Jamani mwenye Dta zaidi atuoe ili tuweze kufunguka Macho maana Kila mahali nasiki hili nikigeuka huku nasikia hili.
Naombeni mwenye Full Data azimuvuzishe huku kwenye JF
Watafika Mbwamaji?
SANDA MATUTU maandamano lini???????
MkuluHayo ndiyo mauzo kamili ya nchi, hilo linaitwa Azimio la Kigamboni
Kuna suala la msingi ambalo tunapaswa kujiuliza.The so called "unplanned miji" imetokana na nini?Mkuu Mkandara hatutofautiani kitu kuhusu haja ya kuwa na míji iliyotengezwa kwa mpango badala ya kuwa na miji ambayo inakua kama ni ajali ajali vile(unplanned). Ila hatuna watu wakutufanyia kazi hiyo kwa sasa. Kwa sababu hatuna serikali yenye bongo inayoona mbele. Na maadamu hatuna kitu kama hicho (serikali) ambacho ni muhimu katika kubuni mipango na kuisimamia kikiwa na baraka na imani ya wananchi basi tuiache ardhi ikae kama pori. Kwani itaoza?? Mbona Mwalimu JKN aliacha madini yetu kwa sababu kama hizo. Kama isingekuwa hii mibaka uchumi si wangekuja kufaidi wajukuu zetu?? Hata miji itajengwa tu, ama na kizazi chetu au kijacho. Jambo ambalo sitaki ni kuibiana kimacho macho kama ambavyo wizara ya ardhi (na serikali kwa ujumla) inafanya sasa.
Kuna suala la msingi ambalo tunapaswa kujiuliza.The so called "unplanned miji" imetokana na nini?
Nafikiri ni system yetu ambayo unademand mtu awe na offer,title na permit ya ujenzi halafu zote hizo upatikanaji wake ni mgumu sana, na hata vikipatikana hakuna support systems kama upatikanaji wa MIKOPO kwa ajili ya kufinance hayo majengo yanayotakiwa kwenye michoro ya Jiji.I THINK THE GOVT. SHOULD CREATE THE MARKET FOR THE SAME.
"unademand certain requirements, wakati hakuna support system ya kuwezesha hayo unayodemand yaweze kufanikishwa...NI NGUMU SANA.KESHO UNASEMA MIJI YETU HAINA HADHI....!!!!!!!
NI KUJENGA MAZINGIRA.THEN THE REST WAACHIWE WASWAHILI. HAWATOSHINDWA.
Jamani kama kuna mtu mwenye access au ujuzi wa kutumia ile website ya MWANAHALISI la jana tarehe 15 mwezi huu wa nne,kuna makara mmoja kwenye page ya 12 inafaa kuwekwa hapa ili wadau wengine wasome kuhusu swala hili.
Napenda kuwakirisha
Tena Waziri mwenye mamalaka ya ardhi kwa kuwaongopea wananchi usiseme. Tarehe 25 May 2008 aliwaahidi wakazi wa Kibamba kuwa wizara yake itafanya utafiti wa bei za soko la ardhi na ujnenzi ktk kata ya Kibamba na kisha atakutana nao ili kujadili viwango vitakavyotumika kuwalipa fidia. Hiovyo wawaruhusu wathamini mali wafanye uthamini wakati utafiti wa soko ukiendelea. Wananchi wakaingia mkenge kuruhusu uthamini ufanyike kisha akaingia mitini na wizara ikaimpose viwango inavyotaka ambavyo vilikuwa ni only 13% of the prevailing market prices.
Ajenda yake ni kufanikisha utwaaji wa ardhi kutoka mikononi mwa wananchi by all dubious means. Kajifunzeni Kibamba. Mkakati sahihi wa kuhakikisha ardhi uliyoanayo inakukwamua kiuchumi ni kwa fedha mbele makaratasi nyuma. Watu kutoka ardhi wakija kwako kwanza waulize bei gani kabla ya kuweka sahihi yako popote pale. kwa mtindo huo hawana ubavu. Mkiingia mkenge mkafanya tamaa kama watu wa Kibamba mkasaini kwanza documents zozote kabla ya bei kutangazwa wazi wazi mmekwisha
Moja ya tatizo kubwa ni wengi wetu (me included) kutozifahamu sheria. Wiki iliyopita kwenye KipimaJoto ilielezwa kwamba thamani ya ardhi unayopaswa kulipwa fidia sio ya soko la sasa. Ardhi itathaminishwa kwa kuzingatia thamani yake kabla ya serikali kutangaza azma ya kuendeleza makazi au miji mipya.
Sheria inaelekeza tofauti na watu wanavyofikiri.
Ergo.... sheria ya ardhi ina hitlafu kubwa na inahitaji marekebisho! Akina Tundu Lissu wameipigia kelele sana, wakaonekana ni wakorofi, mi nawashauri wakazi wa huko Kigamboni na Kibamba wamtafute Tundu Lissu au LEAT wawatetee mahakamani.