Repota ameriport vyema lakini kwa bahati mbaya/makusudi amepotosha kwa kiasi kikubwa,
Marehemu hakuwa ameiweka kiunoni na ilikuwa kwenye droo ya dash board ya gari na alikuwa ametoka kumpokea rafikiake airport na si huko mza kama alivyoriport,
marehemu alimwambia rafiki yake aliyetoka kumpokea kuwa nimeshavuta chuma na akampatia kuiangalia kwa kuwa jamaa alikuwa kiti cha nyuma katika kuangalia angalia akawa amebonyeza trigger hakuwa akijua kuwa kuna risasi moja ambayo ilikuwa tayari kwenye pipeline tayari kwa matumizi (wakati marehemu anampa bastola alitoa magazine)
Ni hiyo risasi moja ambayo hakuna aliyejua imebakia hivyo ikapita kiti cha nyuma na kumpiga jamaa kupitia mgongoni ikaharibu sana sehemu zake za siri,
Na bastola hii hakuwa ameinunua muda mrefu haipiti wiki moja toka ameinunua, waliokuwa ndani ya gari walikuwa watatu marehemu, rafikiake, na aliyekuwa ametoka kupokelewa pia akiwa ni rafikiake,
Maneno ya mwisho mwisho ya marehemu alisema bastola nimenunua mwenyewe na imeniua mimi mwenyewe, nawaomba sana msikubali kusema kuwa wewe ndio umenipiga, please please,
Aliyeifyatua kwa bahati mbaya au pasipo kujua kuwa kuna risasi imebakia hadi sasa anashikiliwa na polisi
Lakini kiukweli hakuna anayefuatilia kwa kudhania alimpiga makusudi,
Unaweza kumwangalia marehemu via facebook Godson Mollel,
Nimeandika bila mpangilio lakini mtakuwa mmenisoma.