Kama wewe ni mwanamke pitia hapa

Chawa Namba Moja

New Member
Jan 2, 2024
3
2
Wakuu habari,

Natumaini mko salama na mapumziko ya weekend ya leo.Leo nitapenda ku shere ushuhuda wangu kuhusu wanawake wanaosumbuka kupata watoto na wengine hambao wamekata tamaa kabisa ya kuzaa

Nakumbuka miaka ya 1990 na kuendelea nikiwa mdogo tukiishi pamoja na Bibi yangu kizaa Mama. Sikuweza kuelewa sana wakati huo maana nilikuwa mdogo na akili ya kutambua mambo pia ilikuwa ni ndogo pia,lakini ambacho nilikuwa nikiona kwa macho wakati huo ni Bibi kutembelewa sana na wanawake.

Haiwezi kupita siku nyumbani ujaona wanawake kuanzia 5 na kuendelea na wakati mwingine wakija kina mama wenye uwezo mkubwa na magari ya kifahari na watoto wao wakiwa na zawadi mbalimbali na kumpatia Bibi yangu.

Kitu ambacho Bibi yangu alipenda kuliko vyote ni wajukuu wake,na miongoni mwa wajukuu zake mimi ndo nulikuwa mjukuu wa kwanza kupitia binti yake ambae ni Mama yangu mzazi.Kwaiyo kaliba kila kitu alikuwa anapenda kuniambia na zawadi zilizokuwa zinaletwa na kina mama wale kwakweli tulikuwa tunafaidi sana
Wakati huo Bibi umri ulikuwa umekwenda sana kwaiyo kuna baadhi ya kazi zake alikuwa akinituma sometimes tunaenda nae porini kwa ajiri ya kumsaidia kutafta miti flani ambayo alikuwa akitumia kuwa tibu wa mama wenye matatizo ya uzazi.

Lakini kitu ambacho kilikuwa kinanipa maswali mengi ni pale mkienda nae porini kumsaidia kuchimba miti ni aina flani ambayo sikuelewa ni ilichukua muda kuja kuniambia maana yake.Ni kwamba akikwambia mjukuu wanga chukua jembe na panga twende huku,unajua tu mnaenda porini kuchimba dawa,lakini mkifika porini ambako kuna mti husika atakwambia nisubiri hapo mita kadhaa yeye atatangulia na muda kidogo atakuita fulaniiii.... njoo unisaidie kuchimba,sasa mimi hali ile kwakweli sikuweza kuelewa nini alikuwa akimaanisha? na nilikuwa nabaki na mshangao tu na maswali mengi.

Basi kila akikwambia twende porini utaratibu ukawa ni ule ule tu,kuna siku ikabidi nimuulize hivi kuna nini? maana tukifika porini unaniacha pale badaa unaniita kuja kuchimba ni kwanini?

Jibu likawa ni kwamba muda ukifika nitakwambia tu mjukuu wangu.

Basi mimi kazi yangu kubwa ilikuwa nj kuhakikisha miti tunayochimba niikaushe vizuri na pia ikisha kauka ninaitwanga inakuwa unga na kumkabidhi yeye,pia alinielekeza jinsi ya kuchonga kijiti kidogo na kukitoboa katikati na kukiwekea uzi mweusi hapo sikujua kijiti hicho kilikuwa na kazi gani hasa.

Niseme ukweli kama ni mema ya nchi mimi mjukuu wake niliyala sana,maana wakati huo shule mimi nilikuwa sipungukiwi kibubu cha kununua vitu shuleni kama vile vibumunda, sukari gulu, kashata nk. Hata wanafunzi wenzangu shuleni wakati wa mapumziko walipenda kucheza na mimi karibu sana wakijua watapata chochote.

Kwakweli kadiri siku zilivyokuwa zikienda nyumbani watu walikuwa wengi,na walikuwa ni wanawake tu,Swali langu nikawa najiuliza hivi hawa wanakuwaga na matatizo gani? na jee vipi kuhusu kile kijiti ninacho kichonga na kukiwekea uzi mweusi kinafanyana kazi gani?

