Nimepona Ugonjwa wa Presha ya Juu kwa kubadili tu mfumo wa maisha

Mfalme_wa_Nyika

JF-Expert Member
May 24, 2023
391
859
Miezi kadhaa iliyopita nilikubwa na misukosuko mingi sana kimaisha na magonjwa mbalimbali makubwa kuninyemelea ikiwamo high blood presha.

Nikiwa kijana kabisa mwenye ndoto za maisha yangu nilishtuka sana nilipofika hospitalini siku moja kwa issue ingine na dokta kunipima presha kwanza kisha kuniuliza kama ninatumia dawa za presha au la!? ( kwa maana yake aliona mimi ni mgonjwa wa presha) nikwambia sijui anaongea nini kwani kuna nini!? mimi situmii dawa zozote nimekuja kwa issue fulani tu. Daktari akaniangalia akasema una high blood pressure hapo ilikuwa 140/90 na mapigo ya moyo yalikuwa 135 ( juu mno kuliko kawaida)

Kifupi nilishtuka sana, kimawazo nikapata stress kubwa mno na utulivu ukanitoka, nikajuta ni bora nisingeenda hospitali kujua hayo, nikamwambia dakari nipime tena akapima baada ya dakika kama 15 hivi, ndio presha inazidi kupanda mpaka 168/110, lakini nilikua kawaida, daktari akaogopa akasema nitulie akapima tena baada ya dakika 10 presha ikapanda mpaka 210/140 na heart rate 150, daktari akaagiza nipelekwe emergency room.

Kwa kweli nilikua kawaida tu natembea na daktari alikua anashangaa kwa presha hiyo inakuwaje niko kawaida na wazo la yeye kuniambia nipelekwe emergency room nipewe dawa zakushusha nilikataa kimoyomoyo nakusema mimi sio mgonjwa wa presha na hapo kukumbuka sala zote nakusali. Nilijua kuwa nimepata panic attack maana napenda sana kuwa na afya na habari za magonjwa huwa zinanipa wakati mgumu kukubali.

Nilienda emegeency room huko nikakutana na mdada daktari mwingine ambaye aliniambia kwa nilivyo haamini anipe dawa hebu tukae tupige stori mbili tatu kwanza kisha tupime presha tena tuone ikoje, basi alikua daktari mwema sana akanipa moyo nakuongea ongea na kila baada ya dakika kumi akawa anapima presha inashuka points zaidi ya 20, 25 mpaka 30, mwisho kabisa ikawa 140/90 hivi, dokta akasema si unaona imeshuka yenyewe ingawa mapigo ya moyo yalikuwa bado juu ya 100 na hivyo mchawi ni wewe mwenyewe angalia mfumo wa maisha yako hata hii iliyopo unaweza ukaibadili kabisa bila dawa na mimi sikuandikii dawa. Shukrani dokta popote ulipo pale Moshi. Nilichukua maneno yako nakufanyia kazi.

Basi nikaondoka hospitalini siku ile ofkoz mawazo yalikuwapo maana bado namba za presha 140 na hivi kwa 90 na hivi zilikua zinanipa mawazo nakuamua kubadili mfumo wa maisha.

Nilikua nina kilo zaidi ya 80 hivi ila hazijafika 90 na mimi mrefu wa cm 178. Nikajiambia moyoni kwanza uzito wangu hauendani na urefu, ni lazima kilo kadhaa zipigwe chini. Pia nikaangalia maisha yangu sipati muda mwingi kulala au kupumzika, nikasema kila siku lazima nilale masaa yasiyopungua nane ila yasizodi saa kumi na mbili. Pia nikaona nina kuwaga naruhusu sana msongo wa mawazo kwa mambo madogo makubwa yote tu nikasema ni bora nianze kuenjoy life na kukubali matokeo yeyote bila kujitesa kuwaza, na pia nikakumbuka ulaji wangu wa vyakula vya kisasa niachane nao, misoda, mi bia (ingawa sikuwa nakunywa sana mara moja moja) na mi chai ya sukari nk mi burger, pizza kuku wakukaanga nk. Pia nikakumbuka kuwa nimeacha kuwa active, nianze mazoezi.

