Tukio la mabomu unachotakiwa kujua | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tukio la mabomu unachotakiwa kujua

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Yona F. Maro, Feb 18, 2011.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Feb 18, 2011
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Tukisema kwa lawama dhidi ya serikali ambazo zinatolewa na wananchi mbalimbali hii ni haki yao kabisa hakuna mtu anayepingwa kwa kutoa lawama zozote zile lakini tunapotoa lawama ni vizuri tuwe na vitu vya ziada yaani unatoa lawama huku ukiwa na suluhisho la suala hilo au ukiwa na mchango wa aina yoyote ambao unaweza kusaidia suala hilo .

  Tukio la mabomu la gongo la mboto na mbagala limetukumbusha mengi haswa suala la watu kuhamia sehemu za karibu na makambi ya jeshi hebu kwanza tuone historia fupi ya kambi hizi .

  Kambi ya gongo la mboto wakati inajengwa enzi hizo ilikuwa mbali sana na raia ila raia walikimbilia maeneo ya jirani na kambi hiyo kwa ajili ya kujihifadhi na shuguli zingine lakini wakati inajengwa ilikuwa mbali sana .

  Kambi ya lugalo nayo ilikuwa mbali sana pamoja na magorofa ya jeshi mwenge nayo yalijengwa kwa ajili ya wafanyakazi lakini yakaonekana yako mbali kwa wafanyakazi wa serikali ndio maana wanajeshi wakamwekwa hapo lakini ona sasa hivi wananchi walivyojaa pembeni mwa magorofa hayo .

  Kambi ya changanyikeni kuna rada ndio maana ni ngumu kwa baadhi ya sehemu raia kusogelea kwa sababu wanaweza kuonwa au kunasana kwenye mitego mengine ya maeneo hayo .

  Kambi ya mabibo nayo wakati inajengwa ilikuwa mbali na mji wakati ule soko la kariakoo linajengwa raia waliohamishwa kule walipewa nafasi maeneo ya mabibo unaweza kuona jinsi gani wakati kambi hizi zinajengwa zilivyokuwa mbali enzi hizo .

  SUALA LA KUHAMISHA KAMBI KUWA MBALI NA RAIA
  Kila mwananchi mwelewa anatakiwa ajue kwamba kambi hizo zimejengwa kwa gharama kubwa sana na kuhamisha kwenda sehemu nyingine pia inahitaji gharama kubwa pengine zaidi kutokana na gharama hizo basin a uwezo wa nchi yetu katika masuala mbalimbali yanayohusu fedha tusihoji kwanini kambi hazipelekwi mbali je nchi ina uwezo wa kujenga kambi zingine mbali zaidi na kama zikienda huko kwa maslahi ya nani ?

  SUALA LA WATU KUJIUZURU
  Kama nilivyosema hapo juu watu wengi hawajui mambo yanayoenda na kuendeshwa ndani laiti wangejua gharama za kuhifadhi mali hizo na kiasi cha bajeti kilichowekwa kwa ajili ya bidhaa hizo kama zinaendana sawa au la kama hazitoshi itasaidiwaje na sio kujiuzuru hata wakijiuzuru wale wanaokuja watapata wapi fedha na uwezo wa kuendesha shuguli hizo tukumbuke hii ni sekta nyeti kwa usalama na maslahi ya nchi yetu sio ya kuchezewa chezewa hovyo .

  KWA WASIOJUA .
  Hifadhi ya silaha inahitaji aina Fulani ya mazingira , hewa na matumizi mengine kama Grisi na mafuta mfano mzinga mmoja ile midigo iliyookotwa inatumia karibu lita 20 za mafuta kwa ajili ya kuosha kama una mizinga kama ile alfu 4 tu unaweza kupiga gharama za mafuta , grisi matunzo mengine .

