Tukio la mabomu unachotakiwa kujua

Kujiuzuru ni lazima. Kwa maana tukio hilo hilo linajirudia tena na tena. Kwa tafsiri yangu kiongozi husika yaani waziri wa ulinzi kaonesha uwezo mdogo mno wa kusimamia wizara yake. Tukiendekeza hili, tusishangae makubwa yatakayokuja mbele yetu.
 
Hakuna haja ya kuunda tume au baraza la kuchunguza matukio haya. Msemaji wa TPDF Brigedia Shy amemaliza kutoa utafiti wake.

This research stinks.
 
Naamini kama tunaweza kubadili magari ya kifahari kwa ajili ya wabunge na viongozi wengine kila baada ya muda mfupi hatuwezi kushindwa kubadili au kuharibu mabomu yaliyopita muda wake. Mungu tuongoze.
 
upuuzi at max level, we ulitaka na sisi tukashiriki kuyahifadhi hayo mabomu?
 
WANANCHI HATUKO SALAMA TENA NA MALI ZETU, KIIO KILA LEO NA MAYATIMA
KUONGEZEKA HIVYO SERIKALI NZIMA IJIUZULU HATA KABLA YA MAANDAMANO
YA KUTETEA 'UHAI WA WENZETU' KUANZA KOTE NCHINI


Mheshimiwa Kikwete kama amiri jeshi mkuu ajiuzulu pamoja na serikali yake. Jukumu la msingi halijazingatiwa; wananchi hatuko salama!! Tusianze kuzungusha kiswahili hapa ni uhai umepotea kwa uzembe!!! Hawa mayatima wanahitaji sauti zetu!!

Hatutaki tena tume kwa hata kule Mbagala chombo kama hicho hakikutusaidia zaidi ya kuwapa wanasiasa na makampuni ya kibiashara kujinadi kwenye kioo cha televisheni mgongoni mwa msiba na damu kwa wengine.

Jukumu la kwanza la kuhitajika uwepo wa serikali katikati yetu NI KUHAKIKISHA USALAMA KILA MMOJA WETU NA MALI ZETU. Kwa mtaji hizi picha nilizoona, serikali nzima ya CCM ijiuzulu mara moja

Mauaji Arusha walitupuuza kana kwamba kuliuaua nzi tu. Kule kwenye mashamba ya mpunga wala hawakujishughulisha kitu kuwajibika mtu. Sasa kama kweli kuna JAMBO AMBALO KIUKWELI KABISA KINATUHITAJI KUANDAMANA MPAKA KUELEWEKE NI KATIKA KUTETEA UHAI WA WENZETU.

Kama tutaona vifo hivi kama vile ni ya 'akina wale' na kwamba sisi wengine hatuhusiki basi hapo ndipo kiama chetu kinapoanzia. Kwa vifo hivi vyote 17 taifa tumepata yatima wangapiii?????????????
 
Hivi hayo mabomu wanayanunua ya nini kama kuyatunza tu yanawashinda shame on you JK mbona hatujasikia Rwanda,Kenya,Uganda yakilipuka kwa nini ni hapa Tanzania tena Dar pekee ilpotokea Mbagala wakasema haitatokea tena sasa Gongola mbote je?
Hapa lazima watu waonyeshe uwajibikaji huu ni uzembe wa hali ya juu:decision::decision::decision:
 
..inavyoelekea kuna watu ambao hawafuati kanuni za uhifadhi wa hayo mabomu.

..kuna uzembe unaoendelea mahali fulani na kusababisha hayo mabomu yakalipuka.

..madai kwamba raia wamewafuata wanajeshi huko porini walipokuwa wameweka kambi hayana msingi.

..je, ni nani alitoa kibali kwa wananchi kujenga karibu na kambi la jeshi?

..JWTZ nao walichukua hatua na juhudi gani kuzuia ugawaji viwanja karibu na makambi yenye silaha za hatari kama hapo Gongolamboto?

..baada ya wananchi kuwa wameshajenga karibu na kambi la Gongolamboto, JWTZ walichukua hatua gani za kiusalama[safety & security measures] kuepusha ajali kama iliyotokea?
 