Nikaanza kufanya mazoezi kukimbia kila asubuhi sio chini ya mwendo wa kilomita 5, nikaanza kuwa na muda maalumu wakulala na kuamka bila kujali chochote mda huo ni lazima nilale, nikapunguza watu toxic maishani wanaonipa mawazo na stress na kutatua changamoto ninazoweza tatua na nisizoweza tupa kule bila kujali sana, kifupi nilikua nacheza na saikolojia yangu, suala la milo mitatu kwa siku nikatupa kule, nikasema ntakwenda na mlo mmoja pekee.

Nikawa nakula breakfast kikombe kimoja cha maji vuguvugu yaliyochanganywa malimao matatu mpaka matano na punje za tano za kitunguu saumu na tangawizi kidogo pamoja na kutafuna ndizi mbivu mbili.

Na kuhusu kula , chakula ni mara moja kwa siku na ni mchana kati ya saa sita mpaka saa nane, na chakula ni mchemsho pekee au raw veggies , hapo siweki chumvi wala nini ili kupata ladha natafuta kwenye viungo kama karafuu, mdalasini, limaio iliki nk na sahani yangu inakusanya 50% mbogamboga za majani kama spinach, mnafu, matembele na matunda kama ndizi mbivu kila mlo, zabibu mara kadhaa, matango mara nyingi na 35% ya sahani ni protein kama samaki, dagaa, nyama ya bata maji, mara nyingi na maziwa mgando yaliyotikiswa kutolewa siagi mara kadhaa (ikumbukwe nyama nyekundu kama ng'ombe mbuzi pamoja na kitomoto niliacha kabisa kula) na 15% ya sahani ni kula vyakula vya wanga ila hapa ugali na wali nimeacha kabisa, hapa ninakula viazi vitamu pekee kiasi kidogo tu kilichochemshwa na 5% ni viungo kama vitunguu maji saumu mdalasini karoti hoho bamia biringanya nk.

Muda mwingine woote nakunywa tu maji si chini ya lita moja na nusu mpaka mbili kila siku mpaka mda wakula tena siku ingine. hakuna cha soda au energy wala bia na kadri siku zilivyozidi kwenda mbele ndivyo nilizidi kuvichukia masoda na mastarehe mengine ambayo tumekuwa tukiendekeza tukidhani ndio utajiri au fasheni.

Na kila jioni nikitoka kazini, badala ya kwenda sijui mahali nilitumia mda huo kufanya tafukuru ya maisha yangu na kuwa na muda na mimi binafsi kwa kutembea tu umbali mrefu kwa miguu huku nikiangalia watu mandhari mbalimbali nk na pia kusali.

Hivyo ndio imekuwa mfumo ma maisha yangu takribani miezi miwili sasa, and guess what!? Mungu hamtupi mja wake and life style changes dont lie.

Kwanza nimeshangaa namna kilo zilivyopungua, kutoka uzito wa mwili wa sijui kilo 86 mpaka sasa jina kilo 69, niko kila siku watu wananiambia nazidi kuwa mtoto kijana yaani nag'aa nina miaka 33 ila muonekano wangu watu wanadhani nina miaka 25, nikawa nimenunua kabisa mashine yakupima BP kutoka duka la vifaa vya mahospitalini kufuatilia muenendo wa presha ya damu ya mwili wangu nyumbani na popote nilipo, cha ajabu kila baada ya muda nilikua naona jinsi namba zinapungua, mpaka kuandika uzi huu napenda kuwaambia kuwa kwa takribani wiki mbili sasa presha yangu imekuwa normalized kabisaaaa yaani NIMEPONA PRESHA BILA KULA CHEMBE YA DAWA ZA HOSPITALINI, kwa kubadili tu mfumo wa maisha kwa sasa haizidi 120/80 na mara kadhaa naikuta iko perfect kabisa chini hata ya 120/80 ...kuna saa ipo mpaka 110/70 au 115 kwa 75 au 105/68 nk kama vile niwaonesha picha hapo hii ni ya muda huu leo nikiwa naandika uzi huu.

Nakuhusu mapigo ya moyo yaani baada ya mazoezi kukimbia kama wiki moja mbili tu yalijua kuwa normal kabisaa yaani hayazidi normal rate ya 100. Jamani sijui nilikua wapi mimi kuendekeza maisha ya gari kila mahali kila sehemu kudhani kutembea kwa miguu ni ufala, ndio maana Mungu alikuumba na miguu utembee sio kuiweka kwenye gari uponyeze tu accelerator, tembeeni hasa vijana wa Daslamu.

Nataka kuwaasa wote kuwa watu wengi wana presha ya juu bila wao kujua, ndio unasikia mtu kaanguka ghafla unaambiwa shambulio la moyo kaenda, nashauri ni vema kujua afya zenu, na hata ukijua una presha ya juu usiogope kabisa kuwa na presha...hofu ni presha yenyewe, presha ya juu unaweza kabisa kuirudisha kawaida ukiamua tu kukana mfumo mbovu wa maisha ya usasa. Mimi ni shahidi wa hilo na wala usikimbilie kwa wapiga dili kwa magonjwa ya watu kutafuta msaada, utapoteza pesa zako, jisaidie mwenyewe hakuna linaloshindikana kwako na kwa Mungu.

Amini. Shukrani kwa Mungu alonipa hekima kuchukua hatua na kubariki hatua zangu sasa mimi ni mtu wa kawaida kiafya.

NB: Yaani maisha ya mazoezi, kula vizuri hapa sio pizza na chipsi kuku, kutokuwa na msongo na hofu ya maisha, kusali kupumzika kucheka nakufurahi, siachii NG'O
 
Uko sahihi. Ila kukimbia kila siku 5 kms na kunywa lita mbili za maji ni chache. Fikisha 3.

usiku hauli kabisa?
yaah kulingana uzito wangu maji lita mbili ni sawa hata kama napoteza sana maji asubuhi kwenye kukimbia, lakini pia napata maji mengine kwenye matunda kama tikitiki maji na matango ninayokula kwa siku, yah lita tatu ni poa pia hasa tunapoingia majira haya yakiangazi, usiku mimi sili kabisa aisee....yaani chakula ni kati ya saa sita na sa nane...mda ntaokula leo ndio kesho hivyo hivyo....siku ingine badala ya chakula narukisha nakunywa tu le'ts say juice ya kijani.....usiku nakula tu ndizi mbili mbivu...kifupi ndizi mbivu nakula si chini ya nne kwa siku....asubuhi mbili na jioni mbili
 
Hongera ila kwa umri wako wa 33yrs bado mapema kusherekea matokeo ya afya yako.
 
Hayo masharti uliyojiwekea hayafai kuigwa sababu yanaweza kuwa na madhara kwa wengine,japo yalikusaidia,hongera sana kwa kupona presha.
 
Hongera ila kwa umri wako wa 33yrs bado mapema kusherekea matokeo ya afya yako.
Ni mwanzo mzuri kaka sijasherehekea ndio kwanza naanza safari kukaniliana na changamoto za maisha na afya....imagine ningekua mzembe na sijui hili tatizo nikakaa nalo na umri huu ingekuwaje huko badae!? muhimu tubadili mfumo wa maisha....mfumo wa maisha ndio chanzo cha matatizo yote kiafya yanayowakumba watu....tunachoweza rekebisha turekebishe nakufanya tusiyoyaweza tumuachie Mungu
 
yaah kulingana uzito wangu maji lita mbili ni sawa hata kama napoteza sana maji asubuhi kwenye kukimbia, lakini pia napata maji mengine kwenye matunda kama tikitiki maji na matango ninayokula kwa siku, yah lita tatu ni poa pia hasa tunapoingia majira haya yakiangazi, usiku mimi sili kabisa aisee....yaani chakula ni kati ya saa sita na sa nane...mda ntaokula leo ndio kesho hivyo hivyo....siku ingine badala ya chakula narukisha nakunywa tu le'ts say juice ya kijani.....usiku nakula tu ndizi mbili mbivu...kifupi ndizi mbivu nakula si chini ya nne kwa siku....asubuhi mbili na jioni mbili
Yan ndizi mpk nne unakula kw siku no hataree sana aisee.
Ndizi nazo sio nzur sana ukizidisha inasemekana huwa ni chanzo cha Kisukar
 
Miezi kadhaa iliyopita nilikubwa na misukosuko mingi sana kimaisha na magonjwa mbalimbali makubwa kuninyemelea ikiwamo high blood presha.

Nikiwa kijana kabisa mwenye ndoto za maisha yangu nilishtuka sana nilipofika hospitalini siku moja kwa issue ingine na dokta kunipima presha kwanza kisha kuniuliza kama ninatumia dawa za presha au la!? ( kwa maana yake aliona mimi ni mgonjwa wa presha) nikwambia sijui anaongea nini kwani kuna nini!? mimi situmii dawa zozote nimekuja kwa issue fulani tu. Daktari akaniangalia akasema una high blood pressure hapo ilikuwa 140/90 na mapigo ya moyo yalikuwa 135 ( juu mno kuliko kawaida)

Kifupi nilishtuka sana, kimawazo nikapata stress kubwa mno na utulivu ukanitoka, nikajuta ni bora nisingeenda hospitali kujua hayo, nikamwambia dakari nipime tena akapima baada ya dakika kama 15 hivi, ndio presha inazidi kupanda mpaka 168/110, lakini nilikua kawaida, daktari akaogopa akasema nitulie akapima tena baada ya dakika 10 presha ikapanda mpaka 210/140 na heart rate 150, daktari akaagiza nipelekwe emergency room.

Kwa kweli nilikua kawaida tu natembea na daktari alikua anashangaa kwa presha hiyo inakuwaje niko kawaida na wazo la yeye kuniambia nipelekwe emergency room nipewe dawa zakushusha nilikataa kimoyomoyo nakusema mimi sio mgonjwa wa presha na hapo kukumbuka sala zote nakusali. Nilijua kuwa nimepata panic attack maana napenda sana kuwa na afya na habari za magonjwa huwa zinanipa wakati mgumu kukubali.

Nilienda emegeency room huko nikakutana na mdada daktari mwingine ambaye aliniambia kwa nilivyo haamini anipe dawa hebu tukae tupige stori mbili tatu kwanza kisha tupime presha tena tuone ikoje, basi alikua daktari mwema sana akanipa moyo nakuongea ongea na kila baada ya dakika kumi akawa anapima presha inashuka points zaidi ya 20, 25 mpaka 30, mwisho kabisa ikawa 140/90 hivi, dokta akasema si unaona imeshuka yenyewe ingawa mapigo ya moyo yalikuwa bado juu ya 100 na hivyo mchawi ni wewe mwenyewe angalia mfumo wa maisha yako hata hii iliyopo unaweza ukaibadili kabisa bila dawa na mimi sikuandikii dawa. Shukrani dokta popote ulipo pale Moshi. Nilichukua maneno yako nakufanyia kazi.

Basi nikaondoka hospitalini siku ile ofkoz mawazo yalikuwapo maana bado namba za presha 140 na hivi kwa 90 na hivi zilikua zinanipa mawazo nakuamua kubadili mfumo wa maisha.

Nilikua nina kilo zaidi ya 80 hivi ila hazijafika 90 na mimi mrefu wa cm 178. Nikajiambia moyoni kwanza uzito wangu hauendani na urefu, ni lazima kilo kadhaa zipigwe chini. Pia nikaangalia maisha yangu sipati muda mwingi kulala au kupumzika, nikasema kila siku lazima nilale masaa yasiyopungua nane ila yasizodi saa kumi na mbili. Pia nikaona nina kuwaga naruhusu sana msongo wa mawazo kwa mambo madogo makubwa yote tu nikasema ni bora nianze kuenjoy life na kukubali matokeo yeyote bila kujitesa kuwaza, na pia nikakumbuka ulaji wangu wa vyakula vya kisasa niachane nao, misoda, mi bia (ingawa sikuwa nakunywa sana mara moja moja) na mi chai ya sukari nk mi burger, pizza kuku wakukaanga nk. Pia nikakumbuka kuwa nimeacha kuwa active, nianze mazoezi.

Nikaanza kufanya mazoezi kukimbia kila asubuhi sio chini ya mwendo wa kilomita 5, nikaanza kuwa na muda maalumu wakulala na kuamka bila kujali chochote mda huo ni lazima nilale, nikapunguza watu toxic maishani wanaonipa mawazo na stress na kutatua changamoto ninazoweza tatua na nisizoweza tupa kule bila kujali sana, kifupi nilikua nacheza na saikolojia yangu, suala la milo mitatu kwa siku nikatupa kule, nikasema ntakwenda na mlo mmoja pekee.

Nikawa nakula breakfast kikombe kimoja cha maji vuguvugu yaliyochanganywa malimao matatu mpaka matano na punje za tano za kitunguu saumu na tangawizi kidogo pamoja na kutafuna ndizi mbivu mbili.

Na kuhusu kula , chakula ni mara moja kwa siku na ni mchana kati ya saa sita mpaka saa nane, na chakula ni mchemsho pekee au raw veggies , hapo siweki chumvi wala nini ili kupata ladha natafuta kwenye viungo kama karafuu, mdalasini, limaio iliki nk na sahani yangu inakusanya 50% mbogamboga za majani kama spinach, mnafu, matembele na matunda kama ndizi mbivu kila mlo, zabibu mara kadhaa, matango mara nyingi na 35% ya sahani ni protein kama samaki, dagaa, nyama ya bata maji, mara nyingi na maziwa mgando yaliyotikiswa kutolewa siagi mara kadhaa (ikumbukwe nyama nyekundu kama ng'ombe mbuzi pamoja na kitomoto niliacha kabisa kula) na 15% ya sahani ni kula vyakula vya wanga ila hapa ugali na wali nimeacha kabisa, hapa ninakula viazi vitamu pekee kiasi kidogo tu kilichochemshwa na 5% ni viungo kama vitunguu maji saumu mdalasini karoti hoho bamia biringanya nk.

Muda mwingine woote nakunywa tu maji si chini ya lita moja na nusu mpaka mbili kila siku mpaka mda wakula tena siku ingine. hakuna cha soda au energy wala bia na kadri siku zilivyozidi kwenda mbele ndivyo nilizidi kuvichukia masoda na mastarehe mengine ambayo tumekuwa tukiendekeza tukidhani ndio utajiri au fasheni.

Na kila jioni nikitoka kazini, badala ya kwenda sijui mahali nilitumia mda huo kufanya tafukuru ya maisha yangu na kuwa na muda na mimi binafsi kwa kutembea tu umbali mrefu kwa miguu huku nikiangalia watu mandhari mbalimbali nk na pia kusali.

Hivyo ndio imekuwa mfumo ma maisha yangu takribani miezi miwili sasa, and guess what!? Mungu hamtupi mja wake and life style changes dont lie.

Kwanza nimeshangaa namna kilo zilivyopungua, kutoka uzito wa mwili wa sijui kilo 86 mpaka sasa jina kilo 69, niko kila siku watu wananiambia nazidi kuwa mtoto kijana yaani nag'aa nina miaka 33 ila muonekano wangu watu wanadhani nina miaka 25, nikawa nimenunua kabisa mashine yakupima BP kutoka duka la vifaa vya mahospitalini kufuatilia muenendo wa presha ya damu ya mwili wangu nyumbani na popote nilipo, cha ajabu kila baada ya muda nilikua naona jinsi namba zinapungua, mpaka kuandika uzi huu napenda kuwaambia kuwa kwa takribani wiki mbili sasa presha yangu imekuwa normalized kabisaaaa yaani NIMEPONA PRESHA BILA KULA CHEMBE YA DAWA ZA HOSPITALINI, kwa kubadili tu mfumo wa maisha kwa sasa haizidi 120/80 na mara kadhaa naikuta iko perfect kabisa chini hata ya 120/80 ...kuna saa ipo mpaka 110/70 au 115 kwa 75 au 105/68 nk kama vile niwaonesha picha hapo hii ni ya muda huu leo nikiwa naandika uzi huu.

Nakuhusu mapigo ya moyo yaani baada ya mazoezi kukimbia kama wiki moja mbili tu yalijua kuwa normal kabisaa yaani hayazidi normal rate ya 100. Jamani sijui nilikua wapi mimi kuendekeza maisha ya gari kila mahali kila sehemu kudhani kutembea kwa miguu ni ufala, ndio maana Mungu alikuumba na miguu utembee sio kuiweka kwenye gari uponyeze tu accelerator, tembeeni hasa vijana wa Daslamu.

Nataka kuwaasa wote kuwa watu wengi wana presha ya juu bila wao kujua, ndio unasikia mtu kaanguka ghafla unaambiwa shambulio la moyo kaenda, nashauri ni vema kujua afya zenu, na hata ukijua una presha ya juu usiogope kabisa kuwa na presha...hofu ni presha yenyewe, presha ya juu unaweza kabisa kuirudisha kawaida ukiamua tu kukana mfumo mbovu wa maisha ya usasa. Mimi ni shahidi wa hilo na wala usikimbilie kwa wapiga dili kwa magonjwa ya watu kutafuta msaada, utapoteza pesa zako, jisaidie mwenyewe hakuna linaloshindikana kwako na kwa Mungu.

Amini. Shukrani kwa Mungu alonipa hekima kuchukua hatua na kubariki hatua zangu sasa mimi ni mtu wa kawaida kiafya.

NB: Yaani maisha ya mazoezi, kula vizuri hapa sio pizza na chipsi kuku, kutokuwa na msongo na hofu ya maisha, kusali kupumzika kucheka nakufurahi, siachii NG'O
Hivyo vitunguu swaumu ulikuwa unakula wakat gani?
Ukimaliza kunywa Maji ya moto na Mlimao ndipo unakunywa au lah?
 
Yan ndizi mpk nne unakula kw siku no hataree sana aisee.
Ndizi nazo sio nzur sana ukizidisha inasemekana huwa ni chanzo cha Kisukar
asikudanganye mtu ndizi zimejaa potassium kwa kiwango cha juu mno...na pottasium kazi yake nikuregulate flow of blood katika mwili inalegeza blood vessel damu inapita vizuri, nakula ndizi balaa na sukari yangu hajawahi kuzidi 5
 
Ni kweli kabisa ukipima presha ikaonekana iko juu cha kwanza kabisa usipanik, epuka kabisa hofu hiyo ni njia moja ya kuitibu ndipo mengine yanafuata.

Pia unene hauna maana kabisa ni cha kuepuka kabisa na kupunguza mawazo.
 
Hivyo vitunguu swaumu ulikuwa unakula wakat gani?
Ukimaliza kunywa Maji ya moto na Mlimao ndipo unakunywa au lah?
vitunguu saumu, navipondaponda kwenye mortar ndogo pamoja na tangawizi, nachukua kikombe ujazo wa maji kama mil 200 ya vuguvugu kisha naweka mchanganyo huo, kisha nakamulia malimao....nachanganya nakunywa...ikumbukwe hii ndio kitu nakula cha kwanza asubuhi yote hiyo baada ya mazoezi tu...maana mimi nimefikia kiwango sinywi hata maji nikiwa nakimbia asubuhi....maji huwa baada ya mazoezi na hiyo breakfast cup
 
Saa tatu hii nko nakula chapati kama 4 na mandondo.. itabd na mimi nianze
maharage ni mazuri sana badala ya nyama, ila tatizo ni hizo pastry yaani hizo chapati na mengineo wanga una sukari nyingi na kuongeza uzito....ila kama upo normal hauna presha we piga ila kama una pressure ya juu achana nayo....kula maharage chemsha weka mafuta kitone tu ya alizeti au mzeituni katia viungo vyote huko usiweke chumvi nyingi kitone tu au usiweke kabisa....kisha chemsha kiazi chako kitamu na mchicha wakutosha kula....afya bora
 
Back
Top Bottom