Tukio la Familia ya Mzee Ishengoma kuvamiwa usiku Dar, wanaishi kama Digidigi, mmoja anusurika kifo mara 3, waomba msaada kwa Rais Samia

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
422
1,049
Hofu imetanda kwa familia ya Mzee Ishengoma ya Goba Jijini Dar es Salaam baada ya hivi karibuni kundi kubwa la watu ambayo idadi yao haikujulikana mara moja kuivamia familia hiyo nyakati za usiku na kufanya uharibifu mkubwa wa mali.

Tukio hilo ambalo limeripotiwa tayari katika Kituo cha Polisi Goba na kufunguliwa jalada la uchunguzi namba GBA/RB/2370/2023 KUHARIBI MALI, inaelezwa lilitokea majira ya saa tano za usiku wakati familia hiyo ikiwa ndani imelala.

Kwa mujibu wa mtoto mkubwa wa familia, Dickson Ishengoma (36), ameiambia Times FM kuwa siku ya tukio wakiwa wamejipumzisha ndani alisikia kelele za ndogo wake kwamba wamevamiwa na vibaka.

Anasema baada ya kusikia kelele hizo, alichukuwa muda akiwa ndani kwake kujua kinachoendea na ndipo aliposikia sauti ya wavamizi wakiwa wanaulizia alipo.

"Baada ya kumkamata mdogo wako walianza kumpiga na kumuuliza wapi nilipo....mdogo wangu aliwadanganya wakaenda upande ambao sikuwepo na hapo ndipo nilipojua kwamba watu hao watakuwa na nia mbaya na Mimi," anasema Dickson.

Aliendelea kusema kuwa kutokana na kunusurika kifo katika matukio matatu tofauti, aliamua kujificha ndani ya nyumba hiyo hadi watu hao walipoondoka na kuahidi kurudi tena."

"Kipindi chote ambacho walikuwa nje wakimtesa mdogo wangu, kundi jingine likawa linafanya uharibifu wa milango na madirisha. Wamehatibu vitu vingi sana hadi sasa," anaeleza.

Awali, Dickson Ishengoma aliiambia Times FM kumekuwa na mgogoro wa ardhi kati ya familia ya Mzee Ishengoma Mfanyabiashara aliyetajwa kwa jina la Timoth Kilumile ambaye miaka ya nyumba alikuwa rafiki ya baba yao.

Anasema katika kipindi chote ambacho walikuwa na urafiki na baba yao hawakuwahi kuambia kama nyumba tunayoishi ni yake na hata yeye (Kilumile) alikuwa akiishi hapa nyumbani hakuwahi kusema nyumba hii ni yake!

Anasema anashangaa baada ya baba yao kupotea katika Mazingira tatanishi mwaka 2018 mfanyabiashara huyo ameibuka na kudai kiwanja na nyumba hiyo ni mali yake.

"Kutokana na madai hayo Mzee Kilumile alikwenda Polisi Goba akiwa na hati ya kiwanja na sisi tukaitwa lakini alipoulizwa kuhusu hati aliyonayo hakuwa na majibu yanayoeleweka! Sisi tukamuomba kama una uhakika eneo ni lake aende Mahakamani tutakuwa kujibu huko," anasema Dickson Ishengoma.
af9102c5-fe78-4fbc-bd64-c01ea588ad36.jpg

Majeraha aliyoyapata Dickson Ishengoma kutokana na misukosuko ya mgogoro huo

Akaongeza, "Unajua Mzee Kilumile pia ana nguvu ya mtoto wake ambaye anacheo kikubwa na yupo JWTZ na hata kuna askari fulani waliwahi kuniambia niwe makini maana Kilumile anawatu wazito nyuma yake."

Tofauti na matarajio yao, usiku wa Julai 6, 2023 kundi la watu wenye silaha mbalimbali walivamia nyumba hiyo na kufanya uharibifu mkubwa wa mali.

"Kinachonishangaza mgogoro wa familia hii nilishaufikisha kwenye vyombo vya usalama hasa Jeshi la Polisi lakini hakuna msaada niliopata hadi sasa! Ofisi ya DCI wanajua, Kanda Maalumu Dar es Salaam wanajua na hata Polisi Goba wanajua lakini hakuna msaada! Natamani mama yangu na Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan anisaidie," anasema.
7821395f-ca7e-4ec1-9da3-8b79533b5166.jpg
Ishengoma anasema alipofikisha suala lake kwa DCI alihakikishiwa suala lake litafanyiwa kazi na kweli baada ya siku tatu alipigiwa simu na mtu aliyejitambukisha kwa jina la Logati Mushi toka Makao Makuu ya Polisi Dodoma na kumpa maelekezo ya kwenda ofisi ya ZCO Dar es Salaam.

"Nilipokwenda kwa ZCO nilikutana na mtu aliyejitambukisha kwangu kuwa ni Msaidizi wa ZCO aliniambia anaitwa Amin Mahamba naye tangu hapo nikipiga simu zangu hapokei," anasema.

Anasema kwasasa hawajui nini wanapaswa kufanya na familia ipo kwenye hofu kubwa kutokana na vitisho ambavyo wanaendelea kuvipata toka kwa mfanyabiashara huyo.

Katika kutafuta ukweli wa mambo, Times FM ilimtafuta kwa njia ya simu Logati Mushi ambapo baada ya kumuuliza kama anafahamu lolote kuhusu sakata la Dickson Ishengoma alikiri kulifahamu.

Mushi alisema alipopokea taarifa toka Ofisi ya DCI Dar aliwasiliana na Ishengoma na kumtaka kwenda kwa ZCO Dar kwa ajili ya msaada zaidi.
6a8f5840-ce5f-47bc-83da-c4d415aa0b25.jpg

Nyumba iliyofanyiwa uharibifu na watu wasiojulikana

"Unajua Mimi nilimsikiliza Bw. Ishengoma peke yake kwa hiyo nikamuomba aende Kanda Maalumu Dar kwa ZCO ili wao waone namna ya kukutana na pande zote mbili na kutafuta muafaka. Hadi sasa sijui wamefikia wapi lakini naomba niachie nijaribu kufuatilia," alisema Mushi.

Aidha, jitihada za kumpata mfanyabiashara Timothy Kilumile siku nzima ya Ijumaa Julai 7 na Jumamosi Julai 8 hazikuzaa matunda. Muda wote simu yake iliita bila kupokelewa.

Hata hivyo, Jumapili Julai 9, 2023 mfanyabiashara huyo alipatikana kupitia namba yake ya simu na alipoulizwa kuhusu tukio la uporaji wa kiwanja na nyumba ya familia ya Mzee Ishengoma, aliomba atafutwe baadae kwa sababu alikuwa kanisani.

"Naomba nikutafute baadae kwasasa nipo kwenye ibada kanisani."

Hata hivyo, hadi saa 7:15 jioni Bw. Kilumile hakupiga simu kama alivyoahidi! Hata alipopigiwa hakupokea.

Jitihada za kumpata Bw. Amin Mahamba ambaye ametajwa kuwa ni Msaidizi wa ZCO Dar hazikuzaa matunda. Muda wote simu yake haikuwa na majibu. Aidha, Kamanda Kanda Maalumu Dar es Salaam Jumanne Muliro pia siku kila ilipopigwa iliita bila kupokelewa.

Times FM tutaendekea kuwatafuta viongozi hao kujua ukweli na undani wa sakata hili.

CHANZO: RADIO TIMES FM

Pia Soma

1) > Mdau: Baada ya baba kupotea, rafiki yake ametuma watu wenye silaha kuvamia nyumba yetu akitaka tuhame

2) > UNDANI WA KIGOGO WA MAFUTA ALIYETEKWA DAR

3) >
View: https://x.com/AbroadTanzania/status/1678301941867364355?s=20
 
Haya mambo huwa ukisikiliza upande mmoja unaweza fikiri mtu anaonewa...

IN THE HIGH COURT OF TANZANIA
(DAR ES SALAAM DISTRICT REGISTRY)
AT DAR ES SALAAM
MISCELLANEOUS CIVIL APPLICATION NO. 479 OF 2022
(Originating from the High Court of Tanzania, Dar es Salaam
District Registry in Civil Case No 167 of 2016)
CRDB BANK PLC............................................................................ APPLICANT
VERSUS
TIMOTH DANIEL KILUMILE CO. LTD..................................... 1st RESPONDENT
DAWSON BUBERWA ISHENGOMA........................................2nd RESPONDENT
RULING

Baba yako hayupo hapo na huyo mwenzake? Hii kesi iliishaje unajua?

Lazima wana mambo yao, wamezulumiana. Ndo maana wanapambana

Na ukiona mtu kakusikiliza na hapokei simu, pengine kajua ukweli.
 
Poleni kwa maswaibu,

Ila kama Mwenye Hati ya Nyumba ni Thimothy sioni kama mtafika popote kungangania mali ambazo si zenu.

Mali zinatafutwa kwa jasho na ni bora mtafute zenu kuliko muendelee na ujeuri wa kuhama kwenye nyumba ya mtu.
 
Haya mambo huwa ukisikiliza upande mmoja unaweza fikiri mtu anaonewa...

IN THE HIGH COURT OF TANZANIA
(DAR ES SALAAM DISTRICT REGISTRY)
AT DAR ES SALAAM
MISCELLANEOUS CIVIL APPLICATION NO. 479 OF 2022
(Originating from the High Court of Tanzania, Dar es Salaam
District Registry in Civil Case No 167 of 2016)
CRDB BANK PLC............................................................................ APPLICANT
VERSUS
TIMOTH DANIEL KILUMILE CO. LTD..................................... 1st RESPONDENT
DAWSON BUBERWA ISHENGOMA........................................2nd RESPONDENT
RULING

Baba yako hayupo hapo na huyo mwenzake? Hii kesi iliishaje unajua?

Lazima wana mambo yao, wamezulumiana. Ndo maana wanapambana

Na ukiona mtu kakusikiliza na hapokei simu, pengine kajua ukweli.
Naona jamaa wameamuwa kutumia mahakama ya Gachacha, maana hizi mahakama rasmi zinapindisha sana haki.

Halafu Ishengoma ni Mhaya.
 
Haya mambo huwa ukisikiliza upande mmoja unaweza fikiri mtu anaonewa...

IN THE HIGH COURT OF TANZANIA
(DAR ES SALAAM DISTRICT REGISTRY)
AT DAR ES SALAAM
MISCELLANEOUS CIVIL APPLICATION NO. 479 OF 2022
(Originating from the High Court of Tanzania, Dar es Salaam
District Registry in Civil Case No 167 of 2016)
CRDB BANK PLC............................................................................ APPLICANT
VERSUS
TIMOTH DANIEL KILUMILE CO. LTD..................................... 1st RESPONDENT
DAWSON BUBERWA ISHENGOMA........................................2nd RESPONDENT
RULING

Baba yako hayupo hapo na huyo mwenzake? Hii kesi iliishaje unajua?

Lazima wana mambo yao, wamezulumiana. Ndo maana wanapambana

Na ukiona mtu kakusikiliza na hapokei simu, pengine kajua ukweli.
Mkuu Kuna mambo unayajua kuhusu huu mgogoro, saidieni hao vijana.

Ila ninachoshangaa ni vijana wa zaid ya miaka 30 kukaa kwao😂
 
Hofu imetanda kwa familia ya Mzee Ishengoma ya Goba Jijini Dar es Salaam baada ya hivi karibuni kundi kubwa la watu ambayo idadi yao haikujulikana mara moja kuivamia familia hiyo nyakati za usiku na kufanya uharibifu mkubwa wa mali.
Niliuliza maswali mengi kuhusiana na suala hili, mleta hoja kamwe hakuweza kujitokeza na kujibu hoja husika. Nafikiri hawa watu wanapaswq kutafuta suluhisho sahihi kuhusu mgogoro huu uliopo.
 
Haya mambo huwa ukisikiliza upande mmoja unaweza fikiri mtu anaonewa...

IN THE HIGH COURT OF TANZANIA
(DAR ES SALAAM DISTRICT REGISTRY)
AT DAR ES SALAAM
MISCELLANEOUS CIVIL APPLICATION NO. 479 OF 2022
(Originating from the High Court of Tanzania, Dar es Salaam
District Registry in Civil Case No 167 of 2016)
CRDB BANK PLC............................................................................ APPLICANT
VERSUS
TIMOTH DANIEL KILUMILE CO. LTD..................................... 1st RESPONDENT
DAWSON BUBERWA ISHENGOMA........................................2nd RESPONDENT
RULING

Baba yako hayupo hapo na huyo mwenzake? Hii kesi iliishaje unajua?

Lazima wana mambo yao, wamezulumiana. Ndo maana wanapambana

Na ukiona mtu kakusikiliza na hapokei simu, pengine kajua ukweli.
Kwahiyo kwenye hii kesi CRDB ndio wamepewa nyumba au? Sasa si watumie dalali wa mahakama?
 
Mkuu Kuna mambo unayajua kuhusu huu mgogoro, saidieni hao vijana.

Ila ninachoshangaa ni vijana wa zaid ya miaka 30 kukaa kwao😂

Ha ha ha! Na Baba yao kakimbia, kama kala vya watu halafu kakimbia sasa inakuwaje? Yawezekana Mzee wa watu kauza Nyumba mambo yake magumu, wao wanakomaa tu.
 
Haya mambo huwa ukisikiliza upande mmoja unaweza fikiri mtu anaonewa...

IN THE HIGH COURT OF TANZANIA
(DAR ES SALAAM DISTRICT REGISTRY)
AT DAR ES SALAAM
MISCELLANEOUS CIVIL APPLICATION NO. 479 OF 2022
(Originating from the High Court of Tanzania, Dar es Salaam
District Registry in Civil Case No 167 of 2016)
CRDB BANK PLC............................................................................ APPLICANT
VERSUS
TIMOTH DANIEL KILUMILE CO. LTD..................................... 1st RESPONDENT
DAWSON BUBERWA ISHENGOMA........................................2nd RESPONDENT
RULING

Baba yako hayupo hapo na huyo mwenzake? Hii kesi iliishaje unajua?

Lazima wana mambo yao, wamezulumiana. Ndo maana wanapambana

Na ukiona mtu kakusikiliza na hapokei simu, pengine kajua ukweli.
NDio ujeruhi watu kweli ,kama kweli una haki si uweke mambo hadharani kuliko kutishia maisha watu,jitu linaenda kanisani halafu linataka kudhulumu yatima, atakuwa anaenda kuimba huko kanisani
 
Back
Top Bottom