  Halafu kuna hili tatizo la mgao wa umeme

  SULUHISHO .
  Matukio kama haya yanagusa sekta muhimu katika taifa yasitumiwe katika kujinufaisha kisiasa hata kidogo , wazalendo haswa wanasiasa kwenye vyama mbalimbali tumieni wataalamu na wajuzi wenu katika kuleta suluhisho mbadala la matatizo haya na sio kupiga domo bila suluhisho la msingi .

  NENO LA LEO
  USALAMA WA NCHI NA WATU WAKE UNAHUSU TAIFA LOTE LA WATANZANIA NA MALI ZAKE SIO CCM WALA JWTZ – WEWE TIMIZA WAJIBU WAKO KWA KULETA SULUHISHO LA KUDUMU KWA VITENDO
   
 2. L

  LAT JF-Expert Member

  #2
  Feb 18, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  i smell crap
   
 3. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #3
  Feb 18, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Holy Crap....!
   
 4. M

  Marytina JF-Expert Member

  #4
  Feb 18, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  naomba utuwekee hapa kiwango cha elimu yako ili tujue namna nzuri ya kukuelekeza,inawezekana huna matatizo ila uelewa na elimu yako ndio kikwazo cha kuanalyise tusije poteza muda bure.
   
 5. M

  Matarese JF-Expert Member

  #5
  Feb 18, 2011
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 519
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  He, shy umekuwa msemaji wa jeshi?
   
 6. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #6
  Feb 18, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,173
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  nimesoma concludsion tu na kouoona kuwa thhis is a crap at its best
   
 7. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #7
  Feb 18, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Hili jambo ndio ninalowaambia wapiga debe wa waziri ajiuzulu hata akija wa chadema atakutana na vizingiti hivyo hivyo wanachukulia kila kitu siasa tu!!!
   
 8. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #8
  Feb 18, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  isee kweli wakinamakamba wengi saana!
   
 9. W

  WildCard JF-Expert Member

  #9
  Feb 18, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Hatusemi wajiuzuru bali WAWAJIBIKE. Kama kile walichoshauri wakati ule wa Mbagala hakikufanyika watuambie.
   
 10. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #10
  Feb 18, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  :rain::rain: nasupport
   
 11. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #11
  Feb 18, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Upupu
   
 12. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #12
  Feb 18, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hilo suluhisho liko wapi? Mbona unaomba wengine tena walete suluhisho!

  1. Hifadhi ya silaha ni majukumu ya jeshi and they should do it safely and as economical as possible, nik jukumu la mganga wa kienyeji kuhifadhi tunguli zake zisidhuru watu wengine kama hilo linawezekana hivyo basik uzembe hauwezi kuvumilika eti kwa sababu ya gharama, je unawza kuquantify ni gharama kiasi gani ya watu waliopoteza maisha yao kule Mbagala na sasa Gongo la Mboto?

  2. Kwa hiyo viongozi wasijiuzulu wala kuwajibika eti hata hao wengine watashindwa?????? ebo???? This is too low for u mkuu......

  3. Nadhani Shy na wewe ni sawa na viongozi wetu wanaodhani thamani ya uhai wa masikini ni ndogo na hivyo inaweza kulingannishwa linganishwa tu na things like " Gharama za kuhamisha kambi ni kubwa". Hivi unaposema hizi kambi zilikuwa mbali ina maana kuwepo kwa watu karibu ndiyo kumesababisha mabomu kulipuka tena zaidi ya mara moja? After all wakati planning za haya makambi zinafanyika ina maana haikufikiriwa kwamba D'salaam itakuja kukua?

  4. Lazima utambue and this has been proven, watu wanaoongoza kuishi maeneo yasiyopimwa ni wanajeshi na ndio maana kandokando ya kila kambi ya jeshi hapo Dar kuna makazi yasiyopimwa na mengi yao yanamilikiwa na wanajeshi wastaafu na ndiyo haswaa walioanza kuvamia maeneo hayo kabla ya wananchi wengine, look at Kawe, Kigamboni, Ubungo Kibangu, Kunduchi, Mabibo, Changanyikeni etc............ Hata serikali nao wakulaumiwa basi ilikuwaje wajenge Airport karibu na kambi ya jeshi na maghala ya silaha? Ujenzi wa chuo cha takwimu kule Changanyikeni, Mabibo hostel, Jengo jipya la TAA etc.

