mtwa mkulu
JF-Expert Member
- Sep 11, 2013
- 8,098
- 9,999
Mwaka 2018 Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) lilitoa waraka wa Pasaka ambao ulikua unakosoa, kuonya na kushauri mambo mbalimbali yaliyokua yakiliathiri taifa kwa wakati huo. Waraka huo ulikua moto kwa serikali ya Magufuli kwa sababu ulikosoa mambo mbalimbali ikiwemo matumizi ya nguvu kufunga biashara pamoja na vitendo vya watu kutekwa, kupotea na miili ya watu kuokotwa baharini kwenye mifuko ya sandarusi.
Kanisa liliitaka serikali ichukue hatua kukomesha vitendo hivyo na kuagiza waraka huo usomwe katika Dayosisi zote nchini. Kati ya Maaskofu 27 wa KKKT, Maaskofu 24 walitii na kuusoma waraka huo kwenye Dayosisi zao, lakini Maaskofu watatu walizuia usisomwe. Maaskofu hao ni Solomon Massangwa wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati (Arusha), Askofu Lucas Judah Mbedule wa Dayosisi ya Kusini Mashariki (Mtwara) na Askofu Alex Malasusa wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani.
Kufuatia Maaskofu hao watatu kwenda kinyume na agizo la Kanisa, waliagizwa kuomba radhi na Halmashauri kuu ya Kanisa. Askofu Lucas Judah Mbedule wa Dayosisi ya Kusini Mashariki aliomba radhi kwa kulala kifudifudi akiwa kwenye vazi lake rasmi la Uaskofu, kama ishara ya unyenyekevu.
Askofu Massangwa wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati (Arusha) aliomba radhi kwa maandishi, na taarifa yake ya kuomba msamaha ilichapwa kwenye gazeti la Mtanzania la April 30, mwaka 2018.
Askofu Malasusa hakuomba radhi na hivyo, kikao cha Baraza la Maaskofu wa KKKT kikalazimika kuketi April 29 mwaka 2018 ili kujadili suala lake. Kikao hicho kiliazimia kumtenga Askofu Malasusa na kumzuia kuwakilisha Kanisa hilo nje ya Dayosisi yake kama hataomba radhi. Baada ya shinikizo hilo Askofu Malasusa alilazimika kuomba radhi kwa maandishi.
Askofu mbedule aliomba radhi kwa kuanguka kifudi fudi kwa unyenyekevu mkubwa
Pia soma
- Baada ya Malasusa kutengwa, askofu KKKT aomba radhi waraka kutosomwa kanisani
- Baadhi ya waumini wa KKKT wataka Askofu Malasusa aombe radhi na Kustaafu