Tuliowahi kunywa sumu tukutane hapa

Tuliowahi kunywa sumu tukutane hapa

Ngoja niandike kwa kifupi,mwaka 2009 ndo nilimaliza form 4,sikuchagua kwenda form 5 ingawa nilkuwa na ushindi mzuri tu(hii ni kutokana na kutaka kupata hela haraka),nilichagua kwenda chuo cha ufundi arusha tech nikachagua kozi ya mechanical engineering,kufika chuo nkaona kozi hiyo ni ngumu na pia haina dili kitaa ajira zenyewe za shida nkaomba kubadili kozi nichukue electronic and telecommunication engineering wakanikatalia nkaamua nimuache chuo,nkatafuta chuokingine,nkapata chuo cha kilimo Moro nkaenda nkasoma miaka 2 nilipomaliza ajira zikatoka wakaajiriwa wa diploma tu,sie wa certificate(astashahada) tukakosa,nipo home sina ramani nikawa nimeshaanza kuujua ugumu wa maisha,Mara nkasikia tangazo redioni kuwa waliofaulu vizur form 4 wanaweza kusoma bachelor ya ualimu masomo ya sayansi na mkopo unapewa kipindi cha kikwete hicho na kweli mkopo nilipata maisha yakawa matamu lakini wenye chuo walikuwa wahindi wahuni wenye mikopo wanatupa discontinue ili waendelee kupata pesa yako wakati unapokuwa nyumbani,mimi walinikamata kwa somo la kemia,nkarudi nyumban lakin nikawa nimepanga kuwa kabla ya kufika nyumban nitanunua sumu,kufupisha n kwamba nilkunywa sumu hyo nkazimia polini Siku 3,nilzinduka asubuh j2,nkaokotwa na mama mmoja,nilkuwa natembea napepesuka ,yule mama alinipeleka kwa mwenyekiti wa eneo hilo akidai Mimi ni Mwiz wa mihogo,wakakusanyika watu wengne wakdai wanichape vboko lakin mwenyekit alikataa akawa ananitetea anasema huyu anaweza kuwa mvuta bangi tu maana midomo ilkuwa imekuwa na magamba,baadae walinipeleka kituo cha redio jamii,baadae mama akapatikana wakanipeleka moja kwa moja hospital, kila ndugu alkuwa anashangaa kwanza nilvyokonda na kuchakaa,wakati miezi michache nyuma walkuwa wanaona picha zangu mtandaon nikiwa nimenawili,matibabu ilikuwa drip ya maji hadi nilitaman madaktar niwaambie kuwa nilkunywa sumu ili nipewe matibabu zaid lakin nilipewa hayo tu na baada ya SKU 3 nikawa nimeruhusiwa
 
