Tuliowahi 'kuchungulia kaburi' tukutane hapa

Tuliowahi 'kuchungulia kaburi' tukutane hapa

Mimi nakumbuka vyenye nilipata ajali ya piki piki hapo Makumbusho nikitokea kwenye shughuli ya kuaga mwili wa classmate wa o'level alafu nawahi kupiga paper mahali.

Ilikua ni split-second event, nikajikuta katikati ya lami, mbele ya daladala kwa chini, derava wa daladala anatoa kichwa dirishani anauliza umeumia. Sikumjibu nikainuka hapo kila mtu ameduwaa magari yote yamesimama nikasogea pembeni nikamuona boda nae kainuka akachukua chombo chake akasoge nilipokuwa akaniuliza vipi umeumia.

Sikuumia hata kidogo wala mchubuko sikupata japo pikipiki ili slide pale kwenye lami kama mita 10 hivi. Boda nae hakuumia watu wanatuangalia tu akawasha chombo nikadandia hao tukasepa mwendo wa kidosi tukawaacha watu wasijue chakufanya.

Hii siku nilikua na rafiki yangu ambae yeye alishatangulia na boda yake, kufika namwelezea story ilivyokuwa mpaka leo huwa anabisha maana sikuwa na hata ushahidi wa jeraha zaidi ya vumbi vumbi kwenye jeans.
Haha eti hao mkasepa mkawaacha wasiwe na cha kufanya
 
Aisee kuna wakati Mungu anakutetea hadi mwenyewe unashindwa kuamini macho yako
Acha asee nilifika home kuwaambia nimepata ajali wakaanza kupigiana simu zisizoisha wanataka niende hospital nikacheki nikakataa kata kata maana hawakuamini kama sijaumia kwa jinsi tukio nilivyowaeleza.
 
Daah inanikumbusha miaka 1996 nikiwa Mpanda, kipindi hicho nikiwa Secondary ili kila inapofika ijumaa nilikua natoroka kwenda machimboni kwakua kipindi hicho hela ilikua inapatikana kirahisi sana.

Nilikua nikifika huko naingia kwenye shimo lenye urefu wa zaidi ya mita ishirini, chini kabisa nilikua naingia ndani ya "fonka " liliokaa mfano wa chumba ambalo ndio nakwenda kuchimba katika mkondo wenye Dhahabu nyingi.

Kwakua nilihitaji pesa nilizoea kufanya shughuli hiyo kwa siri na sikutaka mtu yeyote shuleni na nyumbani ajue kama naendaga machimboni kwasababu nilikua bado mwanafunzi.

Siku moja tulipata jiwe kubwa la dhahabu na baada ya mgao nilipewa milioni 12 malipo ya mwanzo ila kutokana na umri wangu ilikua ni nyingi sana na siku hiyo niliamua kwenda kumpa dada angu aniwekee kisha nikarudi kwa kusubiria hela nyingine.

Tukiwa ndani walikuja jamaa wakiwa na silaha wakitaka wapewe pesa zote, watu walikula bakora siku hiyo ni balaa. Kuna brother mmoja nakumbuka alijisaidia pale pale. Mimi nilitumbukizwa kweny pipa la maji ikawa kila napotoa kichwa nje nakutana na kibao cha kichwani narudi kwenye maji,ilifikia muda nikapoteza fahamu nimekuja kupata fahamu jamaa wamechukua kila kitu lakini bahati yangu ni kwamba hela nilikua nishazipeleka kwa dada angu.

Pamoja na hayo sikuacha kwenda katika uchimbaji na kipindi hicho nikanunua kipimo cha zahabu ambazo zinapatikana juu juu ya kwenye ardhi nikawa naingiza pesa kwenye mashine na kwenye mashimo marefu niliendelea ku- hustle kama kawaida.

Siku moja nikiwa ndani ya shimo chini kabisa udongo ulikua ukiporomoka na maji yalikua yameanza kujaa hivyo nikawa nachota maji naweka kwenye ndoo kisha inavutwa maji yanamwagwa nje ya shimo lakini wakati shughuli inaendelea ulibomoka ukuta na kurudisha ndoo chini,mimi niliona giza ghafla hivyo nikakimbilia kwenye chumba cha shimo ambako nako hakuna njia ya kutokea. Hewa ilikua inapita lakini maji yalikua yakizidi kuongezeka hivyo nikajua lazima nife.

Kwamba mbaaali sana nilikua nasikia sauti za watu wakigombana kwamba waite polisi ndipo waje waanze kutoa udongo Lakin kuna jamaa yangu mmoja siji kumsahau, yeye alikataa akawaambia wachimbe kwanza wautoe mwili ndipo waite polisi kwasababu wakiacha muda mrefu bila kuwahi kuutoa mwili maji yanaweza kuwa mengi alafu ikawa shida ndipo kazi ikaanza.

