Kinachotokea Siku ile mtu anavyochukuliwa MSUKULE

MOSHI UFUNDI

JF-Expert Member
Nov 25, 2022
501
1,145
Kinachotokea Siku ile mtu anavyochukuliwa MSUKULE'

'Contents' hizi hazina lengo baya, ispokua ni elimu ya uzinduzi kuamsha bongo za watu na kufahamu changamoto mpya wanazopitia watu katika ulimwengu wa kiroho.

Sisi sote tuna Imani zetu zilizo thabiti, iwe imani ya Kikristo, imani ya Kiislamu, imani ya kipagani n.k. Kuamini Imani yako isiwe ni kifungo cha wewe kutokufuatilia na kufahamu upande wa pili wa mazingira kuko vipi.

Tunashuhudia kila siku katika madhabahu zetu na mimbari zetu kwamba Dini nyingi zinapigana na shetani, dini nyingi zinapigana na wachawi, dini nyingi zinakemea uchawi.

Hivyo basi sio jambo la ajabu kwasisi WanaKigoma kuzungumzia swala la uchawi (hatujidai nalo, na wala hatulipendi kulinganishwa nalo ispokuwa ni ile hali ya kua karibu nalo kimipaka, kwasababu nchi 4 zinazo ongoza kwa nguvu za giza Afrika ni pamoja na Sudan kusini, Jamhuri ya Afrika ya Kati, na Kaskazini mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Sasa, sisi watu wa Kigoma tupo karibu nalo kimipika kutokea nchi ya Kongo. Hivyo machache katika nguvu za giza tunayafahamu na ndio maana tunakujuza na wewe ili upate kuyafahamu, na sio kwa lengo lingine ispokuwa ni kukupa dondoo moja mbili tatu walau ufahamu yapi yanatokea huko.

Kwakua Dini (imani) yako inakubali uwepo wa Uchawi na madhara yake ndio maana inapigana nao, hivyo ni ishara kwamba dini (imani) zetu zinaufahamu uchawi kwasababu huwezi kupigana na kitu usichokifahamu au kupigana na kitu ambacho hakipo.

Kwa hivyo basi, siku zote matatizo ndio humpitisha mtu sehemu ambazo hakutarajia kupita, ikiwa wewe unaishi vizuri hujawahi kukumbwa na kadhia ya uchawi basi ni jambo la kumshukuru MUNGU wako. Lakini tambua, kutokuguswa na mambo hayo isiwe ni kifungo cha wewe kutokuamini mambo hayo kama yapo na yanatenda.

Aghalabu, leo baadhi ya Serikali kwasasa zinatambua madhara ya uchawi ikiwemo nchi ya Ushelisheli, hivi siku ya juzi wamemtia hatiani Kiongozi wa Chama cha 'United Seychelles', Mh Patrick Herminie' anatuhumiwa kuhusika na Ushirikina akidaiwa kusaidiwa na Mtanzania.

Hivyo basi funguka, mimi ni Admin nakufungulia yale machache niliyo yafahamu kupitia utafiti katika uga huu.

......
Kinachotokea Siku ile mtu anavyochukuliwa MSUKULE, kwa nadharia ya hapa kwetu Kigoma msukule tunamwita SEYA' hii ndio mada natembea nayo siku ya leo. Nifuatilie kwa umakini, hatua kwa hatua.

......
Msukule (Seya) ni mtu ambaye watu kadhaa wanaamini alikufa kimazingara: katika jamii husika mtu huyu amekufa na amezikwa, kumbe inasemekana hajafa kabisa ila amechukuliwa kimazingara na kwenda kuwekwa mahali na mtu mwingine kwa ajili ya kufanyishwa kazi za aina fulanifulani, hasa za kuchosha.

Msukule ni mtu ambaye anahesabiwa amekufa, lakini ukweli ni kuwa mtu huyo huwa amechukuliwa na Mchawi ili amtumie katika kazi zake maalumu au amtumie katika mambo yake mengine anayoyataka.

Utashangaa hili linawezekana vipi: Nguvu hiyo inadadavuliwa kupitia makala hii na wakongwe wa mji wa Kigoma.
....
Katika kila kilinge cha uchawi kuna 'nguvu maalumu iitwayo 'Bakas' sio kila mchawi anaweza kufikia level hiyo, 'Bakas' ni level ya juu kabisa ya kufuru katika kilinge cha uchawi. Wadau wanasema ya kwamba ilipewa jina hilo kulinganishwa na 'baka pygmies' inaaaminiwa kwamba nguvu hiyo ilitokea katika kabila hilo.

