FAJES
JF-Expert Member
- Oct 29, 2017
- 714
- 628
Kama unavyojua buana, ukizaliwa kijijini enzi hizo, ni shida sana kufaulu kwenda Sekondari miaka hiyo ya 2000 mwanzoni mwanzoni maana enzi hizo shule za kata zilikuwa bado hazijaanza.
Sasa ukifanikiwa kufaulu lazima kijiji kizima kijue. Mungu ni mwema buana, akatujalia na akina sisi wa mavumbini tukafaulu na kwenda kusoma soma mpaka tukatoboa kufikia vyuo vikuu.
Shida ikaanza pale Babu yangu alipokuwa akiniasa kabisa kuwa nisipendelee sana kurudi kijijini wakati wa likizo. Na akawa anasema kuwa ikitokea nimerudi basi nisikae sana na nikitaka kuondoka nisipendelee kuaga watu wengi na wala nikitaka kwenda kijijini wakati wa likizo nisiwe natoa taarifa.
Yanai niwe nafanya kushtukiza tu. Kwakweli nilipata wakati mgumu sana kumuelewa Babu yangu ila ndio hivyo akishasema inabidi kutii.
Nina dhani jambo hilo linahusiana na imani za kishirikina. Japo Babu yangu alianza kuwa mtu wa Church ukubwani kuelekea uzeeni ila bado naona alikuwa anafahamu na kuamini sana mambo mengi kuhusu tunguri.
Bahati mbaya mpaka Babu anafariki sikufanikiwa kukaa naye na kumuuliza kwa undani kuhusu kauli zake enzi hizo. Vipi wewe Babu ama Bibi yako amewahi kukwambia jambo kama hili? Unaweza ku-share?