Tulipokuwa primary,unakumbuka?

Yeah yote tisa kumi TUJIFUNZE LUGHA YETU-"KIBANGA AMPIGA MKOLONI"Kiburi si maungwana bwana.
Mhh nawasikitikia sana watoto wa siku hizi sijui wanasoma nini,madogo hata nikiwauliza std 2 walisoma nini hawakumbuki ni michanganyo tu kutokana na haya mambo ya kina mungai. Wakati mie hadi leo nina kitabu cha SOMENI KWA FURAHA
 
I say! Mmenikumbusha mbaali! Nambo ya "Gulio Katerero". Mimi nilifikiri ni jina na tukio la kufikirika tu, haa, kumbe ni gulio la kweli! Hata watoto wa siku hizi, akina Saida wamelitungi wimbo.
 
Ati neno ajuwa linatokana na neno "as you were"
I say! Thanks, nilikuwa sijui asili ya neno hilo, ingawa ktk gwaride la kiskauti tulikuwa tunayatumia maneno "as you were".

Mnakumbuka kile kitabu "Someni Kwa Furaha"? Nadhani kile ndicho kilikuwa na hadithi za "Omari Hodari" na "Bulicheka".

Duuh! "Kana Kansungu, Umwelu!". Yule alikuwa stupid Kalagesye nadhani!

Nani anakumbuka hadithi ya "Bwana Matata"?
 
someni kwa furaha ndicho kitabu ambacho nilianza nacho na nilifurahia sana ule wimbo wa makari hodari.
nani anakumbuka shairi la Mtayapata shambani??????? japo arecite hapa tukumbukie
 

Heee! Yaani hiki kitabu nilivyokuwa nikikiazima maktaba, kilikuwa km cha kwangu; maana kila tarehe ya kubadilisha ikifika, nilikuwa nakwenda kuongeza muda. Tangu nilipokiazima siku ya kwanza, basi sikukiachia. Duuh! Asante kwa kunikumbusha, Jafar.
Lkn mnakumbuka BULGA? Sijui km kwingine mlikuwa mnaita hivyo. Ni ule uji wa ngano, uliokuwa ukipikwa kwa mafuta ya chapa ya mikono (Handshake) na bendera ya USA. Duuh! Wengine walikuwa wakija shule kwa ajili ya kunywa uji tu!
Nimekumbuka mbali sana!
 
 
hahahahahaha hakya mungu hahahaha tena
 
Karudi baba mmoja,toka safari ya mbali,kavimba yote mapaja na kutetemeka mwili,watoto wake wakaja ili kumtaka hali wakataka na kauli iwafae maishani.
Akatamka mgonjwa ninaumwa kwelikweli hata kama nikichanja haitoki homa kali.......kama mnataka mali mtayapata shambani. Japo kwa hapa tu nakumbuki,naam siku hizo zilifurahisha sana
 
Msanii unakumbuka hadithi ya mgeni siku ya kwanza?....mgeni siku ya tisa kwa mateke na magumi,asirudi tena nyumbani afukuzwaye mgeni.
 
du wee unatisha,hahaha umenifurahisha sana,nadhani hiyo ndio maana halisi
 
Nakumbuka nililamwa viboko vitatu kwa kukutwa nasoma huku natoa tabasamu la nguvu kitabu cha Hesabu cha KIONGOZI CHA MWALIMU
 
Kulikuwa na mti unaoitwa mmavimavi. Wale wanafunzi watukutuku wasiopenda hesabu...🙂 walikuwa wanachuma majani yake na kwisha kwenda kuyapikicha kwenye meza ya mwalimu, basi akiingia mwalimu hakai pale mezani maana ni harufu ya haja kubwa tupu...LOL!
Mwalimu huanza kulalama kwamba kuna harufu ya kinyesi na kuangaza huku na huko labda ataona kinyesi, lakini bila mafanikio yeyote na mwisho husogea mbali kabisa na meza hiyo na mara nyingine alikuwa akiwaamrisha baadhi ya wanafunzi waliokuwa wanakaa mbele ili wasafishe...basi watukutu huwaambia wale wasafishe taratibu ili kipindi kiishe...utoto jamani!...🙂
 

LOL!...Kuna mwalimu mmoja alikuwa anaitwa cheka cheka...saa zote alikuwa anaonekana amekenua tu, kama humjui utadhani alikuwa anacheka...🙂. Huyu yeye alikuwa ni Mwalimu mkubwa na pia fimbo mkononi na alikuwa anapenda sana kuchapa hata kama aliyokosewa ni mwalimu mwingine. Na fimbo zake zilikuwa ni kali mno. Basi unajua tena shuleni lolote lile linaweza kutokea hivyo huyu kaptula mbili zilikuwa hazitoshi ili kupunguza ukali wa fimbo zake...tulikuwa tunaweka tatu tatu kujiandaa kwa lolote lile...🙂, lakini alikuwa mwalimu mzuri sana wa hesabu na kiingereza. Mungu amlaze mahali pema peponi.
 
Nakumbuka kitabu cha MASHUJAA WA KAZAKAMBA! hiki kilini vuta sana,
Sikumbuki majina ya wahusika wakuu, ila walimkamata mwizi wa 'nyanya' kama sikosei.
Vitabu vya zamani vilikuwa na ujumbe.
 
Nakumbuka nililamwa viboko vitatu kwa kukutwa nasoma huku natoa tabasamu la nguvu kitabu cha Hesabu cha KIONGOZI CHA MWALIMU

hahahah ebwana umenivunja mbavu kwelikweli, kwa hiyo ticha alikuwa akitoa zoezi wewe unapata zote daily!
 
sio kuvaa kaptula mbili mwanangu ile ilikuwa inaitwa kujaladia
 
Nakumbuka nililamwa viboko vitatu kwa kukutwa nasoma huku natoa tabasamu la nguvu kitabu cha Hesabu cha KIONGOZI CHA MWALIMU

Ulichokuwa unafanya wewe Madilu hakina utofauti sana na alichofanya mwanadada mmoja tukiwa darsa la tano (jina nimebana, ila kwa sasa ni mke wa mtu). Yeye alikuwa mfagizi wa ofisi ya mwalimu mkuu, sasa mle kwenye ofisi kulikuwa na kikokotoo aina ya Casio. Kwa hiyo yeye alikuwa anaiba kile kikokotoo na kukokotoa mazoezi yote ya hesabu na kututupa mbali sie wakali wa namba darasani, hadi ticha akashtuka, kwa sababu ukokotoaji wake ulikuwa hauna sehemu ya njia, kuonyesha jinsi alivyopata jibu, yaani ni swali na jibu tu!
Alipogundulika ilikuwa soo sana, kwa sababu tulimjua kuwa alikuwa kilaza sana mle darasani.
Noma
 
Mnakumbuka "KITABU CHEUSI???????",iliaminika kabisa ukiandikwa humo wewe utakuwa na maisha mabaya kweeli baadaye. Kuna mshikaji aliandikwa tukiwa darasa la nne tulikuwa tunaogopa hata kutembea naye maana ilionekana atatuambukiza the expected misfortunes......... Kweli tumetoka mbaaaali
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…