Hii dunia ina mambo yake. Mimi mmoja kati ya watoro wetu wa3 siku anazaliwa nilikuwa nimebakiza buku tu baada ya kumrudisha wife home kutoka hospital. Kwakuwa ilikuwa usiku nikaona sio ishu, atakula kwa ndugu niliyekuwa naishi nae nyumbani. Ili kupunguza zile za "mzazi hali hiki na hiki" nikapotea nyumbani kama masaa mawili huku nawaza asubuhi itakuwaje. Poda, sabuni, nguo za kumshikia mtoto wakati wa baridi, chakula cha mzazi n.k. hapo hata unga hakuna ndani maana uliisha siku moja kabla hajaenda kujifungua. Nikazuga mpaka saa tatu nikasema ngoja nipande home nikalale mimi mwanaume nitajikaza hadi kesho. Lahaula!! Kufika home kachanga kanalia mama mtu anabembeleza lakini ukisikiliza sauti yake ni kama analia pia. Nikawaza imekuwaje, nikabisha mlango nikafunguliwa. Nikauliza kulikoni, wife aliponijibu sikutaka hata kumwangalia maana nilihisi aibu. Aliniuliza "mbna umeondoka bila kuacha hata chakula, nina njaa tangu nilipokula ule mkate mchana hospital sijala mpaka sasa" nikamuuliza kwann hujala si ungekula kwa bro? "Wamepika wakamaliza wakaenda kulia ndani mwao hata hawajanisemesha." Nyumba niliyokuwa naishi ndio hiyohiyo ilikuwa na chumba kinachotumika kama jiko, fikiria nini kilikuwa kikiendelea. Kwa huzuni kabisa nikamwambia wife nina buku hapa na hukoama ntilie wote wamefunga. Akaniambia atakikaza ila maziwa ndio hamna. Asubuhi niliamka mapema sana kuhangaika nione wataishije. Ajabu ni kuwa hakuna aliyejali zaidi ya kuambiwa "usiku tulipika kaugali kadogo tukaona mzazi hatashiba" sikuwajibu. Mungu alisaidia nikajipanga kwa mbinde maisha yakasonga mpaka mtoto akawa mkubwa. Narudia tena NDUGU ZAKO UNAWAPATA WAKATI WA SHIDA. Fikiria mzazi kabisa, hili mpaka nazama chini sitalisahau na huwa namwangalia mtenda nasema yamepita.
Duh! Kuna watu wana roho ngumu sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Biblia imeandikwa "Imani ni kuwa na hakika na mambo yasiyoonekana, ni bayana ya mambo yatarajiwayo." Toba ni kati ya mtu na Mungu. Binafsi naamini hakuna toba ya mtu>mtu>Mungu (sipingani na dini yoyote) kama amefikia hatua ya kueleza, naamini alishatubu mbele za Mungu na kamwe hiyo roho haitaweza kumfuata ten. Sema Amina
Mkuu nimetoa angalizo tu sasa ni juu yake kujitathimini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi sasahivi nilishawaambia hata ndugu. Rafiki yangu kwenye shida hata kama sio ndugu yangu, namuheshimu kuliko hata ndugu wa tumbo moja. Kuna jamaa hatukuwa na urafiki hata ule wa kusalimiana na kwao zipo kidogo, alikuwa rafiki yangu ghafla mpaka kuna muda alikuwa anawatuita mimi wife na watoto tukapige stori kwake maana tulikuwa majiranu (baadaye nimekuja kugundua alikuwa anatuita tukale kiaina maana alikuwa anatuita wakati mkewe akiwa jikoni. Yaani ilikuwa inaanza hv, mkewe akanakuja anamuita wife ampe kampan jikoni ana stori ampe, mara kidogo watoto wanaitana wanaenda kucheza, halafu baadaye unasikia fulani mwite baba aje tukae huku aikae mwenyewe) huyu hata akikosea namsamehe haraka bila hata kuomba msamaha.
Huyu ndiye ndugu wa kweli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wauza sumu ya panya wengine ni matapeli, eti hata akifa panya hanuki.
Kuhusu suala la kukojoa linatesa ( mimi nilishawahi kuwa nalo nilivyokuwa primary. Nikienda kulala kwa ndugu huwa najifikiria. Unaota kabisa mkojo umekubana unaenda chooni kukojoa, unapokojoa unaishia kukojoa kitandani, baadae liliisha tu lenyewe.
Ila sababu hiyo ilikufanya ujiue kuna matatizo makubwa kuliko hayo na watu wanakomaa nayo
Kuna kaka yangu mmoja alikuwa anakojoa kitandani.
Alikuja kuacha akiwa form 4..

Kila kitu kina faida na hasara, faida aliyoipata ni usafi.
Ni msafi Sana,anafua nguo zake muda wote

Kuna muda Mungu anaruhusu Jambo ili ujifunze Jambo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maisha ndio yalivyo, lakin pole sana
mi kuna miaka nilipitia kipindi kigumu ikatikia hatua nikaenda kulala barabarani ili gari inipitie ilikuwa nyakati za usiku,lakin cha ajabu gari lilikuw likifika karbu yangu linasimama dereva na konda wake wanakuja kunitoa na maneno juu."hili lijamaa limelewa pombe za bure".

