Mwanaume kugombania rimoti ya TV ni ushamba

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,513
Habari wakuu,

Husika na kichwa cha habari hapo juu, kisemacho mwanaume kugombania rimoti ya TV ni ushamba.

Naandika huku nacheka hapa, kisa kulikuwa hivi, kama mjuavyo siku za sikukuu watu hujumuika na familia.

Kilichonichosha ni kwamba kuna mwamba mmoja alikuja kwa familia yetu, kama mjuavyo familia zinakuwa pamoja.

Ajabu ni kuwa mwamba alikuwa kazi yake ni kuangalia TV yaani muda wote ni TV tuu.

Sasa mwamba akishakaa kwa kochi na kibukta chake, hatoki anabadili channel moja kwenda nyingine.

Kimbembe ni kuwa anagombana hadi na watoto kwa kugombania rimoti ya TV, yaani anawakatiza kuangalia vikatuni vyao.

Mwamba mwenyewe ni baba wa watoto yaani hana habari kabisa, watoto wanalia wala yeye amekazana na TV.

Mi nijuavyo wanawake ndio wanakuwa na mambo ya kuangalia TV muda wote pamoja na watoto.
 
Huwa sipendi upuuzi wa kugombania remote, mi kama baba naweka tv kila chumba kuanzia sebuleni. Nikiwa chumbani kwangu sitaki usumbufu kwa ninachotazama, watoto wana yao vyumbani mwao na wale wa sebuleni wana yao huko
 
Mlioenda kubugia pilau za Christmas na mwaka mpya reports zenu zimeanza kutoka!

Mwingn afuate!

Wale wa migombani mda wenu bado nyie mtakua wa mwisho maana ambao wake zao walienda wanasema diameter waliyokuta siyo kbs
 
Mimi ndiyo maana nikisafiri huwa ninafikia Lodge. Gubu kama hizi hapana aisee.
 
Mlioenda kubugia pilau za Christmas na mwaka mpya reports zenu zimeanza kutoka!

Mwingn afuate!

Wale wa migombani mda wenu bado nyie mtakua wa mwisho maana ambao wake zao walienda wanasema diameter waliyokuta siyo kbs
 
Huwa sipendi upuuzi wa kugombania remote, mi kama baba naweka tv kila chumba kuanzia sebuleni. Nikiwa chumbani kwangu sitaki usumbufu kwa ninachotazama, watoto wana yao vyumbani mwao na wale wa sebuleni wana yao huko
Kwa wale wenye uwezo ni vema wafuate mtindo wako wa kuweka TV kila chumba.

Nashauri wale walalahoi wawe wanaenda vibanda umiza au baa.
 
Huo muda wa kugombania rimoti unatoka wapi? Mi ninachojua tv Ni kwaajili ya familia(mke na watoto)
 
Tv ni watoto, mdada wa kazi na Mwanamke...
Mwanaume kama una ulazima nunua king'amuzi chako Tafuta T connector unganisha yako chumbani angalia
Mpira, Movies, mieleka, World Discovery,
 
Mimi cha kuniweka mbele ya tv ni mpira tu tena huwa naenda kuangalia pub. Hata nikirudi home mwisho wa mwaka naweza kukaa mpaka siku tano sijaenda sebuleni maana hakuna cha kukifuata uko.
Sasa Huna Ajira...TV utoe wapi...kapuku wewe
 
Back
Top Bottom