Nilishawahi kupiga mixer ya dozi moja na nusu ya fragile na nusu ya cetrin (sina uhakika kama inaandikwa hivyo) kisha nikashushia bia bingwa. Kabla bia yenyewe sijaimaliza demu wangu akaingia ghetto, aliona siko sawa, halafu pembeni akakuta makaratasi kibao ya dawa basi akajua tayari mana alikua anajua napitia kipindi kigumu mno, akapiga kelele wapangaji wenzangu wakajaa wakaninywesha mchanganyiko wa maji na majivu nikatapika kinoma pale.
Demu akanichukua tukaenda kwake, muda huo m najiona niko sawa tu. Akatuma mtoto wake akanunue maziwa nayo nikapiga huku natapika sio poa. Basi bwana baadae kidogo cha moto ndo nikaanza kukiona, nikawa najisikia hovyo mno yan muda wote nataman niwe natapika. Tumbo linavuruga hatari, mwili hauna nguvu hata kidogo. Sikulala ile siku
Kesho yake mambo yakazidi kuwa hovyo zaidi. Tumbo linauma kinoma yan utafikiri ndani linakatwa katwa, nikienda haja natoa tu vibonge bonge vya damu. Haja ndogo mkojo una mchanganyiko wa damu kama yote asee! Huku hamu ya kula sina nakunywa tu uji. Mungu ambariki yule manzi popote alipo, alinipigania sana. Hali ikaenda hivyo kama siku nne hivi kisha nikawa sawa.
Kamari sio poa jamani, haifai
Sent using
Jamii Forums mobile app