Maisha ni mtihani mzito ndo maana siwez kumdharau mkubwa au mdogo,

maisha yalitight kinoma had wale wanaokuzunguka huwaoni yan.fikiria mwanaume unamaliza hata week huna buku wala jero mfukoni,root za kijiweni nikapunguza ikawa ni Mimi na kitanda kitanda na mm had mwili ukapungua .

umaskini usikie kwa jirani mana hata wasichana walipotea kwenye anga yangu,inafikia hatua unamtizama msichana yuko uchi ila humuoni.simu yangu ya mkononi ikawa inamaliza hata week 3 Hamna sms yoyote iliyoingia ,nafkiri hata voda walinisusia (kidding).
nakumbuka ilikuwa jmoc asubuh nataka niamke nikachote maji nikapokea SMS ya ujumbe kutoka kwa aliyekuwa kama demu wangu ikisomeka hivi."najua unapitia kipindi kigumu cha maisha ila pambana maisha yapo nakuombea kila la kheri kwa mpenz mwngne utakayempata mi nimeamua niwe single.". Aseeeee hii SMS ilinivuruga nikarudi kitandani nikalala licha ya kutokuw na usingiz tena.

lakini cha ajabu mwaka huo huo kuna Siku nilipishana na jamaa njian macho mekunduu AF mweusii tii.akantoa salam kisha akaniomba aniulize kitu pemben ,kumbe anashida na sehem wanapouza bangi ,nikamjibu yeah napafaham ila inaweza niamin lete ela nikufatie ,jamaa akachomoa buku 5 nikaenda ,kufika njian nikawaza sijui nizame ndichi nmpotezee ila roho nyingine ikasita. Nikaamua kumfatia tu kibish.

Maisha yalivyokuwa sasa baada ya kumletea weeder ,jamaa alitokea kuwa mshikaj knoma akawa anantuma kumbe n dreva wa shirika flan kambini huko kigoma ,miez kadhaa mbele akaniunganisha nikapata job tena mshahara wa kutosha.HADI LEO NIPO HUKU NAKULA LIFE

REST IN PEACE RASTA nakukumbuka kwa mchango wako mkubwa kwenye maisha yangu.

OVER
"Nina certificate ya nursing ila nashindwa kupangilia mwandko"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii dunia ina mambo yake. Mimi mmoja kati ya watoro wetu wa3 siku anazaliwa nilikuwa nimebakiza buku tu baada ya kumrudisha wife home kutoka hospital. Kwakuwa ilikuwa usiku nikaona sio ishu, atakula kwa ndugu niliyekuwa naishi nae nyumbani. Ili kupunguza zile za "mzazi hali hiki na hiki" nikapotea nyumbani kama masaa mawili huku nawaza asubuhi itakuwaje. Poda, sabuni, nguo za kumshikia mtoto wakati wa baridi, chakula cha mzazi n.k. hapo hata unga hakuna ndani maana uliisha siku moja kabla hajaenda kujifungua. Nikazuga mpaka saa tatu nikasema ngoja nipande home nikalale mimi mwanaume nitajikaza hadi kesho. Lahaula!! Kufika home kachanga kanalia mama mtu anabembeleza lakini ukisikiliza sauti yake ni kama analia pia. Nikawaza imekuwaje, nikabisha mlango nikafunguliwa. Nikauliza kulikoni, wife aliponijibu sikutaka hata kumwangalia maana nilihisi aibu. Aliniuliza "mbna umeondoka bila kuacha hata chakula, nina njaa tangu nilipokula ule mkate mchana hospital sijala mpaka sasa" nikamuuliza kwann hujala si ungekula kwa bro? "Wamepika wakamaliza wakaenda kulia ndani mwao hata hawajanisemesha." Nyumba niliyokuwa naishi ndio hiyohiyo ilikuwa na chumba kinachotumika kama jiko, fikiria nini kilikuwa kikiendelea. Kwa huzuni kabisa nikamwambia wife nina buku hapa na hukoama ntilie wote wamefunga. Akaniambia atakikaza ila maziwa ndio hamna. Asubuhi niliamka mapema sana kuhangaika nione wataishije. Ajabu ni kuwa hakuna aliyejali zaidi ya kuambiwa "usiku tulipika kaugali kadogo tukaona mzazi hatashiba" sikuwajibu. Mungu alisaidia nikajipanga kwa mbinde maisha yakasonga mpaka mtoto akawa mkubwa. Narudia tena NDUGU ZAKO UNAWAPATA WAKATI WA SHIDA. Fikiria mzazi kabisa, hili mpaka nazama chini sitalisahau na huwa namwangalia mtenda nasema yamepita.
Duu,pole sana,nimeguswa aisee
 
