Ushuhuda: Nilihisi nina upungufu wa nguvu za kiume nilikula sana karanga mbichi, mtindi, vipande vya nazi na mhogo bila mafanikio, NIMEPONA !!

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,033
MUHIMU: TIBA HII SIO KWA WOTE, NI KWA WALE WENYE TATIZO LINALOFANANA NA LANGU.

Nilidhani labda ndio umri umeanza kwenda maana si kwa kuhangaika kulitafuta goli la pili, na kuna kipindi ni kimoko chali kiasi cha kuwa bingwa wa visingizio kukwepa aibu.

Kiukweli nilikula sana dawa asili za kubusti kama vipande vya nazi, karanga mbichi, maziwa ya mgando na sometimes hata mihogo. sijawai kufikiri kutumia mkongo ama kuchanganya panado na Mo extra maana nina elimu ya hivi vitu kuwa na madhara makubwa sana, huwezi kuyaona madhara leo lakini kwa uhakika vinaleta madhara makubwa sana kiafya baada ya miaka kadhaa.

Ilishafika kipindi nikaona basi nikubaliane tu na hii hali japo moyoni nilikuwa naumia maana nikijicheki ndio kwanza hata sijafika 35, Kwakweli mwaka jana biashara zangu za pembeni zilipata mafanikio ila hili tatizo lilinipa stress, nilikuwa najihisi kuna sehemu ya uanaume wangu imetoweka.

KUmbe nilichokuwa sikijui tatizo lipo upande wangu !!

Mwaka jana woooote January Mpaka Decmber nilikuwa naingia kulala saa tisa hadi saa 12 alfajiri na kuamka saa sita hadi saa nane, Ni mwaka mzima kazi yangu ilinihitaji kupiga shift usiku. Sikuweza kutimiza hata jukumu langu la kuwa mlinzi wa nyumbani sana sana nilitumia tu kamera za cctv kucheki mazingira, Mwenzangu nae ilikuwa changamoto kumaliza usiku mzima peke yake na watoto hapo nyumbani.

Sasa kuanzia mwaka huu hali imerudi kawaida naenda asubuhi saa mbili sometimes hata saa nne asubuhi, hivyo usiku nachapa usingizi na napumzika vya kutosha.


Nimekuja kugundua hivi sasa sio kwamba nimepata kiu ya kuendelea la tatu bali mishindo yangu imekuwa ya nguvu sana na ina last muda mzuri, hata mwenzangu kanisahangaa na kuhisi labda huko shift za usiku nilikuwa nina mchepuko ananichosha kabla sijaja kwake 😅.

Nimekuja kugundua kupata usingizi wa kutosha ni dawa nzuri sana ya magonjwa mengi, mwaka jana pia nilikuwa na ukungu kwenye ubingo, kuna baadhi ya nyakati nilikuwa msahaulifu ila kwa sasa hadi najishangaa navyoweza kukumbuka mambo kwa urahisi.

CONCLUSION NA USHAURI WANGU KULINGANA NA NILIYOPITIA HADI KUPONA

1. kubadili badili ratiba ya kulala mfano kwangu mara nilale saa tisa, mara saa 10, mara saa 12 na kuamka, hii haitakiwi, inabidi uwe na muda moja wa kulala

2. Kulala mida ambayo haiendani na uliozoeleka kwa asili hata kwa wanyama wengi kunaweza changia matatizo, muda wa kulala ni baada ya jua kuzama na muda wa kuamka ni alfajiri ama asubuhi, kulala usiku wa manane, mchana, n.k. haifai.

3. Kwa ushauri wa ziada kwa wale ambao mnapenda kutumia simu mkiingia vitandani, kushinda kucheki movies, kucheza games, n.k, nawashauri hizo tabia muache, simu zinaharibu sana ratiba za kulala, waweza jikuta unalaal usiku wa manane daily na kubadili badili muda wa kulala
 
Na nilidhani labda ndio umri umeanza kwenda maana si kwa kuhangaika kulitafuta goli la pili, na kuna kipindi ni kimoko chali kiasi cha kuwa bingwa wa visingizio kukwepa aibu.

