tujikumbushee????

beibe nasty

JF-Expert Member
Apr 11, 2012
1,640
523
wakati upo mtoto ulikua unapenda cheza mchezo upi na nikwanin? Mimi nilikua napenda saana rede coz nilikua straiker wao n nilikua najua, na pia kombolela coz nilikua napenda kujifichaficha weee haya wewe jeee.
 
Rede ya wote...

Reason: mnachanganyika ma-HE na ma-SHE

Mdako

reason: hamkimbizani,ni mzuri mkiwa mmechoka michezo mingine ya kutoa jasho..
 
Mie nilikuwa nacheza michezo mingi tu...kiasi kwamba hata sijui ni mchezo upi nilikuwa naupenda sana!
 
Rede ya wote...

Reason: mnachanganyika ma-HE na ma-SHE

Mdako

reason: hamkimbizani,ni mzuri mkiwa mmechoka michezo mingine ya kutoa jasho..
Gamba umenigusa rede ya wote hehe kama hautaki sambaa nenda kauze ugali na dagaa hahaaaaa na mdako nilikua nachezahad na mkono wa kushoto
 
aah nilikuwa napendaga kucheza kinyumba nyumba af mi nilikuwa mtoto cause nina kaumbo kadogo baba na mama sasa mmhhh!
 
Gamba umenigusa rede ya wote hehe kama hautaki sambaa nenda kauze ugali na dagaa hahaaaaa na mdako nilikua nachezahad na mkono wa kushoto

Jina langu refu sana.. Hivyo watu wanatumia "nick name" yangu,ya Gee Cee..

Bora uweze kushoto,kwani kujifunza kulia ni rahisi.. Niliwahi kufungwa P.O.P. ikawa tabu kwenye mdako..
Nikahamia kwa wanaume ambako nilijifunza danadana..
 
gololi.. Enzi za madungu, macho ya paka, kipusa n.k. Ukiwa na dungu inabidi umtafute mwenye dungu mwenzako ndo mcheze naye. Ukiwa na kipusa au macho ya paka kila mtu atataka kucheza na wewe kwa matarajio ya kukula vigololi vyako..!
 
Dah.. Nilikuwa na shabaha,kwa mitaa ya kwetu ya kishua..

Wakaja watoto wa uswazi,ah.. Walitishajeh! Wana shabaha hamna mfano wake!
 
Jina langu refu sana.. Hivyo watu wanatumia "nick name" yangu,ya Gee Cee..

Bora uweze kushoto,kwani kujifunza kulia ni rahisi.. Niliwahi kufungwa P.O.P. ikawa tabu kwenye mdako..
Nikahamia kwa wanaume ambako nilijifunza danadana..
Gee cee wooow dats preety name any way hapo umetishaaa nimechezesha vichupa saaana
 
Back
Top Bottom