Siku zikaenda nakumbuka kabla ya bibi kuanza kuugua mara kwa mara kuna siku aliniita chumbani kwake akanikaliza akaniambia mjuuku wangu leo nataka nikueleze jambo hata siku nikifa basi uweze kuundeleza kuwasaidia watu.

Alianza kwa kuniambia wanawake unao waona hapa wengi wanashida ya uzazi na wengine wamefungwa na mizimu ya mababu zao na wengine wakibeba mimba zinatoka na hata wengine wamelogwa.

Kwaiyo unao waona wakienda na kurudi na zawadi basi hayo ni matunda ya kazi hii.

Alitoa kama kamfuko flani hivi ndani yake kuna sindano na uzi na vijiti vile nilivyokuwa na msaidia kuchonga alafu akatoa na mfuko ukiwa na zile dawa ambazo zimesagwa zikawa unga nizile ambazo tulikuwa tukienda nae kuchimba.

Basi akatoa chini ya godoro lake sarafu mbali mbali nakumbuka wakat ule zilikuwa ni sarafu za Shilingi tano,shilingi kumi zilikuwa ni sarafu nyingi sana.

Akaanza kuniambia unaona hizi ela, kabla ya kwenda kuchimba dawa kule porini ni sharti uchukue moja ya salafu unaiweka mfukoni mwako unaondoka. Hakikisha wakati unaelekea uko usizungumze na mtu yeyote hadi ufike eneo lilipo ule.mti,ukifika hapo kwenye huo mti toa ile salafu na utasema maneno haya. Kisha idondoshe pale kwenye ule mti na kisha anza kuchimba mizizi yake au kuukata.

Kama umeenda mtu,hakikisha anabaki maali fulani baada ya wewe kuwa umeshafanya manuizi katika ule mti ndio utamuita aje akusaidie kuchimba.

Kingine unaona hivi vijiti kazi ni kwamba baada ya kuwa umeshampatia mwanamke hii dawa ya unga na maelekezo namna ya kuitumia baada ya hapo utachukua kijiti kimoja na utakiwekea uzi huu mweusi na kupima kiuno cha mhusika ambae anatatizo hilo na kisha kabla ya kumfunga kiunoni utamsemea maneno haya,wewe flani bini fulani.

Kisha utamfunga na kumpa maelekezo na ataondoka.Pia akaniambia wakati mhusika anaondoka asimuage mtu yeyote atake kuwepo hapo,yani akitoka ndani ni kmy kmy tu anaenda zake.Pia alisema mjukuu wangu kati ya vitu ambavyo usije kujaribu hata kama nimekufa ni kutembea au kumtongoza mgonjwa,yani kufanya hivyo utakuwa umearibu mashariti ya mizimu na utaona jinsi utakavyo angaika yani utalipa gharama kubwa kumaliza taitizo ilo.

Vitu ambavyo nilishuhudia kwa macho yangu,najua watu mnapinga humu kwamba hakuna dawa hizo.Ni siku ambayo alikuja dada mmoja na rafiki yake sijui taarifa walikuwa wanapata wanapata wapi,uyo dada alikuwa na kama shombe shombe wa kiarabu kwakweli alikuwa ni mzuri sana.Walikuja nikawakaribisha kwenye mkeka na bibi alikuwa ndani akihudumia mwanamke mwingine.

Basi baada ya yule mwanamke kuwa ametoka wale wadada waliingia. Nakumbuka bibi alinita fulaniii. Chukuwa iyo dawa uitwange kisha uchekeche uniletee, Kwakuwa nilikuwa nimeshakuwa na uelewa wa vile vitu haikuwa jambo gumu kwangu.

Nikili kwamba moja ya vitu ambavyo bibi aliniambia ni kwamba hakuna mwanamke mwenye tatizo la uzazi ambae atatumia dawa yangu akacha kupata ujauzito labda mume wake awe hana mbegu za uzazi.