Kiukweli nilikula sana dawa asili za kubusti kama vipande vya nazi, karanga mbichi, maziwa ya mgando, n.k. sijawai kufikiri kutumia mkongo ama kuchanganya panado na Mo extra maana nina elimu ya vitu huwezi kuyaona madhara leo vinaleta madhara makubwa sana kiafya baada ya miaka kadhaa.

Ilishafika kipindi nikaona basi nikubaliane tu na hii hali japo moyoni nilikuwa naumia maana nikijicheki ndio kwanza hata sijafika 35, Kwakweli hata biashara zangu za pembeni zilianza kumea na kunipa faida nzuri ila nikifikiria hili tatizo nilikuwa na stress.

KUmbe nilichokuwa sikijui tatizo lipo upande wangu, Nilikuwa nakosa muda wa kupumzika.

Mwaka jana woooote January Mpaka Decmber nilikuwa naingia kulala saa tisa hadi saa 11 na kuamka saa sita hadi saa nane, Ni mwaka mzima kazi yangu ilinihitaji kupiga shift usiku. Sikuweza kutimiza hata jukumu langu la kuwa mlinzi wa nyumbani sana sana nilitumia tu kamera za cctv kucheki mazingira, Mwenzangu nae ilikuwa changamoto kumaliza usiku mzima peke yake na watoto hapo nyumbani.

Sasa kuanzia mwaka huu hali imerudi kawaida naenda asubuhi saa mbili sometimes hata saa nne asubuhi, hivyo usiku nachapa usingizi na napumzika vya kutosha.


Nimekuja kugundua hivi sasa sio kwamba nimepata kiu ya kuendelea la tatu bali mishindo yangu imekuwa ya nguvu sana na ina last muda mzuri, hata mwenzangu kanisahangaa na kuhisi labda huko shift za usiku nilikuwa nina mchepuko ananichosha kabla sijaja kwake .

Nimekuja kugundua kupata usingizi wa kutosha ni dawa nzuri sana ya magonjwa mengi, mwaka jana pia nilikuwa na ukungu kwenye ubingo, kuna baadhi ya nyakati nilikuwa msahaulifu ila kwa sasa hadi najishangaa navyoweza kukumbuka mambo kwa urahisi.
Safi kabisa peleka moto kijana , kufa kwaja

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Usingizi ni suluhu ya matatizo mengi, jaribu sana ulale masaa yasiyopungua sita kila siku, pia hakikisha hubadilishi badilishi muda wa kulala, kama umejiwekea kulala saa tatu usiku, zikitimia tu, ingia kitandani jilaze, hata kama usingizi unakugomea wewe galagala humo tu kitaeleweka.
Zingatia mazoezi, lishe bora, kunywa maji mengi, pia tafuta vichekesho kama vile pranks, cheka kila siku.
Mbona mengine yatajileta tu, utapelekea moto sana.
 
Usingizi ni suluhu ya matatizo mengi, jaribu sana ulale masaa yasiyopungua sita kila siku, pia hakikisha hubadilishi badilishi muda wa kulala, kama umejiwekea kulala saa tatu usiku, zikitimia tu, ingia kitandani jilaze, hata kama usingizi unakugomea wewe galagala humo tu kitaeleweka.
Zingatia mazoezi, lishe bora, kunywa maji mengi, pia tafuta vichekesho kama vile pranks, cheka kila siku.
Mbona mengine yatajileta tu, utapelekea moto sana.
Na sio kulala masaa ya kutosha pekee bali kulala muda uliopangwa kulala ambao ni usiku na kuamka asubuhi.

Kuna nguvu kubwa sana kulala jua likizama na kuamka jua linapokaribia kuchomoza.

Kinyume na hapo ni kama unachanganya mafaili
 
Back
Top Bottom