Twin angu alijiua kwa sumu..ikanisumbua balaa hiyo hali..! Ilinisumbua kwasababu toka tunazaliwa hatujawahi achana naye hata kwa lisaa...pia dada yangu nayemfata zilikua haziivi..nilikua nampiga balaa...bas akaambiwa asicheze na mimi..kwahyo na mimi kwa hasira nikama nikamblock...sikumjali kabs ni dada au ndugu..mdogo wangu wa mwisho nimeachana aye miaka mingi sana naye nikawa namuona mtoto..so mtu niliyeamua kuwa naye benet ni twin wangu sikua mtu wa marafikia

Alipojiua wenyeji wakaanza kusema akifa pacha mmoja mwingine hachukui round! Ile hali ikawa inaniboa sana.alafu hom wakawa kama wamenitenga fulani( walikua wananiogopa maana niligeuka kama kichaa kbs..nilikua natembea na panga naona kila mwanafamilia ndo chanzo cha twin kujiua!) Two months later nikaamua kunywa piriton 20! Nilienda tu dispensary nikasema mama kanituma umpe piriton ..nikanywa zote...lol.niliamka niko hosp! Na drip za kutosha..nakumbuka nililala tu sema tumboni kulikua kunavuruga! Sikufa...! Nikapewa mshauri akaniweka sawa kias chake .since then sijapata mawazo hayo .!Mungu alinipa utashi tena!rip B!
Dooh!

Hadi mchozi umenitoka, ila inauma asikwambie mtu
 
Mimi sasahivi nilishawaambia hata ndugu. Rafiki yangu kwenye shida hata kama sio ndugu yangu, namuheshimu kuliko hata ndugu wa tumbo moja. Kuna jamaa hatukuwa na urafiki hata ule wa kusalimiana na kwao zipo kidogo, alikuwa rafiki yangu ghafla mpaka kuna muda alikuwa anawatuita mimi wife na watoto tukapige stori kwake maana tulikuwa majiranu (baadaye nimekuja kugundua alikuwa anatuita tukale kiaina maana alikuwa anatuita wakati mkewe akiwa jikoni. Yaani ilikuwa inaanza hv, mkewe akanakuja anamuita wife ampe kampan jikoni ana stori ampe, mara kidogo watoto wanaitana wanaenda kucheza, halafu baadaye unasikia fulani mwite baba aje tukae huku aikae mwenyewe) huyu hata akikosea namsamehe haraka bila hata kuomba msamaha.
Wamebaki wachache sana wa hivi
 
Yaani nawaza nicomment nini lakini kila nachoandika nafuta. Haya maisha ukiona mtu anakuja kukucheka sababu ya hali yako ama akaonesha dharau kwa maamuzi yoyote ambayo ulitaka/uliyafanya ukiwa na hali ngumu, ujue hayajui maisha kabisa. Pole sana mkuu, ila hope sasahv uko vzr. Mimi bado nina visa kadhaa ila nhoja nichaji simu kwanza kisha nitaandika kisa kingine ambacho kilijirudia zaidi ya mara moja.
Aaah wapi hakuna mtu ambae hapitii shurubu kwenye hii dunia hakuna, sema watu wengine wanajifanyaga hawana shida au tatizo

Na hao ndo hujiua ghafla au maradhi ya moyo
 
Aaah wapi hakuna mtu ambae hapitii shurubu kwenye hii dunia hakuna, sema watu wengine wanajifanyaga hawana shida au tatizo

Na hao ndo hujiua ghafla au maradhi ya moyo
Naamini katika kila tatizo la mwenzako kuna cha kujifunz. Katu sipendi mtu anayejifanya haijui shida. Wanaume hufa mapema kuliko wanawake kwakuwa maumivu yao huyaficha. Wakati wanawake hulia hata hadharani
 
Back
Top Bottom