Tumaini TV(TVT) ni Mali ya CCM?

... Japo tunafahamu kwamba Polycap Pengo ni mwanaccm lakini kwani Pengo ndio mmiliki wa TV Tumaini?
Naona unajiuliza na kujijibu. Mzee wa watu unamtaja wakati hana mamlaka yoyote kwa uendeshaji wa TV Tumaini. Laana nyingine mnajitakia tu, hata magonjwa ya akili hayo ni laana za kuwakosea adabu wakubwa
 
Samahani kwa maswali ni katika kukuza uelewa tu je muumini asipochangia gharama za uendeshaji wa Kanisa, Kanisa likigoma kumpa huduma ni makosa ?
TV ipo hewani, ukilipia king'amuzi tu unaipata bila kujali umechangia kanisa au haujachangia. Elewa mada inayozungumzwa, usikurupukie mambo mengine
 
Ni makosa makubwa kwa kanisa kumpa muumini huduma za kiroho kwa sababu zozote, Mungu alituumba bure, akatubariki bure, na kumuomba Mungu ni bure, makanisa wanapaswa kutoa huduma za kiroho bure.
NB. Makanisa yanaendeshwa na binadamu, kuna mambo ya kibinadamu, hawa waendeshaji wanayachomekea ambayo sio ya Kimungu!. Kuna watoto wanakataliwa kubatizwa, ndoa kukataliwa kufungwa na kukataliwa kupewa huduma za mazishi, ni makosa makubwa ya kibinaadamu tuu.
P
Kwa mfano utaratibu wa Kanisa ili utambulike kama Mkatoliki lazima uwe kwanye jumuiya muumini hataki kushiriki jumuiya kwa hiari yake mwenyewe siku imetokea amefariki ndugu ndo wanajitokeza na kusema ni mkatoliki wanataka kanisa limzike je kanisa likisema halimtambui likakataa kushiriki kosa la kanisa ni nini hapo ?
 
CCMM Si chama Cha siasa.

CCMM ni DINI kama zilivyo dini zingine, ukibisha nenda uliza pale St Petro utaambiwa.

Babu alitufunga na kitu kizito shingoni!!!

Bt muda umefika, wajukuu tutakuwa huru tena.

Ameeeen.
 
Naona unajiuliza na kujijibu. Mzee wa watu unamtaja wakati hana mamlaka yoyote kwa uendeshaji wa TV Tumaini. Laana nyingine mnajitakia tu, hata magonjwa ya akili hayo ni laana za kuwakosea adabu wakubwa
bila shaka humjui Pengo
 
Alafu Tangu NDUGU ZANGU CHADEMA waamasishane kususia kuangalia vyombo vya habari vinavyoshikamana na CCM nilitarajia mpaka leo wangekuwa tayari wameanzisha VYOMBO VYAO VYA HABARI.
 
We dogo, kwanza uwe na adabu na heshima kwa wakubwa zako, mimi nimehudumu media kwa miaka zaidi ya 30, kuniambia nimekurupuka ni kama kunitukana!.

Pili naendelea kusisitiza habari ni bure dunia nzima, ili chombo cha habari kiitangaze habari yako kuna mambo 3 lazima yafanyike
1. Uwe na habari kweli ambayo kweli ni habari.
2. Media ialikwe kuchukua hiyo habari na media kuwa facilitated kuiripoti hiyo habari
3. Kuwepo kwa nafasi ya kuitangaza hiyo habari.
Hivyo unavyoona hizo habari za CCM ujue
Kwanza ni habari kweli, pili media imealikwa na kuwa facilitated na tatu nafasi imepatikana.

Kama una tukio lako, waalike media, facilitate them, mtatangazwa kama news za CCM!.
P
NA HAWA NDIO WANAOMBA WAPEWE NCHI!!
 
Mara ya mwisho ametoa kipaimara hapa Parokiani, kwa afya na umri wake ule, hayo uliyoyasema hakika unamuonea. Ndio maana nikakwambia unajitafutia laana tu
Laana nipate kutoka kwa Mtu kama Pengo aliyedai Magufuli chaguo la Mungu ! basi labda Mungu awe shangazi yako
 
Tanzania Daima ya mwenyekiti ilipigwa roba ikapotea
Wakati tukisubiri muendelezo wako, naomba kujitambulisha kwako kuwa mimi ni miongoni mwa watangazaji waanzilishi wa Tumaini media ile 1994, Tumaini media ni independent, inapokea habari na matangazo toka popote as long as sio contents itakayo kwenda kinyume cha imani ya Ukatoliki. Kwa kukusaidia ni kuwa CCM wanalipia, hata makanisa mengine pia wanalipia, njooni tuu mlipie contents zenu mrushwe!. CCM inamiliki Uhuru/Mzalendo, Radio Uhuru, Channel Ten, Magic FM na Classic FM.
Sijui kwanini vyama vingine vinashindwa kuwa na media yake?!, niliwahi kuwa na matumaini na hawa jamaa zangu, Elections 2015 - Mabadiliko Chanya ya Ujio wa Lowassa: CHADEMA Kuhama Ufipa!, Kuwa Makao Yake, Kituo cha TV na Redio!
Kumbe hii ilikuwa ni ndoto tuu ya mchana!.
P
 
Back
Top Bottom