Nashukuru Mungu kuna mmoja wao aliona mwanga wa tochi yangu kupitia kitundu kidogo sana,akawaeleza wenzake kwamba nitakua mzima kwasababu kama ningekua nimepoteza uhai tochi ingezama kwenye maji na isingetoa mwanga hivyo wakapiga kazi kwa kufuata mwanga mdogo wa tochi.

Kuna muda nikawa naita ila kwasababu ya kishindo cha sululu ya kuchimbia wakawa hawasikii baada ya muda walitoboa tundu angalau hewa ikaongezeka na tukawasiliana vizuri hadi nilipo okolewa kutoka kwenye fonka hiyo.

Tangu siku hiyo sikutaka kusikia tena habari za machimbo. Huko roho mkononi maana kazi ngumu, hatari ni nyingi na bado ukipata vihela kidogo majambazi wanakuvizia.
Duuh hadi nimesisimka ulikuwa na uthubutu sana aisee
 
Namkumbuka miaka ya 90 mwishoni mwishoni huko kipindi nikiwa kijijini kwa babu huko migombani migombani moshi, kipindi hicho nikiwa kwenye level ya juu kabisa ya utundu na ukurofi, yaani nikiambiwa kitu mi nafanya kinyume chake, yaani chochote kilicho hatarishi mi ndo akili ilinituma nicheze nacho, sumu sumu za kahawa hizi zilishanifanyia booking kama mara 2 hivi Ila safari zikaahirishwa, nyuki nao hawana adabu kabisa, tena hawa nyuki wa kwenye mapango mapango ni washenzi sana . ila hii kupenda penda asali nayo bana daaaah!! alikufa ng'ombe mi nikapelekwa hospitali,
Sasa kuna siku moja bana, nakumbuka ilikuwa kipindi cha kiangazi nimerudi zangu kutoka skuli jua kali mbaya halafu nina njaa kama ya wiki hivi, nyumbani sioni mtu na hakuna dalili na jikoni pamenuna, nikaona isiwe tabu nikachukua zangu manati nikazama migombani. Kwenye pitapita zangu huko kwenye mikahawa na migomba nikaona kapapai kapo juuu kule karibia kabisa na izraeli mtoa roho anakoishi, shetani alivyo mwehu akaniambi "wewe ni mwanaume panda faster" nikavua chachacha zangu kiroho safi, nikaanza kupanda, daaaah! Kumbe kale kapapai kalikuwa mtego sijui ndo chambo bana! mpapai wenyewe ni ile mipapai sijui ni ya enzi gani maana imekaakaa kama ile minazi ilopandwa enzi za sultan Said sayeed kule zanzibar. Nikajitutumua mtoto wa kiume, shetani nae ananambia "pambana", nikajivuta mtoto wa kiume, shetani nae anakazia "Nenda..." nikafika katikati kuna matawi, nikakaa kwenye tawi nikapumzika, baada ya kama dk 5 safari ikaendelea, mtoto wa kiume nikapambana mzee, nikajikunja mwanaume, nikajivuta sana, shetani nae anakazia "twende tu" daaah, nikafika kwenye vitawi vya pili nikapumzika tena, shetani akanipa wazo, "hebu simama ujaribu kama utafikia, nikasima nikajinyooosha lakini wapi! Nikajivuta lakini wapi...!!
Nyie!!. Shetani mhuni sana, nikakumbatia mpapai nikaendelea na safari, nikajituma sana, nikajinyoosha sana tu, aisee!! Daaah nikafika! Daaaah nikaukumbatia mpapai kwa nguvu then nikakanyoosha mkono wa kushoto nichukue nilichofata, aisee nyie watu. Nakumbuka tu sauti ya kukatika Ule mti wa mpapai Ila baada ya hapo sijui nini kiliendelea. Hadi leo mapapai huwa sili.
[emoji28][emoji28][emoji28] shetani mmbaya!!
 
Hahaha ndio umesusa kabisa na kula mapapai??? Pole sana boss ila nimependa jinsi ulivyosimulia
 
aaah nimekupata mkuu
Tehteh..mama kumbe karibia ufwe?

Bwana mimi Kwa wanaoijua Galanos basi watanijua na usinitaje labda nicheke PM.

Bendera ya ule mlingoti pale mbele ilinasa pale juu kwenye kitundu ule mlingoti ni mrefu saana. Chini ni mnene juu ni mwembamba.

Sasa ikabidi atafutwe mtu anayeweza kupanda miti na na mdogo mdogo mwenye uzito mkubwa ataanguka nao.

Nikaitwa kamvua kalikuwa kananyesha ila kakawa kamekata..na inabidi tuitoe maana mkuu wa wilaya soon anakuja. Nikapanda ila kwa shida saana maana chokaa ikiwa na majimaji huteleza.

Ile nimefika juu na kuishika bendera kumbe kuna zenge la nyingu limefunda hapo. Lote likanizingira na kunin'gata ila sikuiachia bendera nikateleza nayo chini nikaanguka "Paaa".

Mkuu wa shule aliogopa akajua nimefariki maana dakika 20 sijielewi. itaendelea.
 
Tukio
Mwaka 1998 home kulikuwa na mfumo wa kuwasha taa za nje bila switch za ukutani, yaani kulikuwa waya ambao kuna kichwa cha Miguu miwili bana unachomeka kwa multi plug ambayo iliwekwa juu kidogo watoto wasifike na wakubwa wanruhusiwa kuwasha na kuzima (chomeka Chomoa). Siku hiyo nimebaki home mwenyew imefika jioni Giza linaingia likanijia wazo kupanda pale juu ili niwashe (ni chomeke) nikachukua stuli ili nifikie vizuri, kumbe Miguu ya ile plug yote ni chuma Tupu bwana, sasa kidole kimoja kimegusa kwenye moja ya vile vichuma na switch ilikuwa on bwana ile natumbukiza tu nilipigwa shot moja hiyo nilitetemeshwa na jasho kunitoka balaa kulegea juu nilijikuta sakafuni 😂
 
Out of topic...

Niliwahi kuota ndoto enzi zile za msiba wa Nyerere. Ndoto yenyewe ilikua hivi;

Kulikua na watu kama wawili hom na mzee wa tatu na mimi wa nne. Kukawa na jeneza limehifadhiwa kwenye verendah ya nyumba (lilinunuliwa kama akiba emergency na mzee) sasa tupo sebuleni tunaangalia tv mzee akakohoa kidogo tu mara ya kwanza.. mara kidg akakohoa tena mara mbili nikaona wale watu wawili wamembeba mzee na kumlaza kwenye jeneza(hakuwa amekufa). Na ndoto ikaishia hapo.

Sijaelewa mpaka leo hii ndoto ilimaanisha nn ingawa mzee yupo mpaka leo na hana tatzo lolote.

Mungu zidi kumlinda.
Amini ilikuwa ndoto tu mkuu
 
Tukio
Mwaka 1998 home kulikuwa na mfumo wa kuwasha taa za nje bila switch za ukutani, yaani kulikuwa waya ambao kuna kichwa cha Miguu miwili bana unachomeka kwa multi plug ambayo iliwekwa juu kidogo watoto wasifike na wakubwa wanruhusiwa kuwasha na kuzima (chomeka Chomoa). Siku hiyo nimebaki home mwenyew imefika jioni Giza linaingia likanijia wazo kupanda pale juu ili niwashe (ni chomeke) nikachukua stuli ili nifikie vizuri, kumbe Miguu ya ile plug yote ni chuma Tupu bwana, sasa kidole kimoja kimegusa kwenye moja ya vile vichuma na switch ilikuwa on bwana ile natumbukiza tu nilipigwa shot moja hiyo nilitetemeshwa na jasho kunitoka balaa kulegea juu nilijikuta sakafuni [emoji23]
[emoji23] [emoji23] [emoji23] pole mkuu
 
Kumchungulisha mtu kaburi [emoji23][emoji23]

Nilikuwa chuo, demu mmoja rafiki yangu akanifuata anaomba nimuangalizie matokeo yake, nikamwambia nilishaangalia tangu nilivyokuwa home nikamzingua ana sup 3 na kama hajazi clear atakuwa amesha disco, akaniambia niseme ukweli, nikachomoa 50k nikampa kuwa tunaangalia kama akikua hana sup na hajaclear achukue hiyo ela

Mamaa weee, demu alirusha hela chini akaanza kukimbia kumbe ana maradhi yake hatakiwi kuhema kwa haraka, kufika room kwake kazimia, wanampepea akizinduka anasema “...(anataja jina langu) kasema “hamaliziii anazima tena, kuanzia saa 6 mchana alikuja ku recover saa moja jioni, niliiona jela hii hapa na mzaha nikapunguza
 
Hahahaa aisee wewe una vitimbwii yaani nimecheka kama mwehu usiku huu wa manane. Ulihurumiwa sana haukupelekwa hata auxiliary police?
 
Hahahaa aisee wewe una vitimbwii yaani nimecheka kama mwehu usiku huu wa manane. Ulihurumiwa sana haukupelekwa hata auxiliary police?

Nilinunua glucose za kutosha, napiga simu kama nina mgonjwa icu, ma juice, nikifika naambiwa kazinduka mda si mrefu...hayo masaa yalikuwa marefu sana [emoji23][emoji23], all in all nimepitia mengi ya ujana, hawakunipeleka maana hata hao roommates zake ni rafiki zangu walikuwa wananionea huruma tuu
 
Back
Top Bottom