Ili ufikie level hiyo kwanza lazima upitie kozi maalumu ya ufufuo wa mizimu makaburini iitwayo “Mortoo tombo Mivi' yenye maana 'aliye ndani ya kaburi ni wangu'. Ni moja ya kozi ngumu sana na yenye ukatili wa hali ya juu.

Ukisikia mchawi hachoki au mchawi hana huruma basi katika kozi hii ndio hufutwa rasmi kitu kinachoitwa huruma katika nafsi ya mchawi.

Kwanini makaburini?

Hii ni kwasababu inaaminika makaburini ndio kwenye nguvu, makaburi hutoa nguvu (energy) kwa waganga nguli na wachawi nguli, hata unaweza kupata shida ukaenda kwa 'Mganga-Mshirikina' akakuamuru baadhi ya kazi mkazifanyie makaburini, hii ni kwasababu makaburini kuna nguvu ya asili, hata wachawi wenyewe wakizidiwa hukimbilia huko.

Kwakua kozi hiyo ni ngumu na yenye ukatili wa hali ya juu, baadhi ya wachawi wakawaida huogopa kuisogolea na hivyo hulazimika huwalipa pesa nyingi wachawi waliohitimu kozi hiyo ili kuwasaidia kazi hizo za kuwatoa watu msukule,

Kozi ya “Mortoo tombo Mivi' ilianzishwa miaka 500 AD na ilifanikiwa kwa asilimia kubwa miaka ya 1500 A.D huko nchini Zaire na nchi ya Haiti na kuenea sehemu nyingi za Dunia.

Uchawi ni taaluma ya kukufuru, ni taaluma ya ushirikina na ndani ya uchawi kuna vipengele kadha wa kadha vinatesa na kuchosha, humo ndani kuna kozi mbalimbali za kukufuru ikiwemo za (ku-upgrade n.k). Taaluma ya uchawi ni pana sana, ni sawa na hesabu 8+2=10, 5+5=10, 9+1=10, 7+3=10, wachache wanaelewa.

Katika kozi hiyo, moja ya kipengele muhimu ni matumizi sahihi ya majani ya mti wa Mkakaya (Acacia), ndio mti mara nyingi wachawi hupendelea kukusanyikia katika vilinge, ni mti flani umekaa kama mwavuli. Wao huamini majani yake ni muhimu katika kumuadabisha na kummiliki Msukule.

Pia baadhi ya dawa za kichawi hutumika kuleta utata wa kifo cha Msukule mtarajiwa, hii ni kwasababu inaaminika kwamba Mtu anayechukuliwa msukule mara nyingi hufa kifo cha utata. Na anakufa peke yake, na huwa ni kifo cha ghafla, na baada ya kifo chake baadhi ya ndugu huweza kutofautiana na kutiliana mashaka kutokana na kifo cha ndugu yao. Kazi hiyo hufanywa na 'Mkakaya' kupitia kozi ya kustaajabisha.

Sasa, inakuaje hadi mtu anachukuliwa Msukule?

Kwanza tambua hakuna kiumbe yeyote mwenye uwezo wa kutoa roho ya mtu bila idhini ya Mwenyezi MUNGU.
(MUNGU pekee ndiye anayemiliki roho za viumbe vyote).

Kuchukuliwa msukule sio kutolewa roho, bali ni kuhamishwa kimazingira, kutoka ulimwengu wa nuru na kupelekwa ulimwengu wa giza lakini roho yako iko palepale hadi Muumba wako atakapoichukua.

Mkataba maalumu huandikwa baina ya muhitaji (mchawi) na mmiliki wa ngome ya 'Bakas' kwa lengo la kumchukua fulani bin fulani, ima kwa kumla nyama yake au kwa kumtumikisha katika ulimwngu wa kiroho. (Kuna misukule inachukuliwa kwa lengo la kuliwa nyama yake tu nasio kutumikishwa) na mingine hufanywa kuwa ndondocha.

Baada ya mkataba huo, matangazo husambazwa katika vilinge mbalimbali, kwamba fulani bin fulani anahitajika kwa mchawi fulani, je kuna mwenye pingamizi?

Ikiwa msukule anayehitajika ana ndugu yake ni Mchawi katika kilinge husika, basi huyo ndugu yake mchawi anaweza kuweka pingamizi kwa kupinga ndugu yake kuchukuliwa Msukule.

Pingamizi lake litafanyiwa judgment kuliridhia au kulikataa kulingana na level yake ya uchawi. Kama mpingaji anamiliki msukule basi hakuna budi nduguye ataondoka. Ikiwa hamiliki msukule basi mchawi mwenye kuhitaji msukule ataambiwa alete sababu za yeye kumtaka fulani bin fulani.

Hapa sasa kunaweza kutokea 'Conflict of Interest' hadi kufikia wachawi wenyewe kwa wenyewe kuanza kufanyiana uhasama, kufitiniana, kukomoana, kuumizana na kupimana mabavu baina yao.

Tambua kwamba aliyechukuliwa msukule ni mtu yu-hai, ni mzima sio mzimu wala mfu, ameibiwa tu akafichwa, ametekwa akafichwa msukuleni na waliomteka wanamtesa sana kwa kumlisha vyakula visivyofaa ikiwemo pumba, vibunzi, maganda ya miwa na kumfanyisha kazi ngumu.

Sababu zitatolewa za kuchukuliwa msukule, na hizi ndizo sababu zinazopelekea mtu kuchukuliwa msukule.

1-Kwakua mchawi siku zote hatoki mbali, basi ile Husda yake, Chuki, Wivu, Roho mbaya na ukatili wake.
Ndio sababu kuu ya mchawi kumchukua mtu na kumfanya msukule.

2-Aina ya maumbile hitajika'
Hii ni kama mchawi anajambo lake anataka kulifanya lakini anahisi kutumikisha mtu fulani katika jambo hilo itakua bora zaidi.

3-Kuikomoa familia ya mlengwa
Mchawi anaweza akakuchukua kwa lengo la kuikomoa familia yako, au kukukomoa wewe mwenyewe, kuiadhibu na kuipa simanzi familia yako, kwake yeye ndio furaha.

4-Kupata raha na kujiburudisha
Wakati mwingine mchawi hupata raha na kufurahi akimiliki msukule ambaye atakua anambebea mizigo yake mgongoni huku akimchapa mijeledi kama mtumwa, kumfanya anavyotaka ikiwemo kumnyea haja kubwa, kumkojolea, kumtoboa toboa mwili n.k

5-Biashara ya uchawi
Wakati mwingine kilinge cha wachawi huwezi kuhitaji Msukule mwenye sifa kadhaa wa kadhaa, hivyo likatangazwa dau kwa mwenye uwezo wa kumleta kwa ajili ya kufanyiwa biashara.

6-Kuliwa Nyama
Sababu nyingine yakuchukuliwa msukule ni kwenda kuliwa nyama na wachawi wenyewe, nyama ya binaadamu na mafuta yake.

7-Kuongeza nguvu na daraja la uchawi
Baadhi ya level za uchawi huwalazimisha wachawi kumiliki misukule, kuna level huwezi kufikia kama huna misukule kuanzia 10 na kuendelea. Inampa nguvu kubwa ya kichawi mmiliki.

8-Tamaa ya mali:
Mtu mchawi huweza kumchukua mkewe au mumewe au mtoto wake au nduguye akamfanya msukule na kumtumikisha katika biashara zake.

Huko Zaire imeripotiwa miaka ya 1990 imeshuhudiwa Misukule mingi kutumikishwa katika mambo ya uvuvi (hususani katika uvuvi wa kipe).

Anasimulia Jamaa mmoja aliyependa kuongozana na wavuvi kwenda kuvua nyakati za usiku, baada ya wavu kutupwa kwenye maji ili kukamata dagaa, makarabai yakiwa yanawaka kwenye maji, ghafla aliona watu chini ya maji wakifukuza dagaa ziingie kwenye nyavu, akapiga kelele... kiongozi (Captain) akamzuia na kumueleza wale watu ni misukule ya Boss katika kazi zake.
....................
Sasa, baada ya mchawi kutoa sababu zake za kwanini anataka kumchukua fulani bin fulani. Judgment hupita na 'Bakas' huamua.
....
Kinachofuatia ni uvunjaji wa nguvu za Muhusika anayetaka kuchukuliwa Msukule.

Hutumwa kikosi maalumu kuja kuvunja nguvu ya kiroho ya muhusika, ikiwemo kuanza kumroga kama anarogeka, kumvurugia mambo yake kama yatavurugika, na kumfanyia vitimbi kadhaa wa kadhaa, (Hapa sasa ni MUNGU pekee ndio hubakia kuwa mtetezi wako, ni MUNGU ndio huamua urogeke au usirogeke).

Zoezi la kumchukua Mtu Msukule ni zoezi gumu sana na huchukua muda mrefu sana kuja kukamilika hata miaka miwili, mitatu na kuendelea, sio zoezi la papo kwa hapo.

