S V Surovikin
JF-Expert Member
- Aug 8, 2015
- 13,620
- 32,730
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, ni kwamba katika maisha tunakutana na changamoto ambazo wakati mwingine huwa kubwa kwelikweli, au huwa kubwa kulingana na mhusika atakavyoitafsiri changamoto yenyewe ndani ya ubongo wake kitu ambacho hupelekea mhusika kukata tamaa kwa asilimia zote hadi kuona bora kufa kuliko kuendelea kuishi.
Wengine huwa ni changamoto za kutatulika lakini hushindwa kuchukua hatua stahiki kutokana na ujinga au kutokana na kuathirika kisaikolojia kutokana na muda wa changamoto husika.
Sasa basi naomba nisimulie kisa changu kilichonipelekea kutaka kuutoa uhai wangu ndani ya Dar es Salaam na kingine ndani ya Kilimanjaro, japo katika visa vyote sikufanikiwa na ndio maana nipo hai hadi muda huu.
Ieleweke thread kama hizi ni kuwasaidia wengine wenye wanaopita matatizo kama ya waliotangulia, ili wasikate tamaa bali wajue ni hatua gani za kuchukua ili watoke kwenye matatizo waliyonayo na mwisho wabaki wakiusifu na kufurahia uzuri wa kazi za Mungu aliye chanzo chao.
Twende kwenye kisa cha kwanza ambacho almanusra kiondeke na uhai wangu!
Nilipomaliza elimu ya msingi moja kwa moja nikatakiwa kwenda kwa shemeji kufanya kazi ya kuuza kitimoto Arusha huku nikiendelea kusubiri matokeo, lakini safari yangu nilikuwa na wasiwasi maana nilikuwa na tabia ya kukojoa kitandani, sasa nikawa nawaza huko mjini nitakaaje na hii tabia yangu?
Nikajipa moyo tu potelea mbali liwalo na liwe. Sasa nilipofika Arusha, kwa bahati nzuri sikupangiwa kulala na yeyote ila nilipangiwa nitakuwa nalala kwenye makochi ofisini.
Kwa kifupi pale niliishi kijanjajanja na tabia yangu hiyo japo mbeleni waliijua tabia yangu ila wakawa wananisitiri tu 👏👏👏
Mdogomdogo mara nikafaulu kwenda kidato cha kwanza lakini sikukubali kuendelea na shule japo nilibembelezwa sana lakini nikawa sitaki kabisa. Hivyohivyo mpaka ilipotimu mwezi wa 7 mwaka 2010 kaka yangu akapiga simu kwa dada Arusha sasa katika kumsalimia akataka niende Dar nikakae dukani. Ile kaka kutaka niende Dar kulinichanganya kabisa mpaka nikaanza ujeuri kazini maana nilitaka niache kazi shemeji na dada wakakataa sababu nilikuwa nimeshakuwa mtu wa muhimu na mzoefu pale ofisini.
Kweli nilizidisha ujeuri hadi wakayasikia madai yangu wakanilipa changu nikasepa.
Nakumbuka nilipita kwanza nyumbani Rombo nikiwa na kiasi kama laki tatu na chenchi ila mpaka naondoka nilikuwa nimebakiwa na 125,000 wakati nilikaa siku tatu tu nyumbani.
Baada ya siku tatu mimi huyoo Dar es Salaam. Nilitoka asubuhi saa kumi na mbili lakini tulienda kufika saa mbili usiku kwa sababu kuna gari lilipata ajali mbele yetu kulekuke Rombo kabla hata hatujafika mashati. Nilipofika Ubungo nikapokewa na jamaa wa tax aliyetumwa na kaka ndio akanipeleka hadi dukani. Nilipofika nakumbuka tulisalimiana tu akaniingiza dukani usiku uleule. Kuna laki moja ilibaki mfukoni baada ya kutoa nauli nikampa aniwekee mimi nikaendelea na kazi yeye akaketi hapo mlangoni akinielekeza bei ya vitu na namna ya kufanya kazi maana ndio ilikuwa mara yangu ya kwanza kuuza dukani.
Sasa bahati yangu nikawa nalala kwenye chumba changu mwenyewe tena, hivyo ikawa chansi ya kuficha aibu yangu ya kukojoa kitandani maana nilikuwa nikitandika nailoni usiku na asubuhi nalificha.
