Mimi sasahivi nilishawaambia hata ndugu. Rafiki yangu kwenye shida hata kama sio ndugu yangu, namuheshimu kuliko hata ndugu wa tumbo moja. Kuna jamaa hatukuwa na urafiki hata ule wa kusalimiana na kwao zipo kidogo, alikuwa rafiki yangu ghafla mpaka kuna muda alikuwa anawatuita mimi wife na watoto tukapige stori kwake maana tulikuwa majiranu (baadaye nimekuja kugundua alikuwa anatuita tukale kiaina maana alikuwa anatuita wakati mkewe akiwa jikoni. Yaani ilikuwa inaanza hv, mkewe akanakuja anamuita wife ampe kampan jikoni ana stori ampe, mara kidogo watoto wanaitana wanaenda kucheza, halafu baadaye unasikia fulani mwite baba aje tukae huku aikae mwenyewe) huyu hata akikosea namsamehe haraka bila hata kuomba msamaha.