Tukisema mfungo wa Ramadhan ni mwepesi na ni kubadili ratiba ya kula tunakosea?

Uncle bright

JF-Expert Member
Feb 9, 2023
1,040
4,080
tujadiliane sio conclusive statement, Well kwangu navyoona and i am open to be criticised / kuelimishwa ni kwamba :

Huwa nashangaa sana nikiona baadhi (sio wote) waliofunga ramadan wakilalamika swaumu imetaiti (njaa), nina uhakika hawa wanaolalamika (baadhi) hawawezi kutoboa mfungo wa kikristo.

Funga ya mkristo akila saa moja jioni ni mpaka kesho tena saa moja jioni hakuna kunywa maji wala kula, na hata mle hadharani wala hapagawi au kulalamika mnamuingiza tamaa, yani mtu hajala tangu jana lakini haonyeshi dalili yoyote ya kulegea, ndio maana inakuwa ngumu sana kujua kafunga.

Upande wa pili kufungua saa moja jioni, kabla ya kulala mida ya saa nne flani hivi unatupia tena, haijaishia hapo alarm inategwa saa kumi alfajiri kuwahi kuamka kula daku, ni kama vile ratiba ya lunch inahamia alfajiri na ratiba ya chai kabla ya kulala, cha kushangaza baadhi yao hata wakiona mtu anakula hadharani tayari kuna roho ya kutamani inaingia utasikia wakilalamika "huoni aibu kula hadharani", "unahtuharibia swaumu", n.k. Zanzibar wameenda mbali zaidi ukikutwa unashushiwa kipigo.
 
Huwa nashangaa sana nikiona baadhi (sio wote) waliofunga ramadan wakilalamika swaumu imetaiti (njaa), nina uhakika hawa wanaolalamika hawawezi kutoboa mfungo wa kikristo...
Embu tuonyeshe mkristo mmoja tu anayefunga hivyo? Mnavyopenda kula tangu lini mkafunga wenyewe mnajijua kama dini imeshawapita pembeni dunia mmeiweka mbele kiufupi 99% ya wakristo hawafungi funga yao ni kula ila usishibe, ndio maana hata hiyo kwaresma haieshimiwi duniani kote kwasababu hawafungi
 
Huyu mtangazaji maarufu southafrica amekuwa muwazi na kuvutiwa na waislamu wanavyotekeleza ibada zao na ni wengi wanavutiwa hata wewe mleta hoja umevutiwa ndio maana umeamua kuja na chuki zako zisizokuwa na msingi.

Screenshot_20240320-072925_Facebook.jpg
 
huyu mtangazaji maarufu southafrica amekuwa muwazi na kuvutiwa na waislamu wanavyotekeleza ibada zao na ni wengi wanavutiwa hata wewe mleta hoja umevutiwa ndio maana umeamua kuja na chuki zako zisizokuwa na msingi
Anaruhusiwa kuhama dini, kuna uhuru wa kiimani kuhamia dini yoyote na anaweza kurejea kwa uhuru,

shida inakuja ikiwa vice versa, nchi kama Saudia wanakuua
 
Lakini kuwe na mipaka, mfano kuna nchi wanakataza kula hadharani utadhani ni mwezi mtukufu kwa wote

Jambo la watu flani lisilazimishwe liwe la watu wote
Hii ni sawa, Zanzibar tu jtano nilikuwa huko,kila kitu kimefungwa na kuna maeneo hata maji huuziwi,jambo ambalo si sahihi maana kuna wagonjwa, wajawazito, watoto wadogo etc. Tukiheshimiana kila kitu kitakuwa rahisi tu
 
Back
Top Bottom