Tuliowahi kurogwa tupeane uzoefu

Tuliowahi kurogwa tupeane uzoefu

MI NI MMOJA WA WATU AMBAO SIAMINI KATIKA MASUALA YA UCHAWI.
Ngoja nichukue siti mapema nipate uzoefu
haihitaji kuamini kama yapo.
utakutana nayo mubashara siku ukiingia kwenye 18 zao hao mabingwa.
 
ifike kipindi huu uchawi tuu`advance kwa ajili ya maendeleo endelevu ya mazingira yanayotuzunguka..
ili kila mtu anufaike nao,sio unakuwa mchawi,kazi yako kukaba watu waliojipumzisha baada ya mahangaiko ya kutwa nzima,afu unajisifia uchawi,kweli hili ni bara la giza...ndio maana pia kila kitu kizuri kuhusu dini walikifanya weupe,sisi hatukupigiwa chapuo sababu ya upuuzi wetu.
uchawi mkuu katiba yake ni wivu. Labda wabadilishe watafutiwe katiba mpya.
 
Umenikumbusha chuo kuna mwanafunzi alisimamishwa kujibu swali mbele ya darasa, katika kutoa karatasi mfukoni akadondosha bonge la hirizi, kama kikapu cha sokoni, halafu ye hakushtuka.

Wakati anaaondoka kwenda kukaa baada ya kumaliza yaliyompeleka mbele. Lecture akaliona (Lecture mtu mzima sanaa na alikua mtata kinoma yani). Ila siku hio aliongea kwa upole sana kwa mara ya kwanza, uoga wa kuiona ile POWER BANK ilivyokubwa. Ikabidi amwite kwa upole "Bro umesahau zana yako kwenye stage".

Jamaa hakuonesha nidhamu ya uoga, mdogo mdogo akarudi na kuiokota tena kwa swagger aisee. Ma Lecture/Wanafunzi tulikua tunamuogopa jamaa kama gonjwa la UKIMWI, maana muda wowote unajua ukimzingua kina nuka.

Darasa zima tuliangua kicheko, hatari
Jamaa huyu atakuwa ni nahodha wa ukoo. Mikoba yote anatembea nayo kila kona.
Anaweza kuvumbua bombadia ya kilozi mkuu. Ningekuwa lecturer ningemuhamishia engineering hata kama anasomea shahada ya kuchora katuni.
 
Amina mtumishi wa Mungu. Ukisimama kwenye maombi wachawi wanaanza kukuita wewe ndo mchawi maana unakuwa kwenye viwango vingine ambavyo nao vinawachanganya!!!!! Mungu yupo na anafanya Kazi na wanaomhitaji!!!
mkuu naunga mkono hoja asilimia zote.
Walionje ya Bwana Yesu, na sisi tunaoungaunga tutapata tabu sana.
 
Hao wachawi wakianzisha barbershops watapiga pesa za kutosha, kuliko kuwanyoa watu free of charges.
wakiingia brazil na india wakawanyoa wale wamama wakihindi ile minywele wanaweza kuja kupiga pesa mingi sana.
hasa kwa wale wadada magwiji wa kuvaa mawigi aka Nywele za marehemu.
Tatizo machawi karibu yote majingamajinga hayafikiri nje ya boksi.
 
Kiukweli uchawi upo,na kweli wachawi hurudisha nyuma watu,kimaendeleo.kikubwa kumuomba mungu akuepushe na hawa viumbe wenye tabia mbaya. Wana sumbua ndo mana m/mungu kawahidi kuwachoma moto mkali sana wa JEHANAMA.mshirikinafiinalijehanam.
 
Kiukweli uchawi upo,na kweli wachawi hurudisha nyuma watu,kimaendeleo.kikubwa kumuomba mungu akuepushe na hawa viumbe wenye tabia mbaya. Wana sumbua ndo mana m/mungu kawahidi kuwachoma moto mkali sana wa JEHANAMA.mshirikinafiinalijehanam.
sababu zenyewe za kulogana ni za kijingakijinga tu.
mfano. '' kwa nini anatumia jiko la mkaa wakati sisi tunatumia kuni'' ngoja tumkomeshe.
jinga sana wale binadamu wenzagu.
 
wakiingia brazil na india wakawanyoa wale wamama wakihindi ile minywele wanaweza kuja kupiga pesa mingi sana.
hasa kwa wale wadada magwiji wa kuvaa mawigi aka Nywele za marehemu.
Tatizo machawi karibu yote majingamajinga hayafikiri nje ya boksi.
Tatizo wachawi wa kibongo wanafanya uchawi kujifurahisha tu, wakianza kufanya uchawi kama kazi au sehemu ya kujiingizia kipato wanaweza kufika mbali sana hasa kwenye suala zima la teknologia.
 
Dah kuna mmama aliwahi kunipiga beat nlivyomponza mwanae tukafkuzwa nae shule O level.. alinambia anaweka rozali pembeni kwanza.. sijui ameishia wapi.. nahis bado anavua rozali.
 
Mi wakati nakaribia kumaliza chuo nliamka nkakuta nmenyolewa nywele zimemaliza almost miez 3 bila kuota yani full stress ila now naona ndo zinaota japo sikuwah kwenda kwa sangoma.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom