Tuliowahi 'kuchungulia kaburi' tukutane hapa

Tuliowahi 'kuchungulia kaburi' tukutane hapa

Out of topic...

Niliwahi kuota ndoto enzi zile za msiba wa Nyerere. Ndoto yenyewe ilikua hivi;

Kulikua na watu kama wawili hom na mzee wa tatu na mimi wa nne. Kukawa na jeneza limehifadhiwa kwenye verendah ya nyumba (lilinunuliwa kama akiba emergency na mzee) sasa tupo sebuleni tunaangalia tv mzee akakohoa kidogo tu mara ya kwanza.. mara kidg akakohoa tena mara mbili nikaona wale watu wawili wamembeba mzee na kumlaza kwenye jeneza(hakuwa amekufa). Na ndoto ikaishia hapo.

Sijaelewa mpaka leo hii ndoto ilimaanisha nn ingawa mzee yupo mpaka leo na hana tatzo lolote.

Mungu zidi kumlinda.
 
Mie utundu wote nimefanya utotoni nikiwa kwa babu kijijini tulikuwa tukienda kuchunga mifugo tunawatomba mifugo.!
Nilikuwa naenda na stuli ili kupandia juu
Khaa we ulishindikana unabeba na stuli kabisa hawakuwa wanakuuliza stuli unaenda nayo wapi
 
Umenikumbusha nikiwa mtoto bwana nililia kumbikumbi acha zidakwe nikaangiwe Nile, acha nianze kutapika had nikaishiwa nguvu kabisa, tangu siku hyo sipendi kumbi kumbi, kisa kingine nilikuwaga mtundu niliye kubuhu acha nitumbukie kisimani nikiwa mtoto sijui hili wala lile nikaja kuokolewa na wenzangu. Aisee kikubwa mimi nimepitia mengi na kunusurika kifo mara nyingi sana. Namshukuru Mungu dunia hii siji kuondoka had niwe mbibi na mkongojo
Hahaha kumbe utundu ulianza muda enhe
 
Moshi town kukatwa na sime

Hii nayo ingenisababisha niage dunia, mshkaji wangu kabisa tulikorofishana, aliiba kitu home kwetu nikawa ninamwambi arudishe ugomvi ukaanzia hapo, iyo siku amerudisha nipo home nikamwambia mwanzo na mwisho kukanyaga home, ghetto nilikuwa nina sime ya kimasai jamaa aliivuta kaniletea shingoni nikahepa kidogo ikanichubua mpaka leo nina alama, ilienda kutua kwenye ukuta kwa namna ilivyo chimba ukuta isingeniacha salama
Aisee pole I guess na utafiki uliishia hapo
 
Moshi town kukatwa na sime

Hii nayo ingenisababisha niage dunia, mshkaji wangu kabisa tulikorofishana, aliiba kitu home kwetu nikawa ninamwambi arudishe ugomvi ukaanzia hapo, iyo siku amerudisha nipo home nikamwambia mwanzo na mwisho kukanyaga home, ghetto nilikuwa nina sime ya kimasai jamaa aliivuta kaniletea shingoni nikahepa kidogo ikanichubua mpaka leo nina alama, ilienda kutua kwenye ukuta kwa namna ilivyo chimba ukuta isingeniacha salama
Aisee pole I guess na utafiki uliishia hapo
 
Dodoma kipigo cha mbwa koko

2010, dodoma kulikuwa kuna bash royal village dogo wangu akanitunuku rafiki zake wawili niende nao, walikuwa wamevaa ovyo, party ikaisha mda wa kuondoka tunatoka nje tunaelekea kweny gari mob ikaanza kuwavuta wale mademu, ikabidi nikimbie fasta kuchukua gari mademu nimewaacha na mshkaji wangu wamezongwa zongwa, kurudi pale wademu wameingia mmoja seat ya mbele mwingine kakaa nyuma na mchizi, kufumba na kufumbua mob imezingira gari wanataka mademu, mara kioo kimevunjwa mlango umefungulia mademu wanavutwa wamebebwa juu juu ndio kushuka na mimi kwenda kuwaokoa, ebanaeeee nilichezea kichapo siyo cha nchi hii, nilichoropoka nikarudi hotelini, gari la aunt yangu nyang’a nyang’a, demu mmoja aliokolewa na mabaunsa mwingine aliliwa mtungo vichakani
Duuh jamani
 
Bwana Yesu asifiwe kwa wale wenzangu na mimi. Wengine habari zenu?

Ninapoelekea kutimiza miongo kadhaa ya kuwepo hapa duniani nimejikuta natafakari maisha yangu tangu pale nilipoanza kupata akili hadi leo hii nimejikuta natabasamu na kumshukuru sana Mungu maana nimekutana na mengi mazuri, mabaya, ya kukatisha tamaa ila katika yeye anitiaye nguvu nimeyaweza yote na nitaendelea kuyaweza yote.

Nimejikuta nakumbuka tukio moja la huko nyuma nikiwa na miaka sita hivi au saba (sikumbuki exactly ilikuwa mwaka gani). Mimi bwana nilikuwa naishi na sister tangu nikiwa mdogo sana na mpaka leo ukisikia nasema naenda nyumbani maana yake naenda kwa sister (naonekana kituko si eti eeh?)..tuachane na hayo kwanza.

My sister miaka hiyo alikuwaga mwalimu vijiji vya ndani kabisa huko, akiwa anaenda kuchukua mshahara anatumia siku tatu..siku ya kwanza kwenda, siku ya pili anaitumia kuchukua mshahara na kufanya mambo yake na hakukuwa ATM miaka hiyo kwa hiyo unaweza kupata picha na siku ya tatu anaitumia kurudi na wakati mwingine alikuwa anaweza kutumia hata siku nne.

Siku hiyo kabla hajasafiri alinunua kumbikumbi (wenyeji wa mikoa ya nyanda za juu kusini mtakuwa mnazijua, nilikuwa nazipenda sana) basi nilizifakamia zile ndude kama ugomvi, nilizikula kama lita moja hivi. Asubuhi ameamka zake hana hili wala lile akaondoka, mimi mida ya saa moja asubuhi nikaanza kuendesha, baadae nikaanza kutapika matapishi ya njano (mnaitaga nyongo sijui).

Kwa hiyo ikawa ni mwendo wa kuharisha na kutapika, sijui dawa yoyote na hata akili ya kwamba niende kwa jirani nikamwambie hali yangu nikawa sina sijui ndio utoto? Inafika mida ya saa nne mtoto nimechoka nikalala kwenye mkeka nje siwezi tena kusimama nikawa natapika hapohapo sina hata nguvu ya kusimama tena yaani nikawa nikifumbua macho hivi naona kila kilichopo mbele yangu kinazunguka. Ni miaka mingi imepita lakini picha ya siku ile haijawahi kunitoka.

Bahati nzuri akaja rafiki yake sister alikuwa hajui kama kasafiri ndio kunikuta katika hali hiyo akanibeba kunipeleka kwake maana kile kijiji hakikuwa hata na dispensary hadi kijiji cha jirani ... yule dada alikuwa anaitwa Fausta (RIP). Ndio ikawa pona yangu na sister alirudi baada ya siku tatu. Huwa najaribu kutafakari hivi asingekuwa yule dada kuja pale sister angenikuta niko hai kweli?

Tangu siku hiyo hakuwahi kuniacha peke yangu akisafiri maana siku zote nilikuwa najifanya konki siogopi kulala peke yangu. Tena wale wadudu niliwachukia jumla jumla sijawahi kuwala tenaa.

Kama na wewe mdau ulishawahi kupitia ugonjwa au hali yoyote ukaona kifo hiki hapa karibu tushee
Pole sana mkuu Kumbikumbi wana mafuta mengi kwa hiyo ukila wengi lazima tumbo likuchenjie
 
Poleee sana,

Kwa upande wangu, kuna simbilis moja almanusra inifanye nipak vitu vyangu niondoke duniani, shenzi sana, mapenzi haya


Anyway.. tuyaache hayo

miaka ya Nyuma kidogo hapo, nikiwa kama standard three hv au two, nikiwa kwa babu mzaa mama moshi vijijin huko, siku moja nimepanda juu ya mti wa mmerez, (kwa wanao ifahamu hii miti ukiwa umekomaa n mrefu sana) nilikua naupunyua matawi, bwana wee huku na huko nimekata tawi lina kama V hv, hiyo V si ikaja ikanivaa shingon kama tai hv... nilijaribu kulivua weee lakn wapi, huku na huko wapi (nilikua bado mdogo, chini ya miaka 10) so uamuz wa haraka ukanijia nijiachie tu nidondoke nalo, nikaachia panga likatangulia kwanza... Yaan ilitokea kama miujiza vile, ile nataka kujiachia tu likanivuka lenyewe, niko hoi bin taaban hapo, nguvu zenyewe zalisha anza kuisha, nikashuka nikaenda kulala
Hahahaaaa pole mkuu
 
Mwaka 2008 nikiwa Standard 7, Tulienda kufanya mitihani ya Jumamosi shule ya msingi KALOBE Mbeya Mjini

Hapo tulikutana shule zaidi ya 10 kufanya paper moja la kujipima na tulifanya hivyo kila jumamosi lakini kwa kubadili badili shule ya kufanyia kwa malipo ya shilingi 300.

Sasa baada ya Kufanya paper zetu, huwa tulikuwa tunacheza mpira na michezo mingine tukisubiri TOKEO.

Mimi na majamaa mengine kutoka Mixture ya shule mbalimbali tukawa tunacheza TOBO DUNDA Halafu ukipigwa TOBO inatakiwa ukimbie ukamshike Demu mmoja alikuwa anaitwa Grace ILI Uepukane na Kipigo kitakatifu kutoka kwa MASELA.Kwahiyo tuliita TOBO DUNDA, SHIKA GRACE

TUMEcheza tumecheza, Wahuni wakanipiga TOBO, Dah kile kipigo nilipewa na maraia kutoka shule ya 10 siji kukisahau.

Nilikong’otwa kweli kweli mpaka wakaacha wenyewe maana nilikuwa napigiwa kwenye Dawati baada ya kukimbia toka uwanjani nikimSaka Grace nimshike nipone Kipondo.

Nilikuja kushtuka baadae nimelazwa kwenye nyasi na marafiki zangu napewa maji ninywe.

Wale Jamaa zangu walinisindikiza mpaka home nikiwa na Nundu Kama Zote usoni na Damu puani na mdomoni.

Baada ya kufika Home Mzee nae akaniongezea Stiki za kutosha kukazia.

Siji kusahau maana nilipigwa Kama Mwizi Aisee.

Mpaka kesho ,mtoto wangu acheze michezo yote lakini TOBO DUNDA AACHANE NAYO
Hahaha michezo mingine bwana
 
Daah inanikumbusha miaka 1996 nikiwa Mpanda, kipindi hicho nikiwa Secondary ili kila inapofika ijumaa nilikua natoroka kwenda machimboni kwakua kipindi hicho hela ilikua inapatikana kirahisi sana.

Nilikua nikifika huko naingia kwenye shimo lenye urefu wa zaidi ya mita ishirini, chini kabisa nilikua naingia ndani ya "fonka " liliokaa mfano wa chumba ambalo ndio nakwenda kuchimba katika mkondo wenye Dhahabu nyingi.

Kwakua nilihitaji pesa nilizoea kufanya shughuli hiyo kwa siri na sikutaka mtu yeyote shuleni na nyumbani ajue kama naendaga machimboni kwasababu nilikua bado mwanafunzi.

Siku moja tulipata jiwe kubwa la dhahabu na baada ya mgao nilipewa milioni 12 malipo ya mwanzo ila kutokana na umri wangu ilikua ni nyingi sana na siku hiyo niliamua kwenda kumpa dada angu aniwekee kisha nikarudi kwa kusubiria hela nyingine.

Tukiwa ndani walikuja jamaa wakiwa na silaha wakitaka wapewe pesa zote, watu walikula bakora siku hiyo ni balaa. Kuna brother mmoja nakumbuka alijisaidia pale pale. Mimi nilitumbukizwa kweny pipa la maji ikawa kila napotoa kichwa nje nakutana na kibao cha kichwani narudi kwenye maji,ilifikia muda nikapoteza fahamu nimekuja kupata fahamu jamaa wamechukua kila kitu lakini bahati yangu ni kwamba hela nilikua nishazipeleka kwa dada angu.

Pamoja na hayo sikuacha kwenda katika uchimbaji na kipindi hicho nikanunua kipimo cha zahabu ambazo zinapatikana juu juu ya kwenye ardhi nikawa naingiza pesa kwenye mashine na kwenye mashimo marefu niliendelea ku- hustle kama kawaida.

Siku moja nikiwa ndani ya shimo chini kabisa udongo ulikua ukiporomoka na maji yalikua yameanza kujaa hivyo nikawa nachota maji naweka kwenye ndoo kisha inavutwa maji yanamwagwa nje ya shimo lakini wakati shughuli inaendelea ulibomoka ukuta na kurudisha ndoo chini,mimi niliona giza ghafla hivyo nikakimbilia kwenye chumba cha shimo ambako nako hakuna njia ya kutokea. Hewa ilikua inapita lakini maji yalikua yakizidi kuongezeka hivyo nikajua lazima nife.

Kwamba mbaaali sana nilikua nasikia sauti za watu wakigombana kwamba waite polisi ndipo waje waanze kutoa udongo Lakin kuna jamaa yangu mmoja siji kumsahau, yeye alikataa akawaambia wachimbe kwanza wautoe mwili ndipo waite polisi kwasababu wakiacha muda mrefu bila kuwahi kuutoa mwili maji yanaweza kuwa mengi alafu ikawa shida ndipo kazi ikaanza.

Nashukuru Mungu kuna mmoja wao aliona mwanga wa tochi yangu kupitia kitundu kidogo sana,akawaeleza wenzake kwamba nitakua mzima kwasababu kama ningekua nimepoteza uhai tochi ingezama kwenye maji na isingetoa mwanga hivyo wakapiga kazi kwa kufuata mwanga mdogo wa tochi.

Kuna muda nikawa naita ila kwasababu ya kishindo cha sululu ya kuchimbia wakawa hawasikii baada ya muda walitoboa tundu angalau hewa ikaongezeka na tukawasiliana vizuri hadi nilipo okolewa kutoka kwenye fonka hiyo.

Tangu siku hiyo sikutaka kusikia tena habari za machimbo. Huko roho mkononi maana kazi ngumu, hatari ni nyingi na bado ukipata vihela kidogo majambazi wanakuvizia.
DAHHH Aiseee pole sana mkuu.....
 
Namkumbuka miaka ya 90 mwishoni mwishoni huko kipindi nikiwa kijijini kwa babu huko migombani migombani moshi, kipindi hicho nikiwa kwenye level ya juu kabisa ya utundu na ukurofi, yaani nikiambiwa kitu mi nafanya kinyume chake, yaani chochote kilicho hatarishi mi ndo akili ilinituma nicheze nacho, sumu sumu za kahawa hizi zilishanifanyia booking kama mara 2 hivi Ila safari zikaahirishwa, nyuki nao hawana adabu kabisa, tena hawa nyuki wa kwenye mapango mapango ni washenzi sana . ila hii kupenda penda asali nayo bana daaaah!! alikufa ng'ombe mi nikapelekwa hospitali,
Sasa kuna siku moja bana, nakumbuka ilikuwa kipindi cha kiangazi nimerudi zangu kutoka skuli jua kali mbaya halafu nina njaa kama ya wiki hivi, nyumbani sioni mtu na hakuna dalili na jikoni pamenuna, nikaona isiwe tabu nikachukua zangu manati nikazama migombani. Kwenye pitapita zangu huko kwenye mikahawa na migomba nikaona kapapai kapo juuu kule karibia kabisa na izraeli mtoa roho anakoishi, shetani alivyo mwehu akaniambi "wewe ni mwanaume panda faster" nikavua chachacha zangu kiroho safi, nikaanza kupanda, daaaah! Kumbe kale kapapai kalikuwa mtego sijui ndo chambo bana! mpapai wenyewe ni ile mipapai sijui ni ya enzi gani maana imekaakaa kama ile minazi ilopandwa enzi za sultan Said sayeed kule zanzibar. Nikajitutumua mtoto wa kiume, shetani nae ananambia "pambana", nikajivuta mtoto wa kiume, shetani nae anakazia "Nenda..." nikafika katikati kuna matawi, nikakaa kwenye tawi nikapumzika, baada ya kama dk 5 safari ikaendelea, mtoto wa kiume nikapambana mzee, nikajikunja mwanaume, nikajivuta sana, shetani nae anakazia "twende tu" daaah, nikafika kwenye vitawi vya pili nikapumzika tena, shetani akanipa wazo, "hebu simama ujaribu kama utafikia, nikasima nikajinyooosha lakini wapi! Nikajivuta lakini wapi...!!
Nyie!!. Shetani mhuni sana, nikakumbatia mpapai nikaendelea na safari, nikajituma sana, nikajinyoosha sana tu, aisee!! Daaah nikafika! Daaaah nikaukumbatia mpapai kwa nguvu then nikakanyoosha mkono wa kushoto nichukue nilichofata, aisee nyie watu. Nakumbuka tu sauti ya kukatika Ule mti wa mpapai Ila baada ya hapo sijui nini kiliendelea. Hadi leo mapapai huwa sili.
Mkuu kwan papai n mti....? Unapanda vp mpapai.. ?
 
Kumbe ndio wewe. Pole chif
Mwaka 2008 nikiwa Standard 7, Tulienda kufanya mitihani ya Jumamosi shule ya msingi KALOBE Mbeya Mjini

Hapo tulikutana shule zaidi ya 10 kufanya paper moja la kujipima na tulifanya hivyo kila jumamosi lakini kwa kubadili badili shule ya kufanyia kwa malipo ya shilingi 300.

Sasa baada ya Kufanya paper zetu, huwa tulikuwa tunacheza mpira na michezo mingine tukisubiri TOKEO.

Mimi na majamaa mengine kutoka Mixture ya shule mbalimbali tukawa tunacheza TOBO DUNDA Halafu ukipigwa TOBO inatakiwa ukimbie ukamshike Demu mmoja alikuwa anaitwa Grace ILI Uepukane na Kipigo kitakatifu kutoka kwa MASELA.Kwahiyo tuliita TOBO DUNDA, SHIKA GRACE

TUMEcheza tumecheza, Wahuni wakanipiga TOBO, Dah kile kipigo nilipewa na maraia kutoka shule ya 10 siji kukisahau.

Nilikong’otwa kweli kweli mpaka wakaacha wenyewe maana nilikuwa napigiwa kwenye Dawati baada ya kukimbia toka uwanjani nikimSaka Grace nimshike nipone Kipondo.

Nilikuja kushtuka baadae nimelazwa kwenye nyasi na marafiki zangu napewa maji ninywe.

Wale Jamaa zangu walinisindikiza mpaka home nikiwa na Nundu Kama Zote usoni na Damu puani na mdomoni.

Baada ya kufika Home Mzee nae akaniongezea Stiki za kutosha kukazia.

Siji kusahau maana nilipigwa Kama Mwizi Aisee.

Mpaka kesho ,mtoto wangu acheze michezo yote lakini TOBO DUNDA AACHANE NAYO
 
Kwa wale wanaojua flow ya maji ya mto, kuna mahala ambako unakuta maji yanarotate kwa speed ya ajabu, sehemu hii huwa na kina kirefu mnoo ni kama shimo refu katikati ya mkondo wa maji.

Kuna siku tukawa tunavuka eneo la hivi kwa kuruka upande mmoja kwenda mwingine kupitia mawe. Ile naruka keenda upande wa pili nikateleza nakuzama pale kati. Nilizinduka baada ya masaa mawili nikiwa nimezungukwa na ndugu na jamaa hosp.

Ila inshort wanasema ni muujiza tu maana rafiki zangu niliokuwa nao walikaa pale kwa dkk nzima niibuke nikaibuka mara ya 1 wakashindwa nidaka ya 2 pia wakashindwa ya 3 wakafanikiwa ila nikiwa sipumui kabisaa.

Yaliyoendelea ni kazi ya Mungu.
Daah pole sana boss
 
Mimi nakumbuka vyenye nilipata ajali ya piki piki hapo Makumbusho nikitokea kwenye shughuli ya kuaga mwili wa classmate wa o'level alafu nawahi kupiga paper mahali.

Ilikua ni split-second event, nikajikuta katikati ya lami, mbele ya daladala kwa chini, derava wa daladala anatoa kichwa dirishani anauliza umeumia. Sikumjibu nikainuka hapo kila mtu ameduwaa magari yote yamesimama nikasogea pembeni nikamuona boda nae kainuka akachukua chombo chake akasoge nilipokuwa akaniuliza vipi umeumia.

Sikuumia hata kidogo wala mchubuko sikupata japo pikipiki ili slide pale kwenye lami kama mita 10 hivi. Boda nae hakuumia watu wanatuangalia tu akawasha chombo nikadandia hao tukasepa mwendo wa kidosi tukawaacha watu wasijue chakufanya.

Hii siku nilikua na rafiki yangu ambae yeye alishatangulia na boda yake, kufika namwelezea story ilivyokuwa mpaka leo huwa anabisha maana sikuwa na hata ushahidi wa jeraha zaidi ya vumbi vumbi kwenye jeans.
Aisee kuna wakati Mungu anakutetea hadi mwenyewe unashindwa kuamini macho yako
 
Back
Top Bottom