Kwakweli wanawake wanawake walikuwa wanakuja wengi sana nyumbani na baada ya miezi kadhaa kupita walikuwa wanakuja na waume zao na watoto.

Bibi alikuwa maalufu sana hapo kijijini hadi mauti inamchukua alisaidia wanawake wengi sana kutoka maeneo tofauti tofauti.

Hadi sasa mimi ndio naendelea kuyaishi yale alionionyesha bibi yangu maana katika watoto wake wengi wameshika dini na hawataki kusikia mambo hayo kabisa.

UJUMBE WANGU KWA WANAWAKE:
Nina shangaa sana leo hii wanawake hawataki kusikia habari za kutumia dawa za asiri ambazo ndio chimbuko letu afrca,mimi nakumbuka enzi hizo hata dawa za kuzuia kuzaa watu zilikuwepo.

Moja ya dawa za bibi ni kwamba ulikuwa ukija kwa shida kwamba hautaki kuzaa na fulani aisee akikufungia kijiti chake na kusemea maneno flani hakika hata kama wewe mwanaume ungepiga kila siku mzigo hakika uyo mwanamke hato beba mimba kabisa.Lakini akija kwa shida ya uzazi atabeba mimba.

Leo hii wanawake mmeamini sana dawa za uzazi wa mpango ambazo zinakwenda kuharibu mfumo wa uzazi na kadri siku zinavyosogea si ajabu wanaume tujidndae kuoa wanawake ambao ni wagumba.

Wanawake kutoa mimba imekuwa kawaida na wameona ni fashion kwao, kitu kinacho nishangza leo unakuta Mwanafunzi wa chuo ameshatoa mimba zaidi ya tatu,anakuja kustuka kuolewa hakuna kitu,yani uzazi usha haribika ana baki kutapatapa tu na kukesha kwenye makanisa ya Mitume fake eti aombewe apate mtoto pumbafuuuu kabisa,wakati ule unazitoa ulikuwa hauoni kitakacho tokea badaae?

Wanawake kununua ovyo madawa ya mtandaoni bila kujua yametoka wapi na yanatengenezwa kwa njia hipi,leo utashangaa kuona dawa mbali mbali zikitangazwa mtandaoni zinazotoka nje ya nchi eti zikiwa na lengo la kuwasaidia kupata uzazi.Ni mzungu yupi anakutakia wewe mtu mweusi maendeleo? Endeleeni kupigwa na kununua madawa bila kujua yametoka wapi.

Wanawake na ulimbukeni wa kuchoma sindano au vidonge vya kuongeza makalio.

Leo uwezi kushangaa mabinti wakiwa na maumbo kama vile wame zaliwa nayo kumbe ni fake,hivi unataka kuniambia hizo sindano mnazochoma au vidonge hakuna siku vitawalete matatizo? kama vile kansa ya kizazi,PID na mengineyo.Kama wewe ni mwanamke ambae unatumia sindano hizo ku shape umbo lako tambua sasa kwako uzazi ni mtihani na utasugua sana.

WITO WANGU KWA WANAWAKE.
Ebu tujaribu kurudi kutumia dawa za asili yetu afrika,hivi mnataka kuniambia kabla wakoloni kuja kuleta injili na dini za blaaa blaaa babu zetu na bibi zetu hawakuwa na dawa zao? ambazo ziliwasaidia kutatua changamoto zao?.Tatizo tumejifanya ukisasa na kusoma sana na kuupuuzia tamaduni zetu na kuiga tamaduni za wazungu ndo tunajiona ujanja.

Dawa za asili za uzazi hata leo hii bado zipo afrika lakini ni kwakuwa tumeamini sana vitu vya kuletewa na Wazungu na kukalilishwa kwamba dawa za asili ni uchawi wacha muendele kubugia sumu.

Wanawake tafuteni dawa za asili zitawasaidia sana kuliko kuendelea kutumia hizo sumu mkiamini zitawasaidia.

Niwatakie wanawake wote siku njema.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom