CHADEMA inaangalia uwezo na uadilifu; maoni binafsi yasichukuliwe kuwa ni msimamo wa CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA inaangalia uwezo na uadilifu; maoni binafsi yasichukuliwe kuwa ni msimamo wa CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by John Mnyika, Apr 9, 2012.

 1. John Mnyika

  John Mnyika Verified User

  #1
  Apr 9, 2012
  Joined: Jun 16, 2006
  Messages: 715
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinatoa taarifa kwamba maoni binafsi ya viongozi na wanachama wasiokuwa na mamlaka kwa mujibu wa katiba, kanuni na itifaki ya chama kuwa wasemaji wakuu wa masuala ya chama katika ngazi husika yasichukuliwe kuwa ni msimamo wa CHADEMA.

  CHADEMA kinatoa taarifa hii kufuatia maoni binafsi ya muasisi na mwenyekiti mstaafu wa CHADEMA juu ya wajumbe wa tume ya mabadiliko ya katiba yanayoelezwa kutolewa katika mtandao wa jamii wa Jamii Forums kutafsiriwa kuwa ni msimamo wa CHADEMA.

  CHADEMA kinatoa mwito kwa wachangiaji katika mitandao ya kijamii na wananchi kwa ujumla kuzingatia kuwa CHADEMA bado haijatoa kauli juu ya wajumbe wa tume husika kwa kuwa bado CHADEMA inaendelea kufanya uchambuzi juu ya wasifu wa wajumbe wa tume husika na mchakato wa uteuzi wao kama tulivyoeleza kwenye taarifa kwa umma tuliyotoa tarehe 7 Aprili 2012.

  Hata hivyo, izingatiwe kwamba uchambuzi wa wasifu wa wajumbe walioteuliwa kwenye tume husika unaoendelea kufanywa na CHADEMA hauhusu dini za wajumbe wa tume kwa kuwa CHADEMA hakiamini katika udini bali unahusu uwezo na uadilifu wa wajumbe husika na iwapo umezingatia matakwa ya umma na dhamira ya kujenga muafaka wa kitaifa wa kuwa na katiba mpya na bora.

  Izingatiwe pia kwamba kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA ibara ya 3B kifungu cha 3.1.9 ikiwa ni sehemu ya misingi iliyopo kwenye itikadi ya CHADEMA ya mrengo wa kati, CHADEMA inaamini katika umuhimu wa uhuru wa kuamini katika kujenga maadili ya mwanajamii mmoja mmoja bila kuifanya dini kuwa sehemu ya dola na na misingi mingine ya CHADEMA ya kujenga chama na taifa lenye kutoa fursa kwa kuzingatia uwezo na uadilifu bila kujali tofauti zingine.

  Pamoja na kujulisha umma kwamba CHADEMA kinaendelea kufanya uchambuzi wa wajumbe walioteuliwa kwenye tume husika, tulieleza kuwa CHADEMA kilitarajia kwamba Rais Jakaya Kikwete angeeleza pia ratiba ya kufanyika kwa marekebisho mengine muhimu ya awamu nyingine kuhusu bunge maalum la katiba na hatua ya kutunga katiba mpya na usimamizi wa kura ya maoni itakayowezesha wananchi kufanya maamuzi kwa uhuru na kwa haki kabla ya mchakato kufikia katika hatua husika.

  Tunasisitiza umuhimu wa Serikali kutoa kauli kwa umma kuhusu ratiba ya marekebisho ya awamu nyingine ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011 kwa kuzingatia kuwa Ofisi ya Bunge imetangaza kuwa Mkutano wa Bunge utaanza tarehe 10 Aprili 2012 bila marekebisho ya sheria ya katiba kuwa sehemu ya orodha ya miswada ya sheria inayotarajiwa kujadiliwa katika mkutano wa saba wa Bunge.

  Tunarejea kuutarifu umma kuwa Kamati Maalum ya Kamati Kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) iliyoundwa tarehe 20 Novemba 2011 kwa ajili ya kukutana na Rais Jakaya Kikwete kuhusu sheria ya mabadiliko ya katiba ya mwaka 2011 itafanya kikao chake karibuni mara baada ya uchambuzi kukamilika kupitia taarifa ya uchambuzi unaofanywa juu ya uteuzi uliofanyika wa wajumbe wa tume na tamko litatolewa kwa umma kuhusu mchakato huu muhimu kwa maslahi ya taifa.

  Imetolewa tarehe 09 Aprili 2012 na:

  John Mnyika (Mb)
  Mkurugenzi wa Habari na Uenezi
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Apr 9, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Safi sana, nimeipenda hii statement.
   
 3. M

  Molemo JF-Expert Member

  #3
  Apr 9, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Hii ndiyo CDM bwana.Asante Mungu kwa chama hiki makini
   
 4. OKW BOBAN SUNZU

  OKW BOBAN SUNZU JF-Expert Member

  #4
  Apr 9, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 22,667
  Likes Received: 17,719
  Trophy Points: 280
  Kaka umewakata vilimi vyao, mzee kaeleza msimamo wake, mijitu mbayuwayu inatuaminisha kama msimamo wa chama..ila fanyeni kutoa msimamo mapema
   
 5. B

  Bayyo JF-Expert Member

  #5
  Apr 9, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,108
  Likes Received: 917
  Trophy Points: 280
  Well said, I support!
   
 6. m

  mtengwa JF-Expert Member

  #6
  Apr 9, 2012
  Joined: Aug 20, 2011
  Messages: 1,745
  Likes Received: 225
  Trophy Points: 160
  Safi, kauli ya mtu mmoja isichukuliwe kuwa ya chama
   
 7. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #7
  Apr 9, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,265
  Trophy Points: 280
  Naamini hii ni kauli ya Clouds Fm, Asanteni kwa uelewa wenu, pls Foward this kwa Kibonde kwenye Jahazi lake.
   
 8. F

  FJM JF-Expert Member

  #8
  Apr 9, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Naunga mkono hoja 100%. Mnyika hivi ndivyo mnatakiwa kufanya kazi. Mnatoa ufafanuzi haraka. Safi!
   
 9. AirTanzania

  AirTanzania JF-Expert Member

  #9
  Apr 9, 2012
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 1,127
  Likes Received: 678
  Trophy Points: 280
  Asante mkuu kwa haya uliyotuandikia hapa, ila hakuna kulala mpaka mkoloni wa mweusi anang'olewa
   
 10. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #10
  Apr 9, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Mzee mtei ni muasisi na ni muasisisi wa chadema maoni yake yana nguvu katika chama mnyika! hilo halipingiki hata kidogo.
   
 11. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #11
  Apr 9, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Mkuu hapo mmenena ni kweli huwa hamkurupuki.
   
 12. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #12
  Apr 9, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Myika in the JF. CDM wako juu. Hawa wengine hata hawajui kutumia kompyuta.
   
 13. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #13
  Apr 9, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Sasa unataka kulazimisha? yale yalikuwa maoni ya mtanzania kama Kikwete alivyo na maoni yake.
   
 14. m

  mzee wandimu JF-Expert Member

  #14
  Apr 9, 2012
  Joined: Sep 23, 2011
  Messages: 441
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  mkuu asante! kwakutoa taarifa mapema! make kunawatu walianza kung'ang'ania kuwa nikauli ya chama!
   
 15. Bukanga

  Bukanga JF-Expert Member

  #15
  Apr 9, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 2,863
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  Mnyika is young & smart, hard working....

  He deserve some salutation.
   
 16. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #16
  Apr 9, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Maji yemshamwagika tena kwenye udongo wa kichanga, hayawezi kuzoleka.
  Ila mnyika leo kidogo nimekukubali, ila yameshatokea na huyo mzee wenu ndo keshajulikana his true color.
   
 17. D

  David webb Senior Member

  #17
  Apr 9, 2012
  Joined: Nov 20, 2011
  Messages: 159
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MNYIKA unanishangaza sana,mzee mtei ni kiongozi mwenye nguvu sana CHADEMA.mimi naamini hakuteleza hii ni ajenda yake na CDM wanaifanya makusudi.halafu ajabu mpaka ZITTO kamponda ww unajifanya kumtetea.kiufupi chadema ni wadini hata kampeni zao wanaegemea upande mmoja tu.
   
 18. Omuregi Wasu

  Omuregi Wasu JF-Expert Member

  #18
  Apr 9, 2012
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 753
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Naunga mkono hoja. Ubarikiwe!
   
 19. M

  Mahumanga Member

  #19
  Apr 9, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kamanda naunga mkono hoja 100%. Shida ya magamba ni kukosa analytical skills za kuchambua mambo, yanakurupuka tu kuropoka mambo. Sawa Mtei ni mwasisi wa CDM lakini si msemaji wa CDM. Shukuran kwa stament yako kamanda Mnyika.
   
 20. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #20
  Apr 9, 2012
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,650
  Likes Received: 21,865
  Trophy Points: 280
  Aboud Jumbe na Nyerere ndio waasisi wa CCM 1977. Jee Jumbe akitoka huko aliko na kusema lolote hiyo ni kauli ya CCM? Mbona na Nyerere alipolipinga azimio la Zanzibar na kuuzwa kwa NBC hamkusema hiyo ni kauli ya CCM bali mkasonga mbele na kumpuuza?
   
Loading...