Tujikumbushe vitabu vya zamani

Paulo mchafu.
Manenge na Mandawa.
Karudi baba mmoja.
Katiba ya ccm/ somo la siasa.
MY TAKE:sred kama hii iliwahi kutokea humu. Wasubiri wazee wa kuzodoa.
 
Zaidi ya hadithi nakumbuka unapoandika barua kwenda kwa mjomba, mkifunga shule uende. cku 1 kabla ya safar haulalii!
 
Chopeko na mnofu, Sadiki na Sikiri(Chitemo), Jogoo na Pazi, Hawafu mwenye nguvu, Juma na Uledi, Tegeki na Nembo, Moyo na Ndevu, Kibo na Mawenzi, Ali Mtoto Mtundu, Siku ya gulio Katerero, Kuku na Kanga, Mbwa na Paka, Sungura na Fisi(Chawote), Mfalme ana masikio marefu kama ya Punda, Kijiji cha Ujamaa, Mua uliozamisha meli n.k
 
Mkuu inaonekana ulikua unashika namba moja darasani! Yani umenikumbusha Vihadithi vingi kweli.. Asante sana.
 
Nani anakumbuka kijitabu kimoja kilikua kinasema Mgeni siku ya KWANZA mpe sijui wali na nyama, Mgeni siku ya PILI sijui nini nini... Nakumbuka tu Mgeni siku ya SABA mpe JEMBE akalime! Loh!
 
Nani anakumbuka kijitabu kimoja kilikua kinasema Mgeni siku ya KWANZA mpe sijui wali na nyama, Mgeni siku ya PILI sijui nini nini... Nakumbuka tu Mgeni siku ya SABA mpe JEMBE akalime! Loh!

"Mgeni siku ya kwanza mpe mchele na panza, mtilie kifuuni mkaribishe mgeni".
"Mgeni siku ya pili mpe maziwa na samli, mali yakikuzidia mzidishie mgeni".
"Mgeni siku ya tatu nyumbani hamkuna kitu, kuna vibaba vitatu pika ule na mgeni".
"Mgeni siku ya nne mpe jembe akalime akirudi muagane, msindikize mgeni".
"Mgeni siku ya kumi kwa mateke na mangumi, mfukuze mgeni".

Halafu hadithi ya Bulicheka na mkewe Eliza, walipokwenda kwa "Wagagagigigogo" long time ago.
 
Back
Top Bottom