ah bougwan,salamu mkuu!kweli umechoka kuwinda sana? kisha,asungoje kujibiwa akasema"sikiliza bougwan nitakusimulia hadithi,ni khabari za mwanamke nawe kwa hiyo utasikiliza sivyo?palikuwa na mtu na ndugu yake mwanaume,ikawa mwanamke anampenda sana yule ndugu,na yule ndugu anampenda sana yule mwanamke.Lakini yule ndugu alikuwa alikuwa na mke mwingine mpenzi wake.wala hakumpenda yule mwanamke akamfanyia dhihaka.basi yule mwanamke kwa kuwa alikuwa mwerevu na mwenye moyo wa kutaka kisasi akafikiri moyoni akamwambia yule mwanaume,nakupenda na ukifanya vita na ndugu yako nitakusaidia,na yule mtu alijua ni uwongo lakini kwa kuwa alimpenda sana yule mwanamke akayasikiliza maneno yake akafanya vita na ndugu yake.Na baada ya kuuawa watu wengi ndugu yake akamtumia habari kumuuliza"mbona wataka kuniua?tokea utoto wangu nilikupenda.Nimekudhuru namna gani?ulipokuwa katika dhiki aikukuokoa? nasi tulienda pamoja kufanya vita,tukagawana mateka,mwanamke kwa mwanamke,ng'ombe kwa ng' ombe? basi mbona wataka kuniua ndugu yangu kipenzi? basi moyo wa yule mtu ulikuwa mzito akajua kuwa matendo yake ni maovu,akamuepuka yule mwanamke na kukomesha vita,akakaa katika nyumba moja na ndugu yake.muda ukapita yule mwanamke akamuijia na kusema" na tuyasahau yaliopita nitakuwa mke wako.Na katika moyo wake alijua kuwa anasema uongo lakini kwa kuwa alimpenda sana akamuoa.basi usiku alipoona yule mtu kalala,yule mwanamke akatwaa shoka katika mikono ya mumewe akaenda kumwua pale pale usingizini.kisha kama simba aliekwisha kula shibe yake,akaweka kitanzi cha kipini cha shoka lile lenye damu ktk kiwiko cha mkono wa mumewe aliekuwa usingizini,akatoka na kwenda zake.Kulipopambazuka,watu wakaja wakipiga kelele' lousta ameuawa usiku,wakaja nyumbani mwa yule mtu wakamkuta bado amelala,na karibu nae lipo lile shoka lenye damu limelala.Ndipo walipovikumbuka ville vita, wakasema'tazam! hakika amemuua ndugu yake,wakataka kumwua,lakinj aliondoka upesi akakimbia na alipokuwa akikimbia akamwua yule mwanamke.Lakini mauti haikuweza kutafuta maovu aliyoyafanya yule mwanamke, na uzito wa dhambi yake ulimkalia yule mwanaume.hivyo ametupwa na watu wake,na jina lake ni twezo katikati ya watu wake,maana mzigo wa dhambi aliyoitenda yule mwanamke umetwikwa juu yake.basi yule aliekuwa mkuu hutembeatembea mbali na kwao,hana nyumba wala mke na hivyo atakufa kama mnyama aliepigwa,na jina lake litalaaniwa toka vazazi hata vizazi, kwa kuwa husemwa alimwua ndugu yake lousta kwa hila wakati wa usiku.basi yule mzulu akanyamaza nikaona jinsi hadithj yake inavyomuhuzunisha.akasema" mimi ndio huyo mtu bougwan na wewe nisikilize,kama mimi nilivyo ndivyo na wewe utakavyokuwa,chombo kitu cha kuchezea ng'ombe achukuaye mzigo wa maovu wa mtu mwingine.Sikiliza ulipomnyemelea bibi wa usiku mimj nilikufuatia,alipokupiga kisu ktk chumba cha malkia nyleptha mimi nilikuwamo pia, ulipomuacha aende zake kama nyoka ktk miamba, mimi nilikuona nikajua kuwa amekuloga na kuwa mtu mwaminifu ametoka ktk uaminifu wake na yeye aliependa njia iliyo nyooka amechagua njia iliyopotoka.Nisamehe baba yangu kama maneno yangu ni makali lakinj yanatoka ktk moyo uliojaa.Usionane nae tena na hivyo utashuka ktk kaburi lako kwa heshima.Ama sivyo utakuwa kama mimi nilivyo kwa ajili ya uzuri wa mwanamke unaochakaa kama vazi likiisha valiwa.Nimesemaaa.