nchi yetu.
- Sajili Jina la Biashara/Kampuni kabisha kisha omba leseni ya kawaida. na ufungue Akaunti ya Benki.Ukishakamilisha Hatua hii unakuwa sasa wewe ni mfanyabiashara na Mkurugenzi wa Kampuni.
- Tengeneza Business cards,websites,social media pages na sajili namba ya simu maalum kwa ajili ya Biashara.
- Anza sasa kutafuta wateja kwa njia ya Outreach,Pigia simu au watumie Email.Weka tu lengo la Kupiga Simu 5 kwa siku na kutumia emails 5 kwa siku.Kwa wiki unakuwa umewafikia watu 50.
- Endelea kufuatilia changamoto za watu na kadiri unavyofuatilia ndivyo utakavyotengeneza mtandao wa wateja.
NJOO TUPIGE PESA