Kipindi hicho tulikuwa tandika ila baada ya miezi michache akahamia kwake Tabata, hivyo ikawa nikifunga duka tunalala sehemu moja!😬
Kimbembe kikaanza. Kipindi hicho nilikuwa najitahidi hata sinywi soda hovyohovyo na maji hasa ile mida ya jioni kuelekea usiku lakini wapi! Nilikuwa nikijitahidi sana naweza kukosa siku 2 ndani ya wiki. Mambo yakawa magumu kwangu.
Lile jambo liliniathiri kisaikolojia kwa wakati huo kuliko wakati mwingine wowote tangu kuzaliwa. Nimajiona sifa na nikaanza kulaumu kwanini hata nilizaliwa?
Yani nalala na mtu msafi, asiyependa uchafu, nyumba safi, kitanda kisafi, mashuka masafi, nina akili timamu lakini nakojoa kitandani? Nikawa sina amani na mawazo ya kutaka kujiua yakaanza kumea kwenye akili yangu maana nilijiona nikifa nitakuwa na amani na hakuna chochote kitakachoendelea.
Kaka alikuwa hapendi kabisa hiyo tabia yangu na tangu utotoni alikuwa hapendi
Kadri siku zilivyokuwa zinaenda mimi nikawa naanza kufikiri mbinu nzuri ya kuniondoa chapu, ilipofika mwezi wa pili mwaka wa 2011, nakumbuka siku hiyo nilifata bia na baiskeli nikakutana na jamaa anatembeza sumu za panya, mende, kunguni nk; nikamsimamisha nikamuuliza sumu ya bei ghali kabisa ni sh ngapi? Akajibu kuwa ni buku.
Nikamwuliza sifa zake akasema hiyo sumu huua panya fasta na akishakufa hanuki. Sikuongea sana nikamwambia anifungie.
Niliporudi dukani nikaendelea na mambo yangu kama kawaida huku lengo langu likiwa ni kwenda kujiulia mbali na eneo la nyumbani. Kesho yake asubuhi nikadamka nikaenda kwenye kimsitu fulani kiko pale Tabata kisukuru kwa pembeni sijui eti ni wa jeshi, maana mission yangu ilipofeli kule, muda wa kutokea barabarani kuna mbaba aliniambia we mtoto unafanya nini kwenye huo msitu wa jeshi?
Sasa baada ya kuingia kwenye hicho kimsitu nikapanda juu ya mikorosho huku nikifikiria namna nitakavyoingia makazi mapya ambayo ni ya kufikirika zaidi. Baada ya muda nikaibugia ile sumu yote ambayo ilikuwa kama vile vitambi vya kwenye packet ndogondogo.
Baada ya kuibugia nikashuka zangu juu ya ule mkorosho ili nisije kuanguka saa ya kufa. Nikakaa pale chini ya mti muda mrefu bila kuhisi chochote ndio nikaamua kutafuta njia ya kutoka ndani ya ule msitu baada ya njaa kuwa kali kwenye mida ya saa nane mchana, nikatokeza barabarani ndio huyo dingi akakutana na mimi akaniuliza, wee mtoto umetoka kufanya nini ndani ya huo msitu wa jeshi? Nikamwambia nimetoka kujisaidia.
Tukaachana mimi nikaelekea na njia ya kupandia Tabata migombani ili nikavizie chakula dukani kwa rafiki wa kakaangu ambaye pia ni rafikiangu ili nikampange endapo akiulizwa na kaka nilikuwa wapi aseme nilikuwa kwake. Kweli mpango wangu ukaenda fresh ila misheni yangu ya kuwahi kwa father God ikafeli.
Niliporudi kwa kaka nikamkuta anapambana na kazi huku anafua mashuka niliyokojolea usiku huo kitendo ambacho kiliniumiza mara dufu. Katika kuniuliza nilikoamkia asubuhi nikamdanganyadanganya ikabidi anivungie tu sababu akishaanza kuona kama dishi lango haliko poa.
Tukaendelea vizuri tu shetani wangu akawa ndio kanikomalia vizuri yani hata asubuhi najikuta nakojoa kitandani kama mtoto mdogo wakati mimi ni mkaka wa miaka 20 kabisa. Hazikuisha hata wiki mbili nikanunua sumu nyingine ya panya nikainywea bafuni muda ambao nilikuwa mwenyewe usiku lakini yenyewe niliitapika tu wala sikuhisi chochote kibaya wala nini.
Nikaona huu sasa ni uduanzi, kesho yake mchana nikashuka ile sumu ya kuulia mbu nikaipulizia kwenye kikombe alafu nikaenda kununua sindano zile za mahospitalini nikainyonya kwa ile sindano kisha nikajidunda mguuni alafu nikaionja kidogo lakini matokeo yake pale nilipojidunda pwlivimba alafu pakawa panauma sana lakini sikupatwa na tatizo lingine.
Nilitokewa na kidonda lakini kilipona chenyewe bila hata mtu kujua Mwezi wa tatu mwaka huohuo nikaenda kununua sumu nyingine ya panya ambayo ni kapakt kadogo sana kalikofungwa na karatasi mbili, nikakaweka kwenye juice fulani zilizokuwa zinaitwa juice za glass au pride juice nikanywa usiku wa saa tano ambapo muda huo kaka alikuwa anakunywa bia na marafiki zake kibarazani nje ya duka.
Ile nimeinywa tu nikahisi kuzunguzngu na dalili ya kutapika, nikajikaza nikatoka kama naenda kuoga na nilipofika nyuma ya nyumba tu nikatapika chakula chote cha mchana alafu nikaishiwa nguvu kiasi. Nikadaka ukuta nikadondokea kwa jamaa mmoja ambaye muda mwingi anakuwa hayupo nyumbani huja usiku kwa usiku na usiku huo alikuwa ameshalala ila mimi nikadondokea pembeni kidogo ya gari lake nikawa natapika maji na kujiharishia mfululizo mpaka nikaishiwa nguvu kiasi kwamba nilikuwa nikitazama balbu iliyokuwa juu yangu naiona kama imesambaa.
Muda mfupi baadae nasikia kaka akiita hadi kwa baadhi ya majirani akiniulizia maana niliacha ndoo ya kuogea kule na sabuni kule bafuni alafu hajui nilipo na ni usiku sana.
Akawa anahangaika bahati nzuri baadaye sijui alifikiria nini akapanda juu ya ule ukuta akaniona, akaja fasta akamwamsha na yule jirani huku mimi nawasikia tu ila siwezi kufanya chochote hata kutoa sauti au kukunja hata kidole cha mkono siwezi.
Wakaja mbiombio wakaenda kuleta mabarafu wakaniwekea ila nikawa hata sitingishiki ila masikio yangu yakawa yanasikia kuliko kawaida. Mara nasikia wakisema, ameshakufa, hahemi huyu, kafanyaje? Nini kimemkumba?.
Basi nilishangaa kaka akisema amekunywa sumu huyu. Kauli ile ilinishtua japo nilikuwa marehemu 90% Wakashauriana mara wakanibeba wakanitupa kwenye gali wakaniwahisha hospitali ya amana, lakini katika kunibeba kule kote nilikuwa naelewa nimebebwa lakini sihisi/yani mwili wangu ulikuwa hauhisi chochote tena hata walinifinya nikajua nimefinywa lakini sikuhisi maumivu.
Kufika amana nikapokelewa fasta nikawekewa maji tu kumbukumbu zikakomea pale hadi asubuhi nilipozinduka nimezungukwa na marafiki wa kaka wengi na mirija ya maji.
Kila mtu akawa anataka kujua nilipatwa na nini lakini nikasema sielewi ilikuwaje.
Kikubwa pale nilipona bila bata kutumia dawa tofauti na maji niliyowekewa.
Kingine nilipotoka hospitali nilipoteza uwezo wa kuonja kwa muda wa karibu mwezi mzima na kuna namna nilikuwa nikiisikia ile harufu ya sumu kwa muda huohuo ikaja kupotea Kifupi kaka alihonga pale nisipelekwe polisi kwa kosa la kujiua ndio tukaondoka. Sasa mpaka leo najiuliza madaktari na kaka walijuaje nimekunywa sumu?
Sijawahi kupata jibu ila mwaka 2016 ndio nilimwambia kaka ukweli.
Tatizo la kukojoa kitandani lilikuja kuisha baada ya kuacha mchezo wa kujichua, na hii niligundua baada ya kukaa muda wa mwezi sijajichua likaisha lenyewe ndio nikajua kumbe ndio dawa ya tatizo.
Na nashukuru baada ya kujua nilikuwa nakojoa kitandani kwa sababu ya kujichua kulikopitiliza, ilibidi niache huo mchezo mara moja!
Kisa cha pili nitakileta maana vidole vimechoka kutyp
KISA CHA PILI KIPO COMMENT YA 43