Tuliowahi kunywa sumu tukutane hapa

Tuliowahi kunywa sumu tukutane hapa

Kiukweli watu hujiua kutokana na kukosa suluhisho ya kile wanachokiona ni tatizo kwao, ambacho kwa wengine huenda ikawa ni kitu cha kawaida kabisa lakini wao hukiona kama kitu kikubwa sana.
Ndio maana ni vizuri mtu ukiwa na kitu kinakusumbua jaribu kutafuta mtu wa karibu unaemuamini mzee au Kijana mwambie tatizo lako na jinsi linavyokutesa, naamini atakushauri na kukutia moyo.
Pia nawashauri pia wale wanaofuatwa kuombwa ushauri ni vizuri waoneshe ushirikiano kwa watu hao, kuwatia nguvu na moyo, na usikione wanachopitia ni kama kitu cha kijinga sana hasa kwa kujionesha mbele yao.
Kuna mtu anahitaji maneno machache tu ili arudi Kwenye hali yake tena, Kuna mtu anataka kupewa confidence tu ili ajione yuko sawa kama wengine, katika maisha haya nimegundua wengi kuna vitu vinawatesa na wanaumia navyo moyoni either vya kimaumbile au kisaikolojia tu ambavyo wakishauriwa wanaweza kuviona ni vya kawaida.
Imagine kama mleta Uzi alitaka kujiua tu sababu ya Kukojoa kitandani, naamini alikosa mtu wa kumpa confidence na kinyume chake wanafamilia wengi huanza kueneza habari nje, na kumfanya mhusika aathirike vibaya kisaikolojia. Wapo watu huwa wanawaza mbali mpaka kufikia hatua ya kutaka kujiua eti tu sababu Pua yake iko hivi, mdomo wake uko hivi, sura yake iko hivi, mfupi sana, miguu yake....na vitu chungu mzima vya kimaumbile, hii huanzia mashuleni mpaka mitaani.
Ni vizuri tujijengee utaratibu wa kuwafichia siri wenzetu katika familia au mashuleni huko, pengine wewe ni mwalimu unaona mwanafunzi wako anakasoro flani na wenzake humtania, hujui tu ni namna gani mtoto huyo anapitia mateso ya kifikra na kuathiri uwezo wake darasani. Kuna wanafunzi hawatamani kabisa kuja shule sababu ya kutaniwa, anakuja tu basi hana la kufanya lakini concentration yake Kwenye masomo ni ndogo sana, Jitahidi kuwatia moyo watu kama hawa Ndugu mwalimu au mwanajamii yeyote.
Kuna ndugu yako anatatizo fulani ambalo ni la aibu, mtunzie siri usimtangaze, mtie nguvu. Kuna mtu anatatizo flani msaidie, mtie nguvu mpe japo ushauri kama huwezi kumpa pesa au kitu. Kuna watu hujiua sababu tu anadaiwa elfu kumi! Elfu Kumi ni nini ukifananisha na uhai? Pengine alitakiwa mtu wa kumshauri tu labda ukakutane na anayemdai umuombee ampe muda kidogo zaidi, au waandikishane amlipe kidogo kidogo.....
Kiufupi Tujitahidi kutowadhalilisha au kutowanyanyapaa Binaadamu wenzetu, Tuwatie nguvu. Kingine watu wa waliosomea Mambo ya Saikolojia au ushauri wanahitajika sana hawa wawepo na kutushauri kuhusu yale tunayopitia katika maisha yetu ya kila siku.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilishawahi kupiga mixer ya dozi moja na nusu ya fragile na nusu ya cetrin (sina uhakika kama inaandikwa hivyo) kisha nikashushia bia bingwa. Kabla bia yenyewe sijaimaliza demu wangu akaingia ghetto, aliona siko sawa, halafu pembeni akakuta makaratasi kibao ya dawa basi akajua tayari mana alikua anajua napitia kipindi kigumu mno, akapiga kelele wapangaji wenzangu wakajaa wakaninywesha mchanganyiko wa maji na majivu nikatapika kinoma pale.

Demu akanichukua tukaenda kwake, muda huo m najiona niko sawa tu. Akatuma mtoto wake akanunue maziwa nayo nikapiga huku natapika sio poa. Basi bwana baadae kidogo cha moto ndo nikaanza kukiona, nikawa najisikia hovyo mno yan muda wote nataman niwe natapika. Tumbo linavuruga hatari, mwili hauna nguvu hata kidogo. Sikulala ile siku

Kesho yake mambo yakazidi kuwa hovyo zaidi. Tumbo linauma kinoma yan utafikiri ndani linakatwa katwa, nikienda haja natoa tu vibonge bonge vya damu. Haja ndogo mkojo una mchanganyiko wa damu kama yote asee! Huku hamu ya kula sina nakunywa tu uji. Mungu ambariki yule manzi popote alipo, alinipigania sana. Hali ikaenda hivyo kama siku nne hivi kisha nikawa sawa.

