Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,447
- 7,830
'The IPU Governing Council elects the IPU President for a term of three years. He or she must be a sitting Member of Parliament throughout the term of the presidency'
Leo Tulia Ackson amechaguliwa kuongoza umoja wa mabunge duniani kwa kipindi cha miaka mitatu. Moja ya sifa ya kuendelea kuwa rais wa umoja huo ni kubaki kuwa mbunge kwa kipindi chote cha muhula wake wa miaka mitatu.
Tanzania inatarajiwa kuingia kwenye uchaguzi mkuu miaka miwili ijayo, Tulia atakuwa amebakisha mwaka mmoja kwenye muhula wake wa Urais IPU. Ukiachana na uchaguzi wa 2020, Sugu amekuwa na rekodi nzuri ya matokeo Mbeya mjini huku mwaka 2015 akizoa kura nyingi mpaka kuwa mbunge wa kwanza aliyechaguliwa kwa namba kubwa ya kura Tanzania nzima.
Mwaka huu wa 2023 wawili hao wamekuwa wakirushiana vijembe kila mmoja akitamba kumgaraza mwenzake uchaguzi wa 2025 huku Dkt. Tulia akianza na Sugu kujibu mapigo.
Uchaguzi wa ubunge jimbo la Mbeya Mjini umetiwa ndimu na chumvi! Tusubiri 2025..
Pia, soma=> Dkt. Tulia Ackson ameshinda Urais wa IPU kwa kishindo, apata kura 172 kati ya 303