Tujiulize: Kwanini ghafla vifo vimekuwa vingi?

Tujiulize: Kwanini ghafla vifo vimekuwa vingi?

Jamani kwanini serikali yetu inaficha Mambo Kama China Communist part ya shimpiing? Watu wanakufa hawatangazwi, wagonjwa wengi, hapa Dodoma Hospitali ya Benjanimi Kuna wagonjwa zaidi ya 15, na general Kuna wagonjwa zaidi ya 10, mpaka wataalamu wamesema msimlete Bibi yenu Tena huku Hali mbaya, Basi angalau watangaze tujue
Uandishi wako huwa unanikosha sana mkongwe.
Maadam majina ya hao 10 hayajatolewa, hivyo naomba tusianze udhalilishaji wa marehemu wa watu!. Please!.
Tanzania waliokufa kwa Corona ni 10 tuu!.
P
Kwenye Corona, tunatumia taarifa rasmi pekee. Kwa mujibu wa taarifa rasmi za vifo vya Corona kwa Tanzania is only 10!. Wengine wote waliofariki bila kipimwa, wamekufa kwa matatizo mengine, na hata kama ni Corona, bila kupimwa na kuthibitishwa kuwa ni Corona, inakuwa ni wamekufa kwa maradhi mengine!.
P


Msikilize Prof kutoka Tabora​
Mwana familia pole sana. Watanzania tufike mahali tufahamu kwamba kazi ambayo JPM anaifanya ni kwa ajili ya Watanzania wote. Wakati wa JK misururu ilijaa kwenda India, ni kweli tumepiga hatua kubwa sana lakini bado tunahitaji kukaza kamba kwa sababu wapo wengi ambao wanapiga vita uimarishwaji wa huduma hapa Tanzania kwa sababu ya ubinafsi. JPM yeye kaonyesha njia Watanzania tuipende nchi yetu na tusijifanye hatufahamu yaliyotokea wakati wa Mzee rukhsa na BWM na JMK. Ni wakati wa kutetea rasilimali na kuona keki ya Taifa inawafaidisha Watanzania.

Just imagine AIDS, Ebola inatengenezwa ili tu kuua watu? Hata misaada tu wanaweka dawa kutumaliza then kuna vinguchiro vimo humu JF vinawatetea baada ya kulishwa peremende. Tuwe makini na tupiganie taifa letu.
Kwa hii komenti
IMG-20200424-WA0008.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwezi huu tumeanza kusikia vifo vingi bila kuambiwa vimetoka wapi. Wiki hii moja tu kuna wazee baba wa rafiki na Mama wa rafiki wamefariki kwa mazingira kama ya Corona ya homa, kushidwa kupumua na kukohoa. Wato walikuwa na magojwa mwngine na miaka zaidi ya 68.

Uchunguzi uliofanywa kwenye state ya new york kwa kuchunguza watu 3000 ambao hawaumwi wamekuta 14% kwa jimbo zima na 20% kwa mji mkuu wa New york wameumwa na kupona bila kujua hivyo kuna mengi ambayo hatujui kuhusu huu ugojwa.

Ushauri wangu kwanza wafiche wazee wako kama wapo na waelimishe, pili serikali ipime watu zaidi kama inawezekana na tatu ni lazima wahauri watu wasiwnde sehemu ambazo si za lazima.

Yaani huu ugojwa unachochoe magojwa watu walionao wazidiwe hivyo wenye pumu utaambiwa ni pumu, wenye kisukari hivyo hivyo hatutajiua idadi lakini tukiona misiba gafla inakuwa mingi tujiulize kwanini sana


Nimepata habari mbaya leo jumapili asubuhi rafiki yangu kafariki kwa Corona na wazazi wangu wanasema kuna jirani naye kafariki.
 
We ni muongo, mchina katangaza baada ya vifo kuisha na kudhiti ugonjwa, tena ni baada ya research ya chuo flani huko kutoa hesabu upya.
Hivi sisi tuko mwanzoni au mwisho wa corona?

Wewe unazungumzia mwishoni China, topic inauliza kwa nini ghafla vifo vimeongezeka? Ndio nikatoa jibu kwamba China pia vifo vya mwanzo (mwezi wa 12 mwaka jana) walitaka kuficha lakini baada kuona maambukizi yana kasi na watu wanapoteza maisha, wakaona waanze kutangaza vifo kutokana na hali halisi.

Unacho zungumzia ni kitu kingine tofauti. Swala la China kudanganya idadi ya waliokufa ni topic nyingine, tunazungumzia "kwanini ghafla vifo vimekuwa vingi?".
 
Woga na unafiki Ni kitu kibaya Sana...mwaka huu watu watajifunza kuwa kupiga kura Ni Ni suala linalohusu maisha ya na kizazi chote.Tanzannia huwa tunachukulia Siasa za Nchi Kama Ushabiki ea Simba na Yanga.
Hizi tetesi zonazoendelea kuhusu Hali ya ugonjwa wa Kakorona'' hapa nchini zinshitaji kuwekwa saws.Kama Ni uongo kwa faida faida ya Nani!
Na kwa Nini watu wazushe kuhusu vifo.
Kwa Nini taarifa kuhusu kujikinga zinatolewa kwa kukinzana.Ingekuwa nchi za wenye hofu ya MUNGU Naibu Wazir wa Afys na RC Dar wangeomba kupumzika
Vyombo vya habari vyote vimeshindwa kufanya uchunguzi wa tetesi zonazoendelea,wanalinda ugali wao.
Ukiangalia mwenendo wa Korona kwa nchi nyingi ...hakika Tanzania inahitaji Neema ya Mungu kuliko nchi hizo...Sasa Sina uhakika Kama Mungu yupo hivi!

Umeandika Kwa uchungu Sana mkuu, pole Sana mkuu

Tanzania iliwekwa mikononi mwa Mungu, Tumeanza kuona matendo makuu ya Mungu kutendeka, wagonjwa wengi kwa mkupuo kupona, Kutokuongezeka wagonjwa wapya ama kupungua kabisa, Sasa Wakati Mungu anatenda makuu, ni kweli wale wenye Imani haba, kupoteza kupo

Tulizana mkuu, Tanzania tunakwenda kuuona ukuu wa Mungu wetu hata kwako hattatokea mwenye maambukizi na Kwa majirani zako pia, Kwa Imani inawezekana
 
Mpaka Corona ikiisha wangapi humu jf watakuwa hai...hii K vant ya wapi😁😁😁
 
Hii ni habari ya kweli kabisa.
 

Attachments

  • 57088F93-0716-489B-AB43-A4250931FE5B.jpeg
    57088F93-0716-489B-AB43-A4250931FE5B.jpeg
    30.9 KB · Views: 9
Nasikia yule wa Korea tayari unaliwa wali mwenye taarifa sahihi atujuze , dikteta akiondoka ni furaha kwa dunia
Mpaka saa moja ilopita alikuwa bado you hai. Ila ni mgonjwa sana kwa siku kadhaa. Hali ilizidi kuwa mbaya baada ya kufanyiwa operation. Leo pia kashindwa kujitokeza kwenye siku kuu ya kijeshi ambayo masilaha huonyeshwa kupitia gwaride.
 
Hakuna kitu kama ''ahadi ya siku ya kufa''. Huu ni msemo wa kizamani na umeshapitwa na wakati. Nchi zilizoendelea wananchi wake wanaishi maisha marefu kulinganisha na nchi zetu za dunia ya tatu. Kwa nini? Unataka kutuambia kuwa Mungu amefanya upendeleo na kuwapa watu nchi zilizoendelea ahadi ya maisha marefu na huku kwetu akatupa ahadi ya maisha mafupi? Ni watoto wangapi chini ya umri wa miaka mitano wanafariki nchi zinazoendelea kwa kukosa huduma muhimu za afya au lishe bora? Hawa watoto wadogo kabisa waliahidiwa maisha ya chini ya miaka mitano? Bila shaka msemo wako unapotosha na unafanya binadamu wawe wazembe kufuata kanuni bora za maisha wakidhani hawatakufa kama ahadi yao haijafika!
Mkuu tukianzisha arguments namna unayotaka tutakuwa tunaingia kwenye kukosoa imani sasa.

Kikubwa ni kuwa tunaamini kufa ni stage ya mwisho ya uhai wa binaadamu na dhana ya kuwa kila mtu atakufa kwa ahadi aliyoandikiwa na Mungu ni kupunguza nadharia juu ya kifo maana hakuna jibu sahihi juu ya ni kwann watu wanakufa so tunaounguza maswali lundo kuhusu kufa na kikubwa zaidi ni kujipa moyo kuwa kufa kupo ila kuhusu kwann huyu anakufa maoema na huyu anabaki hayo tumuachie Mungu pekee.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpaka saa moja ilopita alikuwa bado you hai. Ila ni mgonjwa sana kwa siku kadhaa. Hali ilizidi kuwa mbaya baada ya kufanyiwa operation. Leo pia kashindwa kujitokeza kwenye siku kuu ya kijeshi ambayo masilaha huonyeshwa kupitia gwaride.
North Korea nao ni sawa na maiti zinazotembea Kama waafrica utakuta nao eti wanahangaika kuokoa uhai wa mtu anayekuja kuwatesa hizo akili matope.Hapo ni sawa na polisi kuisaidia ccm
 
Swali lako halina maana yeyote kipindi hiki ambapo sirikali imeamua kufuata ushauri wa Mwigulu Nchemba. Kwanini usishangae toka majuzi kimyaaaa no New case, no death no recovery! Only in Tz can happen this!!
 
Back
Top Bottom