Kamari sio poa jamani, haifai

Sent using Jamii Forums mobile app
demu yuko wapi sasa ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukweli ni kwamba sumu za panya nyingi zinazouzwa hazina madhara kiivyo kwa binadamu. Hata mie nlijaribu pakti 4 tofauti sikufa nliishia kuharisha na kutapika

Nakuja PM mkuu unipe jina na rangi ya hiyo sumu iliyokupelekesha nami niitafute.
uitafute tena ??? kwa nn usione uzuri wa ww kuwa hai mkuu ? nn shida share nasi tunaweza kukusaidia pia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli mkuu unakuta hawajui namna akili inavyovurugika.
Madharau yapo kila mahali! Kuna kipindi nikiwa fresh kiuchumi nilikuwa nikiona mtu anafanya kazi ya mtaji mdogo, nawaza kichwani kimya kimya kwamba mimi siwezi kufanya kazi kama hiyo.
Miaka michache mbeleni nilikuja kuuza matunda kwa mtaji ambao hufikia hata laki tano. Kumbuka nyuma ya hapo nilikuwa nadharau hata kazi ya mtaji mdogo hata wa milioni moja
Hili ni funzo katika maisha usimdharau mtu kwa sababu hujui kesho yake. Maisha hayana kanuni hivyo ni vema kuheshimiana, kusaidiana na kutiana moyo.
 
Nilipitia kipindi kigumu sana kwenye maisha yangu, kigumu mnoo! Nae akawa bega kwa bega na mimi kunisaidia kila hatua (abarikiwe)..shida ni huko alikokua anapata hizo hela, yakawa yaleyale ya Baraka Da Prince na Ruby (Nivumilie Song)

Sent using Jamii Forums mobile app
Daah, kumbe yapo sawa na yale ya Bahati Bukuku. Pole vipi mkuu ulisamehe au ndo, hukukumbukq hata ule wimbo wa Boss wa Feruzi
 
Daah, kumbe yapo sawa na yale ya Bahati Bukuku. Pole vipi mkuu ulisamehe au ndo, hukukumbukq hata ule wimbo wa Boss wa Feruzi
Sikuachana nae kwa ubaya. After all nilikuja kugundua mitazamo yetu imebadilika, wakati mimi bado nafikiria uaminifu ni nguzo muhimu yeye alikua anafikiria kuwa anaweza kuwa na mwingine ambaye kwa madai yake eti hampendi as long as jamaa ana provide yale ambayo mimi siwezi.

Tutafute pesa jamani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh kiongozi pole kwa situation uliopitia na hakika kwa changamoto hizo sidhani kama kuna tatizo ambalo utashindwa kukabiliana nalo maana ni zaidi ya ujasiri.
 
Hii dunia ina mambo yake. Mimi mmoja kati ya watoro wetu wa3 siku anazaliwa nilikuwa nimebakiza buku tu baada ya kumrudisha wife home kutoka hospital. Kwakuwa ilikuwa usiku nikaona sio ishu, atakula kwa ndugu niliyekuwa naishi nae nyumbani. Ili kupunguza zile za "mzazi hali hiki na hiki" nikapotea nyumbani kama masaa mawili huku nawaza asubuhi itakuwaje. Poda, sabuni, nguo za kumshikia mtoto wakati wa baridi, chakula cha mzazi n.k. hapo hata unga hakuna ndani maana uliisha siku moja kabla hajaenda kujifungua. Nikazuga mpaka saa tatu nikasema ngoja nipande home nikalale mimi mwanaume nitajikaza hadi kesho. Lahaula!! Kufika home kachanga kanalia mama mtu anabembeleza lakini ukisikiliza sauti yake ni kama analia pia. Nikawaza imekuwaje, nikabisha mlango nikafunguliwa. Nikauliza kulikoni, wife aliponijibu sikutaka hata kumwangalia maana nilihisi aibu. Aliniuliza "mbna umeondoka bila kuacha hata chakula, nina njaa tangu nilipokula ule mkate mchana hospital sijala mpaka sasa" nikamuuliza kwann hujala si ungekula kwa bro? "Wamepika wakamaliza wakaenda kulia ndani mwao hata hawajanisemesha." Nyumba niliyokuwa naishi ndio hiyohiyo ilikuwa na chumba kinachotumika kama jiko, fikiria nini kilikuwa kikiendelea. Kwa huzuni kabisa nikamwambia wife nina buku hapa na hukoama ntilie wote wamefunga. Akaniambia atakikaza ila maziwa ndio hamna. Asubuhi niliamka mapema sana kuhangaika nione wataishije. Ajabu ni kuwa hakuna aliyejali zaidi ya kuambiwa "usiku tulipika kaugali kadogo tukaona mzazi hatashiba" sikuwajibu. Mungu alisaidia nikajipanga kwa mbinde maisha yakasonga mpaka mtoto akawa mkubwa. Narudia tena NDUGU ZAKO UNAWAPATA WAKATI WA SHIDA. Fikiria mzazi kabisa, hili mpaka nazama chini sitalisahau na huwa namwangalia mtenda nasema yamepita.
Ubaya ni kwamba mtenda yeye huwa anasahau haraka sana. Sahau na kusamehe tu mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilipitia kipindi kigumu sana kwenye maisha yangu, kigumu mnoo! Nae akawa bega kwa bega na mimi kunisaidia kila hatua (abarikiwe)..shida ni huko alikokua anapata hizo hela, yakawa yaleyale ya Baraka Da Prince na Ruby (Nivumilie Song)

Sent using Jamii Forums mobile app
ama kwa hakika kizuri hakikosi kasoro. pole zake na zako maana upendo wake kwako ulifanya aafanye lolote kwa ajili yako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ama kwa hakika kizuri hakikosi kasoro. pole zake na zako maana upendo wake kwako ulifanya aafanye lolote kwa ajili yako.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndo' hivyo mkuu. Nami nakiri kuwa alinipenda, mchawi pesa tu. Vijana tutafute pesa, watu hata mpendane vipi lakini pesa ikikosekana mambo yanaenda kombo. Upendo sio jawabu la kila kitu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom