Swahili AI
JF-Expert Member
- Mar 2, 2016
- 6,183
- 46,729
Habari Wakuu, nakuja mbele yenu kuomba ushauri, japo nimepata shauri mbalimbali za hapa na pale kwa watu wa karibu na wa mbali niliowahi kukutana nao.
Nianze na historia yangu kwa ufupi. Nilizaliwa mwanzoni mwa miaka ya 90.
Mama alizalia nyumbani kwao wakati bado ni mwanafunzi, haikua rahisi kwa maelezo yake kwa jambo la kubeba mimba ili hali walikua jamii maskini na wapo watoto 7 kwa wakati huo japo wamezaliwa wengi zaidi ya hao.
Ilifika kipindi walimfukuza nyumbani na kuenda kukaa kwa mama mmoja mpaka alipojifungua.
Miaka hiyo ya 90 mwanzoni nikiwa bado mdogo aliolewa kwa ndoa na mwanamume mwingine ambaye sio baba mzazi.
Hakika ndoa ilikua ya kifahari maana sio kwa picha hizo nilizoona kwenye albamu ya picha enzi hizo. Sherehe ilifana sana.
Mwaka 1997 ulitokea ugomvi mkubwa kati ya mama na baba wa kambo, mama aliamua kuondoka na kurudi kijijini ila hakufikia kwa baba na mama yake ila kwa rafiki yake kipenzi wa kusoma nae.
Nakumbuka rafiki yake na mama alikua akiiuza baa maarufu hapo kwenye hiyo wilaya, ambapo alitupa chumba kimoja wapo cha wageni ili tujihifadhi hapo.
Siku moja nikiwa nacheza nje na watoto wenzangu, babu alipita na kuniona maana palikuwa na maarufu na babu alikuwa mtumishi wa serikali hivyo akitoka kupokea mshahara dirisha la halmashauri basi hupita kwenye hiyo baa na kupata kinywaji.
Aliponiona akauliza mama yuko wapi?
Watoto hua hatuna siri, basi nikajibu yupo ndani. Kisha babu akaondoka zake. Jumapili nilimuona bibi ghafla akimsihi mama waondoke nae kurudi nyumbani.
Nakumbuka siku hiyo nilitembea umbali mrefu sana hadi tukafika kwa babu na bibi. Tulikaa hapo kwa muda wa siku 7, na nilikua nasoma darasa la 1, hivyo nilikua naenda shule ya jirani ili nisikose masomo, babu aliomba kwa mkuu wa shule nisome hapo.
Jumapili ya hilo wiki baba wa kambo alikuja kutuchukua na land rover 109.
Tukarudi mjini. Maisha yakaendelea japo nilikua mtoto sio vyote nakumbuka.
Nakumbuka siku moja tulijipata nyumbani kwa msimamizi wa ndoa ya baba wa kambo na mama. Sikumbuki kwanini. Nilikaa pale kwa muda mrefu huku nikiendelea na masomo yangu ya darasa la 2.
Tarehe 31 Desemba 1999 tulihamia kwenye nyumba aliyojenga baba wa kambo nje kidogo ya mji.
Mambo yalizidi kuwa mabaya, ugomvi ulishamiri kwa miaka mingi sana japo mama hakuwa anaondoka tena kurudi kwao, maana yake alipambana na hali yake maana hapo familia iliongezeka na kufikia idadi ya watoto wa 3 ambapo wa 2 walikua ni wa baba wa kambo
Kipindi chote cha utoto baba mzazi alikuwa anakuja kwa mwaka mara moja kuniona shule ya msingi na tulipiga picha na kwenda sehemu za mjini na kula vizuri. Nakumbuka baba mzazi nilikua namuita mjomba. Maana watoto niwaropokaji. Japo alikuwa akinunua zawadi kwa ajili yangu, mama alizificha au kugawa ili kulinda ndoa yake.
Ilifika hatua yale maisha ya ugomvi na amani kukosekana nyumbani, mama aliondoka ghafla bila kujua alipokwenda.
Ikumbukwe kwa miaka yote hiyo, hakuna mtu alitetamka kwamba nina baba mzazi ambaye yupo sehemu fulani, so kwa utoto ule nilijua baba wa kambo ndie baba mzazi. Hata majina ya shule nilitumia ya kwake.
Tusonge mbele zaidi, nilipofika advanced level, form 5 na 6 nilianza kwenda nyumbani kwa baba mzazi na mawasiliano yalipamba moto kwa kipindi hiki. Nilikua namiliki simu so ilikua rahisi kuwasiliana.
Baba mzazi alinieleza sababu kwanini hakumuoa mama, na akaoa mwanamke mwingine. Sikua huru sana wakati nipo kwa baba mzazi na ukizingatia maam wa kambo yupo maana ni mazingira mageni kwangu.. Uzuri ni kwamba nilikaa kwa baba mzazi kipindi cha likizo fupi tu.
Tuendelee mbele zaidi.
Kwa sasa ni mwajiriwa wa serikali, baba mzazi amekwisha staafu na baba wa kambo alikua mfanyabiashara lakini kwa sasa kasi na uwezo umepungua na hana msaidizi kwakua mwanae wa kwanza kwa mama ni mlemavu na wa pili bado anasoma chuo.
Kwa sasa nipo kwenye kipindi cha kuhitajika na wote, baba mzazi na wa kambo kwenye mambo mbalimbali.
Mfano nimeshindwa kufunga ndoa kisa baba wa kambo kutaka mama arudi kwanza nyumbani baada ya kuachana miaka 13 iliyopita.
Ndugu wa baba mzazi wamekua wakinitambua na kunishirikisha kwenye mambo mbalimbali ya kifamilia sasa, na kuna baadhi ya vitu baba wa kambo anavijua na vingine havijui na hii ni kutokana na ukaribu na urafiki wangu na baba yeyote nitakavyoona.
Mfano; baba wa kambo ni mshirikina kwenye biashara zake, hivyo sijawahi mueleza kuhusu watoto niliyozaa, japo baba mzazi anawajua wote.
Niwaombe ushauri wana jamvi, nisimame na yupi kwa sasa?
Pili, mimi sio mwandishi mzuri hivyo muniwie radhi.
Tatu, nipo tayari kutoa ufafanuzi mzuri endapo kuna mahali hapajaelewekaa vizuri.
Nia nikupata ushauri.
Asanteni na karibuni