Tujikumbushe

Ratili moja pesa moja!!!.......Mayai ya Ratili moja pesa moja,dhahabu ya Ratili moja pesa moja hahahah!!!!!!!....Mfalme juha ilikuwa Raha tupu!!
mkuu pale ukianza kusoma ukiwaza sana utaona mwandishi katumia mandhari ya ajabu sana,eti pazia ilifungulia halafu wakaingia kwenye nchi inayoitwa kichaa
 
nakikumbuka sana aise
Sijui hiki kitabu kinapatikana wapi
Mwenye nacho please aniambie kiko wapi
Nkuu hata mi navitafuta ila vingi vinauzwa online,ila sikushauri kuvinunua online kwa ajili ya utapeli
 
Hiki kitabu nilikipenda sana,
Na nikazidi kukupenda baada ya kuja chuo na kufanya option course ya mwandishi wake E. Semzaba,nikaamua kukisoma tena hakika nikazidi kukipenda!
Cantalisia unakumbuka binti mazoea?
 
Last edited by a moderator:
Nkuu hata mi navitafuta ila vingi vinauzwa online,ila sikushauri kuvinunua online kwa ajili ya utapeli

Mkuu hivyo vya online hapana mkuu
na vingi washavifanyia editing wameondoa ule uhalisia wake
Ila hata ukikipata tuu ni bora sana mkuu
Nikuombe aise unitumie list yote kwenye pm mkuu nitashukuru aise
 
Aisee hiki kitabu sitakaa nikisahau maishani mwangu.
Young_Master huyu jamaa kwa hiki kitabu nimemkubali,jamaa alikuwa na idea ya ajabu na huwezi kumfananisha na mwandishi yeyote.

Kuna zile hadithi za kina Willy Gamba sijui ni kitabu gani ...
Ebwana Excellent umenikumbusha mbali sana nikirudi hm lazima nivitafute kadri niwezavyo nivisome upya .
]
MWAKALINGA hizi kazi za fasihi siku hizi waandishi hawaandiki vizuri kama zamani,wanaangalia pesa tu
 
Last edited by a moderator:
Mkuu hivyo vya online hapana mkuu
na vingi washavifanyia editing wameondoa ule uhalisia wake
Ila hata ukikipata tuu ni bora sana mkuu
Nikuombe aise unitumie list yote kwenye pm mkuu nitashukuru aise
Poa nitakutumia
 
Kumbe wazee tupo wengi humu, halafu huwa mnajidai kama vi teenager mkiwa MMU.
 

Source: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...e-alfulela-ulela-uza-ghali-usiuze-rahisi.html
 
Nakitafuta kitabu kilichokuwa na story ya WAGAGAGIGIGOKO sikikumbuki jina lakini kilikuwa kinasisimua sana.....by the way ule moyo wa kusoma vitabu kama hivi sijui nimeuweka wapi (nitautafuta) au vitabu vya kileo hovyo?

Halafu kuna alfu lela ulela - siku elfu na?..................... Kaka zangu walipokuwa wakikisoma/na kutuhadithia usiku nilikuwa sipati usingizi, ni hofu tupu.............

Halafu kuna cha darasa la tatu kiswahili kilikuwa na story ya sungura na sizitaki mbichi hizi...siukumbuki ule ushairi vizuri

.......sungura mimi maskini uvivu wangu nyumbani.................
 
X-paster alituletea kipande hiki kitamu:

 


platozoom Mkuu siku hizi hakuna vitabu vya maana,waandishi wanaangalia hela kuliko kuwaangalia wasomaji,hawajui wanapoandika ndo hadhira inafurahia kazi zao...siku hizi jina la kitabu kizuri ila maudhui hamna lolote
 
Last edited by a moderator:
Last edited by a moderator:
Ribosome hivi hakuna hadhithi ndefu kama hizi za kusoma online?yaani huwa zinafurahisha sana

Kuna moja nzuri sana niliipata online, inaitwa "Tata za Asumini", ukii google utaipata, hizi zingine inabidi x-paster aje kutupa ujanja.

Alf leyla u leyla ipo ya Kiingereza, One thousand and one nights na Umsolopagas ipo ya Kiingereza, nimesahau jina lakini niliwahi kuzisoma, nikipata link ntakuwekea.
 
Kuna moja nzuri sana niliipata online, inaitwa "Tata za Asumini", ukii google utaipata, hizi zingine inabidi x-paster aje kutupa ujanja.
Ribosome thanks ebu ngoja nitafute kwanza hiyo ya Tata za Asumin
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…