Kuna michakato mingi ya kufuru hupitika humo katikati, ambayo humpima mchawi kiwango chake cha ukatili na kutokukata tamaa hadi lengo lake litimie. Kamwe mchawi hachoki. Na wakati mwingine zoezi huwa linafeli kulingana na hali ya nguvu ya muhusika anayetaka kuchukuliwa msukule.

ZOEZI LENYEWE SASA,

Baada ya kifo cha ghafla, chenye utata
Siku ya mazishi au ndani ya siku tatu (isizidi siku tatu) muuaji/mchawi anaenda kaburini usiku akiwa na aidha mkia wa mnyama au pembe ya mnyama iliyokolea dawa za kichawi mchanganyo wa majani ya Mkakaya'.

Akifika kaburini atalitishia kaburi kwa vifaa hivyo akisema maneno "inuka mama yako amekuamrisha utoke nje" hapa anatumika "mama" kwakuwa ndiye mwenye unasaba wa kuaminika.

Baada ya hapo, kaburi linafunuka, na mfu hutokea lakini katika hali isiyoonekana kwa macho ya kawaida. Hapo mchawi humchukua mtu wake hadi kwenye chumba maalumu alichokitenga nyumbani kwake.

Akifika naye maskani, hamfanyi chochote hadi siku 7 zipite, kisha anampiga dawa kali sana ambazo zitamvuruga kabisa uzima wake wa akili na baadaye kumkata ulimi.

Toka hapo sasa, atakuwa amekamilika msukule na upungufu wa akili, viungo na uhai wake upo mikononi mwa boss wake.

Atalishwa na mchawi mwenyewe na hataweza kutembea kwenda kokote bila ruhusa ya boss. Na kama akiwa na njaa hutoa sauti ya kuunguruma kama paka, hawezi kuongea.

Hutembea kwa kutambaa kwa kuburuza mikono na miguu. Mara nyingi msukule hutembea kama sokwe mtu kwa kutumia Miguu na mikono.

Kwanini siku 7 baada ya kufa?

Wachawi wanapomuua mtu huwa wanapata hofu. Huogopa ile hali. Hivyo wanapomuua mtu huwa wanasubiri kwanza ili wajue kama watafuatiliwa ua laa.

Hivyo wanapomuua mtu humuweka kwanza kwa siku saba bila kumdhuru au kumfanya chochote. Siku saba zikipita kimya ndio hupata amani kwamba hakuna mtu wa kutufuatilia.

Kwanza wataanza kumkata ulimi ili asiweze kuongea chochote tena. Na wakishamkata ulimi wanamuhifadhi kwanza kama alichukuliwa kwa ajili ya kuliwa nyama watasubiria ifike siku ya arobaini.

NINI HUTOKEA ILE SIKU YENYEWE YA KUTANGAZWA MSIBA?

Msukule huwa mzima wa afya, huwa hajafa, wala hajatolewa roho.
Huchukuliwa mtu mzima kabisa kimazingaombwe.
Inapoonekana amekufa huwa ni mazingaombwe tu, kinachozikwa ni kitu kisicho mtu wakati mwenyewe anashuhudia lakini haonwi na yeyote.

Nguvu ya madawa ya mazingaombwe hufanya asijitambue, asionekane, asiguswe wala kugusa, asizungumze wala kusikika na pia hupotezwa kumbukumbu kwa kutotambua ndugu wala kwake.

Dawa haidumu, inabidi kila baada ya muda fulani apewe zingine kumzubaisha zaidi hadi mazishi yatapokamilika. Hakika siku hiyo ya mazishi ndio siku ambayo wachawi huwanga mchana kweupe kwakuhakikisha kwamba mtu wao hagunduliki na wala hafurukuti humo ndani hadi mazishi yapite. huwa ni uchawi mkali sana siku hiyo nguvu zote huamia hapo.

Baada ya wao kuzika, ndipo msukule anahama nyumbani kwake na kwenda kukaa eneo lile la kaburi palipozikwa, na kisha sasa ndio mchawi huja kumchukua hapo na kwenda naye nyumbani kwake.

Wachawi wanatesa, wachawi wanaumiza, wachawi wanarudisha watu nyuma na ndio maana katika vitabu vya imani hukumu ya mchawi ni kuuwawa.
................

Vyombo vingi vya habari ikiwemo Millard Ayo hapa mkoani Kigoma vimewahi kuripoti watu kadhaa waliosadikika kufa na kuzikwa lakini wakarudi,

Ni ngumu sana msukule kurudishwa kwa nguvu za waganga, mara nyingi msukule anayerudi ni yule ambaye Boss wake amefariki.