  Mkuu nikisoma thread yako vizuri ni kama unataka kusema wananchi ndiyo wenye makosa, kama huo ndiyo msimamo wako u r wrong, very wrong!
   
 13. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #13
  Feb 18, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145


  mkuu huu ni utetezi wakijinga saana tunakatwa kodi kubwa sana kwenye mishahara yetu kazi mojawapo yakufanyia ni hiyo ya kulinda, kununua mabom mengine. unaposema gharama unamaanisha nini!?

  na je hizo gharama zipo tz tu na zimeanza saizi! msitoe uteteza wakiivyo niwakijinga sana mkuu jiandaeni upya, na mnaposema umeme kwavipi sasa, si bora mngekata umemesehemu zoote mkaacha huko na huwa mnafanya hivyo na hakuna mtu anayewalaumu leo mnasema nini!

  TATIZO VILAZA WENGI KWENYE GVMT HII.
   
 14. Iramusm

  Iramusm JF-Expert Member

  #14
  Feb 18, 2011
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 424
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Nimeisoma mada lufika mwisho nkajiona kama nimepoteza muda vile!!!!
   
 15. G

  Gathii Senior Member

  #15
  Feb 18, 2011
  Joined: Feb 9, 2011
  Messages: 164
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Daah kweli tunatofautiana.

  Ndugu yangu wewe Mtanzania kweli? Anayeishi na kuona yote yanayotokea?

  1. Mikataba tata ya madini
  2.EPA
  3.RICHMOND+DOWANS.
  4.Milipuko ya Mbagala

  ...na hata Kilichotokea baada ya tukio lenyewe la Gongo la Mboto, waheshimiwa kusema hawana habari hata saa moja baada ya milipuko kuanza,waheshimiwa wengine kulipongeza jeshi n.k na nini kinafanyika juu ya yote hayo yaliyotokea,nini kauli na vitendo vya viongozi wetu tuliowapatia dhamana..


  Kama unaona yote hayo na bado unaona watu kulaumu yaliyotokea gongo la mboto basi nakupa hongera ndg yangu,na walio kuuliza level yako ya Elimu nawasihi wakuache mkuu, wakusamehe tu.
   
 16. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #16
  Feb 18, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  Suala si kupanuka kwa mji...hapo tunalalamikia usalama wake why yalipuke? Hata kama kambi ingekuwa msata!!
  Wanasema ufinyu wa bajeti ulifanya washindwe kuyaharibu...je ufinyu huu hauwahusu wale waheshimiwa waliopewa 90m kila mmoja majuzi kule dodoma?
   
 17. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #17
  Feb 18, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Tangu jana nilishasema, kuvielimisha vichwa vibovu kama shy ni kupoteza muda tuu.
   
 18. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #18
  Feb 18, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Kumbe wee SHY ni **** (TUSI) sana?

  Unaandika upupu gani hapo juu? Huu utetezi wako, hata bibi yako angelitowa utetezi wa maana kuliko huo.

  Kwani nani kasema wahamishe kambi za jeshi? Hayo makambi acha yabaki tu hapohapo yalipo.

  Wabakize bunduki na risasi tu. Sisi hatuna noma nazo na kweli kuhamisha kambi ni aghali sana.

  ILA HAYO MABOMU, kama hawawezi kuyahamisha basi wayauze kwa Museven au Rwanda kama siyo Congo.

  Ningelikuwa nimefyatuka basi ningelisema hayo mabomu Wayachukue na wajishindilie .............unajua wapi.

  ANGALIZO: Shimbo alishakuwa na nyumba ndogo familia ya SHY.
   
 19. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #19
  Feb 18, 2011
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Kwa vyovyote vile ,serikali yote inatakiwa ijiuzuru
   
 20. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #20
  Feb 18, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Inanukaaaaaaaaaaaa
   
Loading...