Mkuu Bob,
Nakubaliana na wewe kuwa tunatakiwa kupiga vita dalili zote za udini na ukabila ingawa naweza kutofautiana nawe juu ya kulinda muungano kwani muungano kwa mfumo tulionao mimi natamani uvunjike hata leo.
Kwa upande mwingine, ninasikitika sana kwamba kauli tunayolalamikia imetolewa na mzee ninayemheshimu, mzee Mtei. Kwanye andiko lake, mzee Mtei kaandika, rightly, kwamba madhehebu ya dini yana inflluence isiyoweza kupuuzwa kwenye jamii . Kwa mtazamo wangu, kama maoni yake yangelenga ile tume kupata uwakilishi toka BAKWATA, CCT, PCT nk sioni kama ingeleta mkanganyiko huu ulioletwa kwa kuangalia tu idadi ya wajumbe waislam na madhehebu mengine.
Tumepiga sana kelele baada ya Mkapa kutoa kauli zisizostahili kwenye kampeni za ubunge huko Arumeru. Kwangu mimi, heshima ya mzee Mtei kwenye jamii si ya chini sana kuliko Mkapa, mzee Mwinyi nk. Mimi naweza kuandika kile ninachojisikia kuandika, lakini hawa ni watu wanaopaswa kupima kauli zao kabla ya kuzitoa. Katika hili mzee Mtei kachemsha big time.