Wewe shy ni msen......malizia mwenyewe hata kama nikiongozi umejibadilisha jina ku@;"@&$);:?'#^*#€ma weww huwezi andika as if huelewi sawa wamejenga serikali ilikuwa wapi kuwazuia wasijenge...hala kama wewe si mjinga wa wajinga,wewe umetoa solution ipi kama gharama ya kuhamisha ni kubwa acha kutafuta cheap popularity unakuwa mpumbavu kama si mtanzania unati&$@%^£><<€+=]}a nini? **** mkubwa umeniudhi walai ningekujua nakushoot wacha nikanyeee debe.....
 
hii serikali bwana ni kichekesho kabisa,
nilikuwa naongea na Mwananjeshi mmoja ananiembia kuwa hayo mabomu mengiu yalikuwa ni ya mwaka 1971,1972..etc
inasemekana walikuwa wakipewa pesa kila mwaka kununua mapya na vifaa vingine jamaa wanaweka kibindoni na kuthaminisha hayo yaliyo expire.
Ni uwazi usiopingika kuwa wanajeshi woye walijua kuwa hayo mabomu yangeweza kulipuka mda wowote
hivyo si ajabu wote wakawa wameshakimbia nyumba zao kabla ya mlipuko
wasingeweza kutoa taarifa kwa wannchi kwani waliogopa kujulikana kuwa walijua litatokea na kwa nini walishindwa kuyazuia mapema?
Hivyo hilo lilijulikana, na kama hawajafa ..inawezekana kabisa ikawa hivyo
Hata jamaa yangu kanieleza kuwa hakuna mwanjeshi hata mmoja aliyekufa( unless kama ameniingiza mjini kwa hilo):usa2:
 
Tutaachaje kuilauumu serikali wakati ndiyo inayoongoza na haijawahi kupata kuwepo nyingine baada ya Uhuru? Inamaana kuwepo kwao kuna maanisha nini kama si kuongoza? Na kuoongoza maana yake ni nini si ni pamoja na kupangilia makazi ndani yake kukiwepo ulinzi wa mali na uhai wa raia wake? Si serikali hiihii inayo ratibu vifo na uzazi ama....

Tutaacha kuilaumu iwapo kama kwa miaka kadhaa ya uhuru raia waligoma kulipa kodi ya kufanya shughuli za serikali kama sivyo lawama haikwepeki ndiyo maana waliomba kutuongoza na ulinzi na usalama wa raia na mali zao ni moja la jukumu kuu la serikali; wamebeba hiyo dhamana na hakuna mwingine mwenye hiyo dhamana! Kama watashindwa na kama wataomba kusaidia basi wawapishe wenye uwezo...Roho za binadamu si za kuku ambaye unaweza mchinja saa yeyote ile unapotaka bila kujali vitetea vyake vitabaki vipi let us be serious!
 
tukisema kwa lawama dhidi ya serikali ambazo zinatolewa na wananchi mbalimbali hii ni haki yao kabisa hakuna mtu anayepingwa kwa kutoa lawama zozote zile lakini tunapotoa lawama ni vizuri tuwe na vitu vya ziada yaani unatoa lawama huku ukiwa na suluhisho la suala hilo au ukiwa na mchango wa aina yoyote ambao unaweza kusaidia suala hilo .

Tukio la mabomu la gongo la mboto na mbagala limetukumbusha mengi haswa suala la watu kuhamia sehemu za karibu na makambi ya jeshi hebu kwanza tuone historia fupi ya kambi hizi .

Kambi ya gongo la mboto wakati inajengwa enzi hizo ilikuwa mbali sana na raia ila raia walikimbilia maeneo ya jirani na kambi hiyo kwa ajili ya kujihifadhi na shuguli zingine lakini wakati inajengwa ilikuwa mbali sana .

Kambi ya lugalo nayo ilikuwa mbali sana pamoja na magorofa ya jeshi mwenge nayo yalijengwa kwa ajili ya wafanyakazi lakini yakaonekana yako mbali kwa wafanyakazi wa serikali ndio maana wanajeshi wakamwekwa hapo lakini ona sasa hivi wananchi walivyojaa pembeni mwa magorofa hayo .

Kambi ya changanyikeni kuna rada ndio maana ni ngumu kwa baadhi ya sehemu raia kusogelea kwa sababu wanaweza kuonwa au kunasana kwenye mitego mengine ya maeneo hayo .

Kambi ya mabibo nayo wakati inajengwa ilikuwa mbali na mji wakati ule soko la kariakoo linajengwa raia waliohamishwa kule walipewa nafasi maeneo ya mabibo unaweza kuona jinsi gani wakati kambi hizi zinajengwa zilivyokuwa mbali enzi hizo .

Suala la kuhamisha kambi kuwa mbali na raia
kila mwananchi mwelewa anatakiwa ajue kwamba kambi hizo zimejengwa kwa gharama kubwa sana na kuhamisha kwenda sehemu nyingine pia inahitaji gharama kubwa pengine zaidi kutokana na gharama hizo basin a uwezo wa nchi yetu katika masuala mbalimbali yanayohusu fedha tusihoji kwanini kambi hazipelekwi mbali je nchi ina uwezo wa kujenga kambi zingine mbali zaidi na kama zikienda huko kwa maslahi ya nani ?

Suala la watu kujiuzuru
kama nilivyosema hapo juu watu wengi hawajui mambo yanayoenda na kuendeshwa ndani laiti wangejua gharama za kuhifadhi mali hizo na kiasi cha bajeti kilichowekwa kwa ajili ya bidhaa hizo kama zinaendana sawa au la kama hazitoshi itasaidiwaje na sio kujiuzuru hata wakijiuzuru wale wanaokuja watapata wapi fedha na uwezo wa kuendesha shuguli hizo tukumbuke hii ni sekta nyeti kwa usalama na maslahi ya nchi yetu sio ya kuchezewa chezewa hovyo .

Kwa wasiojua .
Hifadhi ya silaha inahitaji aina fulani ya mazingira , hewa na matumizi mengine kama grisi na mafuta mfano mzinga mmoja ile midigo iliyookotwa inatumia karibu lita 20 za mafuta kwa ajili ya kuosha kama una mizinga kama ile alfu 4 tu unaweza kupiga gharama za mafuta , grisi matunzo mengine .

Halafu kuna hili tatizo la mgao wa umeme

suluhisho .
Matukio kama haya yanagusa sekta muhimu katika taifa yasitumiwe katika kujinufaisha kisiasa hata kidogo , wazalendo haswa wanasiasa kwenye vyama mbalimbali tumieni wataalamu na wajuzi wenu katika kuleta suluhisho mbadala la matatizo haya na sio kupiga domo bila suluhisho la msingi .

Neno la leo
usalama wa nchi na watu wake unahusu taifa lote la watanzania na mali zake sio ccm wala jwtz – wewe timiza wajibu wako kwa kuleta suluhisho la kudumu kwa vitendo http://www.mnyonge.blogspot.com/


unastahili kunyongwa tafadhali jitokeze hadharani kama kweli utanusurika kwa kauli za kijinga kama hizi! Go to hell~
 
Unafuga simba huku humpi nyama ale unategemea aache kukutafuna?
Ni heri hayo mabomu yasinunuliwe mbona yanasababisha hasara kwanza kuyanunua kwa pesa zetu adimu halafu kuua mnunuzi!
Jiulize je hao waliojenga karibu na kambi ni chanzo cha milipuko?
Kwa sababu si hao tu walio umia. haya mabomu yamefika hadi mbezi Tabata na maeneo mengine ya mbali toka glamboto.
Wote tumeumia kwa sababu mabilioni ya pesa yalitumika kununua hayo mabomu. Na mabilioni pia yatatumika kufidia wahanga wa hayo mabomu.
Hapo lazima mtu awajibike tu
ili UZEMBE huu USIJIRUDIE.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom