Kiukweli watu hujiua kutokana na kukosa suluhisho ya kile wanachokiona ni tatizo kwao, ambacho kwa wengine huenda ikawa ni kitu cha kawaida kabisa lakini wao hukiona kama kitu kikubwa sana.
Ndio maana ni vizuri mtu ukiwa na kitu kinakusumbua jaribu kutafuta mtu wa karibu unaemuamini mzee au Kijana mwambie tatizo lako na jinsi linavyokutesa, naamini atakushauri na kukutia moyo.
Pia nawashauri pia wale wanaofuatwa kuombwa ushauri ni vizuri waoneshe ushirikiano kwa watu hao, kuwatia nguvu na moyo, na usikione wanachopitia ni kama kitu cha kijinga sana hasa kwa kujionesha mbele yao.
Kuna mtu anahitaji maneno machache tu ili arudi Kwenye hali yake tena, Kuna mtu anataka kupewa confidence tu ili ajione yuko sawa kama wengine, katika maisha haya nimegundua wengi kuna vitu vinawatesa na wanaumia navyo moyoni either vya kimaumbile au kisaikolojia tu ambavyo wakishauriwa wanaweza kuviona ni vya kawaida.
Imagine kama mleta Uzi alitaka kujiua tu sababu ya Kukojoa kitandani, naamini alikosa mtu wa kumpa confidence na kinyume chake wanafamilia wengi huanza kueneza habari nje, na kumfanya mhusika aathirike vibaya kisaikolojia. Wapo watu huwa wanawaza mbali mpaka kufikia hatua ya kutaka kujiua eti tu sababu Pua yake iko hivi, mdomo wake uko hivi, sura yake iko hivi, mfupi sana, miguu yake....na vitu chungu mzima vya kimaumbile, hii huanzia mashuleni mpaka mitaani.
Ni vizuri tujijengee utaratibu wa kuwafichia siri wenzetu katika familia au mashuleni huko, pengine wewe ni mwalimu unaona mwanafunzi wako anakasoro flani na wenzake humtania, hujui tu ni namna gani mtoto huyo anapitia mateso ya kifikra na kuathiri uwezo wake darasani. Kuna wanafunzi hawatamani kabisa kuja shule sababu ya kutaniwa, anakuja tu basi hana la kufanya lakini concentration yake Kwenye masomo ni ndogo sana, Jitahidi kuwatia moyo watu kama hawa Ndugu mwalimu au mwanajamii yeyote.
Kuna ndugu yako anatatizo fulani ambalo ni la aibu, mtunzie siri usimtangaze, mtie nguvu. Kuna mtu anatatizo flani msaidie, mtie nguvu mpe japo ushauri kama huwezi kumpa pesa au kitu. Kuna watu hujiua sababu tu anadaiwa elfu kumi! Elfu Kumi ni nini ukifananisha na uhai? Pengine alitakiwa mtu wa kumshauri tu labda ukakutane na anayemdai umuombee ampe muda kidogo zaidi, au waandikishane amlipe kidogo kidogo.....
Kiufupi Tujitahidi kutowadhalilisha au kutowanyanyapaa Binaadamu wenzetu, Tuwatie nguvu. Kingine watu wa waliosomea Mambo ya Saikolojia au ushauri wanahitajika sana hawa wawepo na kutushauri kuhusu yale tunayopitia katika maisha yetu ya kila siku.
Sent using
Jamii Forums mobile app