Hivyo anakosa huduma za chakula na maelekezo mengine, kisha huanza kutanga tanga hovyo na kwakuwa maisha yake yote alikuwa akipewa dawa kali na kwasasa hapati tena dawa hizo, hivyo taratibu nguvu zile huanza kumtoka na kurejea katika ulimwengu wa nuru.

Kwasababu katika uchawi Msukule harithiki, yani endapo Boss atakufa, misukule yake haiwezi kuchukuliwa na mchawi mwingine bali itaenda hovyo labda kama alimuuza kwa Boss mwingine kabla hajafa, au kama mkoba wake wa uchawi alimrithisha mtu basi atamrithisha na misukule hiyo.

Tofauti na hapo msukule atakwenda hovyo na huwenda akarejea kutoka ulimwengu wa giza na kuja ulimwengu wa nuru kutokana na kupungua kwa makali ya dawa.

KUTOKA KIGOMA.
 
Kinachotokea Siku ile mtu anavyochukuliwa MSUKULE'

'Contents' hizi hazina lengo baya, ispokua ni elimu ya uzinduzi kuamsha bongo za watu na kufahamu changamoto mpya wanazopitia watu katika ulimwengu wa kiroho.
li ya dawa.

KUTOKA KIGOMA.
Kwasababu katika uchawi Msukule harithiki, yani endapo Boss atakufa, misukule yake haiwezi kuchukuliwa na mchawi mwingine bali itaenda hovyo labda kama alimuuza kwa Boss mwingine kabla hajafa, au kama mkoba wake wa uchawi alimrithisha mtu basi atamrithisha na misukule hiyo.

Tofauti na hapo msukule atakwenda hovyo na huwenda akarejea kutoka ulimwengu wa giza na kuja ulimwengu wa nuru kutokana na kupungua kwa makali ya dawa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwasababu katika uchawi Msukule harithiki, yani endapo Boss atakufa, misukule yake haiwezi kuchukuliwa na mchawi mwingine bali itaenda hovyo labda kama alimuuza kwa Boss mwingine kabla hajafa, au kama mkoba wake wa uchawi alimrithisha mtu basi atamrithisha na misukule hiyo.

Tofauti na hapo msukule atakwenda hovyo na huwenda akarejea kutoka ulimwengu wa giza na kuja ulimwengu wa nuru kutokana na kupungua kwa makali ya dawa

Sent using Jamii Forums mobile app
Nyongeza nzuri na msisitizo.
 
Kwasababu katika uchawi Msukule harithiki, yani endapo Boss atakufa, misukule yake haiwezi kuchukuliwa na mchawi mwingine bali itaenda hovyo labda kama alimuuza kwa Boss mwingine kabla hajafa, au kama mkoba wake wa uchawi alimrithisha mtu basi atamrithisha na misukule hiyo.

Tofauti na hapo msukule atakwenda hovyo na huwenda akarejea kutoka ulimwengu wa giza na kuja ulimwengu wa nuru kutokana na kupungua kwa makali ya dawa

Sent using Jamii Forums mobile app
Naona umegongelea nyundo, Nini Siri ya wachawi kuishi mda mrefu
 
Kwasababu katika uchawi Msukule harithiki, yani endapo Boss atakufa, misukule yake haiwezi kuchukuliwa na mchawi mwingine bali itaenda hovyo labda kama alimuuza kwa Boss mwingine kabla hajafa, au kama mkoba wake wa uchawi alimrithisha mtu basi atamrithisha na misukule hiyo.

Tofauti na hapo msukule atakwenda hovyo na huwenda akarejea kutoka ulimwengu wa giza na kuja ulimwengu wa nuru kutokana na kupungua kwa makali ya dawa

Sent using Jamii Forums mobile app
Hujasema chochote mkuu
 
Kinachotokea Siku ile mtu anavyochukuliwa MSUKULE'


uwenda akarejea kutoka ulimwengu wa giza na kuja ulimwengu wa nuru kutokana na kupungua kwa makali ya dawa.

KUTOKA KIGOMA.
Maswali mawili:
1. Msukule akiwa kwa mchawi anaweza kufanya mapenzi? yaani anaweza kuchkuliwa ili uwe unamgegeda Boss mchawi? Misukule inazaliana?
2. Inakuwaje kama wamechukua Msukule ambao ni mgonjwa hasa magonjwa sugu?
 
Back
Top Bottom