Tulimpa mwizi mateso haya, kila siku ile picha inanijia akilini

Boss la DP World

JF-Expert Member
Dec 12, 2021
1,997
7,552
Miaka ya 2005 wizi wa kutumia silaha za jadi ulikithiri sana Dodoma. Katika kijiji tulichokuwa tunaishi. Pale nyumbani tulikuwa na duka kubwa hivyo siku hiyo jamaa walipanga kuja kuvunja na kuiba.

Mida ya sa 5 usiku duka limefungwa, tumeingia kulala, tukasikia jamaa wanafoka nje huku wananoa mapanga, kuchungulia dirishani, tunaona njemba kama 6 hivi, zina mapanga, mmoja ana gobole.

Walikuwa na nondo fulani hivi kwaajili ya kuvunja mlango, sisi tulikuwa na silaha baridi inaitwa upinde na mishale ya kutosha, hivyo tukawajibukuwa atakayegusa kufuli ya fremu tutamtifua, yule jamaa mwenye gobole akapiga moja hewani.

Kaka yangu akaniambia gobole huwa na risasi moja tu hivyo kwakuwa sisi tuna mshale tutoke nje, tukachungulia kwa dirishani tukajiridhisha kuwa mlangoni hakuna mtu, wote wamesimama dukani, na baada ya risasi ile moja, walianza kuvunja makufuli ya fremu.

Nikamtanguliza bro, akafungua mlango fasta akapiga mshale mmoja ukaenda kugonga kwenye frem, jamaa kumbe waoga waka anza kukimbia, nasisi tukawaunganishia huku tunapiga kelele.

Raia wengine wakaunga, kumbe nao walikuwa wanangoja wakuanzisha, basi mwizi mmoja akaanguka kwenye ka mtaro alishindwa kuruka, tukamkamata yeye, pia lile gobole walilitupa na ile nondo ya kuvunjia kufuli. Na mapanga 3 waliyatelekeza.

Yule jamaa tumemshika, balozi wa mtaa akatoa wazo kuwa aingiliwe kinyume na maumbile😂 ila kaka akasema hiyo ni adhabu ndogo, tukambeba mpaka kwenye ka pori fulani, tukatafuta mifuko ile ya plastic.

Tukamvua nguo zote, tukamlaza juu ya gogo tukafunga kamba mikono na miguu yake tukaiunga na lile gogo, jamaa analia kwa huruma, anatukumbusha amri inayosemac Usiue.

Sasa ile mifuko ya plastic tukaiwasha moto, si unajua ikiungua inaangusha vitone vya uji uji wamoto, ndo tukawa tunamdondoshea mgongoni anajaribu kutikisika lakini wapi, alilia, alijikojolea, alitubu, akatutajia majina ya wenzake, akatutajia jirani yetu aliyewapa ramani.

Balozi akatuma vijana kumchukua yule jirani akaletwa akiwa amepigwa mapanga na wale vijana hivyo yeye hatukumwongezea adhabu.

Baada ya hasira kupungua tukawaacha porini tukasepa, yule jirani yu hai mpaka leo, alichofanya ni kuhama kijiji, yule mwizi alikufa baada ya mwezi na siku kadhaa maana hakwenda hospitali alijiuguza tu kwake.

Tangu sikuile hatukupata usumbufu, polisi walikuja kesho yake wakachukua maelezo na vielelezo, badae mjumbe akateta nao wakaondoka mazima.

Sema mjumbe alikuwa anakopa sana dukani😭
 
Kuna siku tulikuwa tunatoka club..mida ya saa 7 tunarudi nyumbani..kufika sehemu mafuta yakakata..tukavizia bodaboda mmoja tukampa 10k na kidumu akatuchukulie mafuta ayalete then tutampa hela yake..yule boda si akasepa mazima..bahati nzuri kuna mmoja wetu alikumbuka kukariri no za ile pikipiki..ilibidi wawili tushuke tutembee mpk kituo cha mafuta kuchukua mafuta..

Kesho yake sasa ilikuwa jumamosi..tukajipa kazi ya kuzunguka vijiwe vyote vya bodaboda kuitafuta ile pikipiki..tumezunguka mpk tumefika kijiwe cha 5 hatujaiona..tukasema hapana..huku tunakoenda haiwezekani yule bodaboda kijiwe chake kiwe huku,maana ni mbali sana na pale tulipomsimamisha jana...tukashauriana tugeuze..tukapita kijiwe cha 1 cha 2 cha tatu tukaiona ile pikipiki..kumbe wakati tunapita alikuwa amempeleka mteja sehemu

Sasa tulichofanya tukamwita dogo mmoja(maana tulihisi may be alitukariri sura) tukamwambia aikodi ile pikipiki imlete home...so sisi tukatangulia then tulipofika tu tukampigia dogo aikodi..yule boda akamleta dogo mpk tunapoish(wote 3 tulikuwa tumepanga nyumba 1 tumegawana tu vyumba)

Dogo akajidai kama hana hela hvyo akamwambia jamaa waingie wote ndani akampe chake..kuingia tu..kuna jamaa angu mmoja alikuwa nje..akaingiza pkpk ndani..geti likafungwa,jamaa akawekwa mtu kati

Aiseee..kuna watu tunacheka nao tu ila wana roho mbaya jmn..jamaa alikula mateso ya kimya kimya..hakuna fimbo wala kuunguzwa wala nn..ila alishindwa kutembea kwa zaidi ya nusu saa,miguu yote ililegea!!

Yule boda alikuja kuwa mshkaji wetu mzur sana mpk tunahama yale maeneo!!
 
kwahiyo hapo ulipo unanuka damu ya mtu, umeua. ulijiona kama wewe ni mtakatifu sana, kama Mungu angekuwa anakuadhibu wewe namna hiyo ukikosea ungekuwa hai leo?

Unadaiwa nafsi ambayo Mungu aliiumba wewe uliiua. wanadamu wote ni wadhaifu na wana makosa, na wanadamu wote wanao uwezo wa kubadilika kama wakipewa second chances. kuna watu mtaani hapa walikuwa wabaya, wachawi, wezi, na majambazi lakini Mungu amewabadilisha. na fahamu kuwa Mungu anawapenda watu wote, wachawi, wezi na majambazi wote bado Mungu anawapenda na anatamani wabadilike, hafurahii kifo cha mtu mwenye dhambi hata siku moja.

Ni sawa na wewe ukiwa na watoto hata wawe wezi bado utawapenda tu damu nzito kuliko maji, hivyo huwezi kujua ni alianzaje au maisha yepi yalimkuta hadi akawa mwizi asiwe kama wewe. mlidhulumu nafsi, rudi kwa Mungu ama la damu hiyo itakulilia wewe na kizazi chako na yaweza kuja kulipizwa hata kwa watoto wako.

Mbona watoto wanazaliwa wazuri tu ila wanafika mahali wanakuwa majambazi? wa kwako wana exception hiyo? Rudi kwa Mungu, tubu na uokoke kwa JIna lake Yesu Kristo ili usamehewe dhambi zako usiende na damu ya mtu huyo mautini kwasababu utaitolewa hesabu.
 
kwahiyo hapo ulipo unanuka damu ya mtu, umeua. ulijiona kama wewe ni mtakatifu sana, kama Mungu angekuwa anakuadhibu wewe namna hiyo ukikosea ungekuwa hai leo? unadaiwa nafsi ambayo...
Zamani nilikuwa nawaonea sana huruma wezi wanapopigwa, ila sasa hivi hata nione anang'olewa macho sitaumia kabisa.

Wezi sio watu wazuri kabisa wanarudisha nyuma sana maendeleo.
 
Zamani nilikuwa nawaonea sana huruma wezi wanapopigwa, ila sasa hivi hata nione anang'olewa macho sitaumia kabisa.
Wezi sio watu wazuri kabisa wanarudisha nyuma sana maendeleo.
sio kwamba siwajui, nilishawahi kuibiwa duka zima. lakini bado naamini second chance. mtumbaya anaweza kubadilika kuwa mzuri kuliko hata wewe kama akikutana na Yesu Kristo moyoni.
 
kwahiyo hapo ulipo unanuka damu ya mtu, umeua. ulijiona kama wewe ni mtakatifu sana, kama Mungu angekuwa anakuadhibu wewe namna hiyo ukikosea ungekuwa hai leo...
Jamaa walienda na gobole na mapanga, kama walitaka kuiba chumvi tu mapanga ya nini!? Ebu nenda kasome ule uzi wa watu waliokutana na majambazi/wezi ukashuhudie wezi walivyo wakatili.. Au we jamaa ni mwizi nini? Au hujawahi kuibiwa!?

Mwizi aliniibia laptop week moja kabla ya mitihani yangu ya chuo, kimsingi aliiba maisha yangu yote ya chuo mpuuzi yule.

Mwingine akanipora s7edge yangu wakati ina week tu (wale wezi wa bodaboda)

Wezi wanastahili kifo Maninaer zao.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom