Tujiulize: Kwanini ghafla vifo vimekuwa vingi?

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,607
8,744
Mwezi huu tumeanza kusikia vifo vingi bila kuambiwa vimetoka wapi. Wiki hii moja tu kuna wazee baba wa rafiki na Mama wa rafiki wamefariki kwa mazingira kama ya Corona ya homa, kushidwa kupumua na kukohoa. Wato walikuwa na magojwa mwngine na miaka zaidi ya 68.

Uchunguzi uliofanywa kwenye state ya new york kwa kuchunguza watu 3000 ambao hawaumwi wamekuta 14% kwa jimbo zima na 20% kwa mji mkuu wa New york wameumwa na kupona bila kujua hivyo kuna mengi ambayo hatujui kuhusu huu ugojwa.

Ushauri wangu kwanza wafiche wazee wako kama wapo na waelimishe, pili serikali ipime watu zaidi kama inawezekana na tatu ni lazima wahauri watu wasiwnde sehemu ambazo si za lazima.

Yaani huu ugojwa unachochoe magojwa watu walionao wazidiwe hivyo wenye pumu utaambiwa ni pumu, wenye kisukari hivyo hivyo hatutajiua idadi lakini tukiona misiba gafla inakuwa mingi tujiulize kwanini sana
 
Mkuu vifo vimekushtua mpaka umekosa usingizi??Relax bro kila mtu atakufa kwa ahadi ya mola wake so km case ni Corona basi ndo itakuwa aina ya kifo alichopangiwa mja ndo maana unakuta kuna Corona kali lakini kuna wanaokufa kwenye ajali mbalimbali.

BTW tuchukue tahadhari zaidi kujilinda na maambukizi pengibe ss hatukuandikiwa tufe kwa Corona

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1587867932946.png



1587867872327.png
 
Woga na unafiki Ni kitu kibaya Sana...mwaka huu watu watajifunza kuwa kupiga kura Ni Ni suala linalohusu maisha ya na kizazi chote.Tanzannia huwa tunachukulia Siasa za Nchi Kama Ushabiki ea Simba na Yanga.
Hizi tetesi zonazoendelea kuhusu Hali ya ugonjwa wa Kakorona'' hapa nchini zinshitaji kuwekwa saws.Kama Ni uongo kwa faida faida ya Nani!
Na kwa Nini watu wazushe kuhusu vifo.
Kwa Nini taarifa kuhusu kujikinga zinatolewa kwa kukinzana.Ingekuwa nchi za wenye hofu ya MUNGU Naibu Wazir wa Afys na RC Dar wangeomba kupumzika
Vyombo vya habari vyote vimeshindwa kufanya uchunguzi wa tetesi zonazoendelea,wanalinda ugali wao.
Ukiangalia mwenendo wa Korona kwa nchi nyingi ...hakika Tanzania inahitaji Neema ya Mungu kuliko nchi hizo...Sasa Sina uhakika Kama Mungu yupo hivi!
 
Yaani huu ugojwa unachochoe magojwa watu walionao wazidiwe hivyo wenye pumu utaambiwa ni pumu, wenye kisukari hivyo hivyo hatutajiua idadi lakini tukiona misiba gafla inakuwa mingi tujiulize kwanini sana
Mkuu Kamundu, nakuomba please, tusitishane!. Tangu kuibuka kwa ugonjwa wa Corona, so far kwa Tanzania, kumetokea vifo 10 tuu ndio vya Corona, sasa hii habari ya vifo vingi, inatokea wapi?.

Kila lenye mwanzo lina mwisho, uhai upo umeumbwa na kifo pia kipo kimeumbwa, ile siku unazaliwa tayari kifo chako umeisha andikiwa, hivyo hata hao 10 waliokufa waliandikiwa, wakati huo huo vifo vingine vya magonjwa mengine vinaendelea daily na sio Corona!.

Kwa mujibu wa utoaji wa taarifa za Corona, taarifa zote rasmi zitatolewa na serikali pekee, hivyo hata akitokea mtu mwingine yoyote akafa kwa kuonyesha dalili zote za Corona, huyo atakuwa amekufa tuu kwa mengine na sio kwa Corona!.
Tanzania hakuna vifo vyovyote vya Corona zaidi ya vile 10!, sasa kwa idadi hiyo ukilinganisha na vifo vya Italy or US compared, kuna vifo vingi gani?. Mkuu Kamundu, Tusitishane jamani!.
P
 
Mkuu vifo vimekushtua mpaka umekosa usingizi??Relax bro kila mtu atakufa kwa ahadi ya mola wake so km case ni Corona basi ndo itakuwa aina ya kifo alichopangiwa mja ndo maana unakuta kuna Corona kali lakini kuna wanaokufa kwenye ajali mbalimbali.

BTW tuchukue tahadhari zaidi kujilinda na maambukizi pengibe ss hatukuandikiwa tufe kwa Corona

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna kitu kama ''ahadi ya siku ya kufa''. Huu ni msemo wa kizamani na umeshapitwa na wakati. Nchi zilizoendelea wananchi wake wanaishi maisha marefu kulinganisha na nchi zetu za dunia ya tatu. Kwa nini? Unataka kutuambia kuwa Mungu amefanya upendeleo na kuwapa watu nchi zilizoendelea ahadi ya maisha marefu na huku kwetu akatupa ahadi ya maisha mafupi? Ni watoto wangapi chini ya umri wa miaka mitano wanafariki nchi zinazoendelea kwa kukosa huduma muhimu za afya au lishe bora? Hawa watoto wadogo kabisa waliahidiwa maisha ya chini ya miaka mitano? Bila shaka msemo wako unapotosha na unafanya binadamu wawe wazembe kufuata kanuni bora za maisha wakidhani hawatakufa kama ahadi yao haijafika!
 
Back
Top Bottom