Zanzibar 2020 Tume ya Uchaguzi Zanzibar: Kura ya mapema (Oktoba 27) haitahusisha Askari wote

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Jaji Mkuu mstaafu Hamid Mahmoud amesema kura ya mapema haitawahusisha wapiganaji wote wa vyombo vya ulinzi ikiwemo majeshi na Polisi, kama inavyodaiwa na watu wanaojaribu kupotosha ukweli na madhumuni ya kura hiyo.

Alisema hayo wakati akizungumza na viongozi wa vyombo vya ulinzi Chake Chake Pemba. Alisema sio wanajeshi wote waliopo Zanzibar na Polisi, watapiga kura hiyo siku moja kabla ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 28.

“Napenda kutoa ufafanuzi kuhusu kura ya mapema, sio askari wote watashiriki katika kura ya mapema ya tarehe 27 Oktoba... kura hiyo ni kwa watu maalumu ikiwemo watumishi wa tume na wasimamizi wa uchaguzi na askari ambao watahusika katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 28 tu”alisema.

Alisema vipo jumla ya vituo vya kupiga kura 1,412, ambapo watumishi wapatao 7,000 watashiriki katika kura ya mapema Oktoba 27 kwa upande wa Unguja na Pemba.

‘’Hizo ndiyo sababu za kuwepo kwa kura ya mapema. Kati ya vituo vya kupigia kura 1,412 vilivyopo Unguja na Pemba, ni vituo 407 vitatumika kwa ajili ya kupiga kura hiyo siku moja kabla ya kura ya watu wote ya Oktona 28,”alisema.

Alisema tayari tume ya uchaguzi imetoa tangazo kwa vyombo vya ulinzi, kuwasilisha majina ya watu wao ambao watapiga kura ya mapema siku moja kabla ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 28.

Aliwataka viongozi wa vyama vya siasa, kuondoa hofu na wasiwasi kuhusu kura ya mapema, ambapo utaratibu wake upo unafahamika na kusimamiwa na mawakala wote wa vyama vitakavyoshiriki katika uchaguzi.

Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Thabit Faina Idarous alivipongeza vyama vya siasa kwa kufanya kampeni za kistaarabu wakati kampeni zikiwa zimebaki siku 23 kuingia uchaguzi mkuu wa Oktoba 28.

Alisema vyama vya siasa kupitia wagombea wake wote, wamezingatia kanuni na sheria za uchaguzi kufanya kampeni zitakazozingatia amani na utulivu na kuepuka matusi.
 
Njia za kughairisha uchaguzi zimeshindikana, ndio wamekuja na staili hii ya kupiga kura mapema. Goli la mkono hili.
 
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jaji Mkuu Mstaafu Hamid Mahmoud amesema vyombo vya Ulinzi vitapiga Kura siku moja kabla ya Uchaguzi Mkuu, Octoba 28 na tayari Tume imeshatoa tangazo kwa vyombo vya ulinzi na kuwasilisha majina ya wapiga kura.
Ameeleza pia.

"Sio Askati wote watashiriki katika kura ya mapema ya tarehe 27 Oktoba, kura hiyo ni kwa watu maalum ikiwemo Watumishi wa Tume, Wasimamizi wa Uchaguzi na Askari ambao watahusika na Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28 tu" Jaji Mkuu Mstaafu, Hamid Mahmoud.
 
Njia za kughairisha uchaguzi zimeshindikana, ndio wamekuja na staili hii ya kupiga kura mapema. Goli la mkono hili.

Afadhali goli la mkono wachezaji wako uwanjani ,hapa wanawafanya watu wote ni wasenge !!!! ni goli la makalioni hili
 
Watumishi wa NEC hawatoshiriki?

Daftari la hao wapiga kura litawekwa wazi lini?

Wizi huu hata mtoto mchanga huwezi kumdanganya , Tafuteni njia nyengine hapa hata hamjachemsha mumeunguza sufuria
imagine hao wanajeshi na polisi siku hiyo wanaenda na vitambulisho vya kazi zao na kuonyesha then vitambulisho vingine vya kupiga kura ,maana bila hivo raia wa kawaida wanaweza kuchanganywa na jeshi
 
ACT welala wanasubiri kura za huruma toka CCM.

Hakuna sababu zozote za kuwafanya Wazanzibari kupiga kura siku Mbili.
HUWA NAWASHANGAA SANA WAISLAM POPOTE WALIPO PALE WANAPOFANYIANA DHULMA KWA SABABU YA KUENDEKEZA MASLAHI BINAFSI. YANI KWELI KABISA UNAMKUTA MTU ANASWALI KABISA SWALA TANO HALAFU AKITOKA MSIKITINI ANAFANYA NJAMA NA HILA ZA JAMBO BAYA LISILO LA HAKI NA LINALOWEZA KUSABABISHA WATU WAKAFARAKANA NA YA KUJENGA CHUKI.

MAMBO YA DHULMA YANAYOFANYWA NA CCM KULE ZANZIBARI YALIPASWA KULAANIWA NA WAUMINI WOTE WA KIISLAM DUNIANI MANA NI DHULMA ZA WAZI KWA BINADAM YEYOTE MPENDA HAKI.
DINI YA KIISLAMA INAJIPAMBANUA KAMA DINI YA HAKI .
HIVI CCM wao wangependa mambo wanayowafanyia wengine wao nao siku moja wafanyoiwe ? Au ni kiburi cha kudhani kuwa wao watakaa madaraiani milele?
TUME ilyojaa makada wa CCM inaonuonyesha wazi jinsi chama hicho kilivyokosa watu wenye hofu kwa Mwenyezi Mungu. Kila idara imejawa na hila tu bila kujali furaha ,amani na ustawi wa binadamu.
CCM inaona raha sana kuwaacha Wazanzibari kuendelea kuishi kwa chuki ,hila na mifarakano kwa kwa sababu ya kulinda neno CCM utafikiri Hicho chama ni Aya iliyoteremshwa na Mwenyezi Mungu kumbe ni chaka tu kilichoundwa na watu na kitakufa kama waasisi wake nao wanavyozidi kuondoka duniani . Waanzilishi wa CCM wanavgozidikupungua kwa kutangulia mbele za haki ndivyo na chama hicho kinavyopoteza nguvu duniani. Hivyo kukifanya Chama cha mapinduzi kuwa ndicho kilichobeba roho na maisha ya watu ni kujidanganya kwani kimeanzishwa na wanadamu walioumbwa kwa udongo.
 
Back
Top Bottom