Huihui2
JF-Expert Member
- Jan 5, 2012
- 5,528
- 8,373
Alianza Patrick Mwalunenge, Mwenyekiti wa CCM Mbeya kusema kuwa mwaka 2025 kutakuwa na Fomu Moja tu ya kugombea ubunge jimbo la Mbeya Mjini.
Leo kuna clip ya dak 3 inatembea ikimuonyesha mtu mmoja akihutubia mkutano wa CCM Mbeya huku Spika wa Bunge Tulia Ackson ambaye ndiye Mbunge wa sasa wa Mbeya Mjini. Mtu huyo ameongea yaleyale yaliyotamkwa na Mwenyekiti wa CCM Mbeya.
Ni wazi hizi ni siasa chafu ambazo ziko kinyume na Katiba ya JMT na hazina tija kwa wananchi wa Mbeya.
Kama ni kweli Tulia Ackson ameifanyia Mbeya mambo makubwa kwa nini anaogopa ushindani?