Tujikumbushe vitabu vya zamani

alfu lela ulela elfu mia na moja
amina anakula wali kwa sindano
man umenirudisha,bali sana

Hasa pale Amina alipomgeuza mumewe Mbwa baada ya kumfuatilia kwenye karamu ya wachawi wakila nyama za watu- Ilikuwa inatisha Alfu lela ulela- Bwana akubariki kwa kunikumbusha Amina
 
mfalme juha..... na wagagagigikoko....
Kwenye kitabu cha Mfalme Juha (Farouk M. Topan), hakuna simulizi ya wagagagigikoko, wagagagigi koko ni masimulizi ya kwenye kitabu kinacho itwa Someni Kwa Furaha a.k.a Someni Bila Shida. Na ni katika zile safari za Bulicheka, ambaye aliandamana na mkewe Lizabethi.
 
Da! kaka umesababisha nimekumbuka mbaali sana.
Kumbe sio mambo ya dini tu bali hata huku upo deep sana.
Chukua senx hiyo.
 
sikumaanisha kuwa wagagagigikoko wako kwa mfalme juha.. nilikuwa nimemaanisha vitabu viwili tofauti..
 
Sio siri wapenzi kukumbushana ya mbali kuna raha zake. navitafuta sana hivyo vitabu kama unyoya wa kipanga azizi, maua ya malan (sijui kama natamka sahihi) Tuanze lini, pia nakumbuka hadithi kama nimeua saba kwa mpigo; pinokyo; mfalme juha, alflela ulela; safari ya bahari nyeusi, waridi;n.k. ooh kweli enzi hizo zilikuwa na raha yake hata watoto walikuwa na nidhamu.
 
Da! kaka umesababisha nimekumbuka mbaali sana.
Kumbe sio mambo ya dini tu bali hata huku upo deep sana.
Chukua senx hiyo.
Kwa bahati nilianza kujisomea vijitabu, kabla sijaanza chekechea... na nilipikuwa shule ya msingi nilikabidhiwa madaraka ya kutunza library ya shule, hapo sasa ndipo vitabu vilinikoma. (Karibia ya robo ya vitabu vya hadith viliamia nyumbani).
 
hata sielewi vimeedna wapi ivi vitabu
how i wish nivipate tena!!

sasa ivi sijui watoto wanasoma madude gani yalabi
 
sikumaanisha kuwa wagagagigikoko wako kwa mfalme juha.. nilikuwa nimemaanisha vitabu viwili tofauti..
Sawa mkuu, yote ni katika kunogesha mjadala, wakati mwingi huwa tunaelewa sivyo na mwandishi alivyo kusudia.

samahanimkuu kwa kuto kukuelewa.
 
Kisiwa Chenye Hazina, Robinson Crusoe, Jamaa Hodari Kisiwani, Hadithi ya Kisonoko (Cinderela).
 
Kisiwa Chenye Hazina, Robinson Crusoe, Jamaa Hodari Kisiwani, Hadithi ya Kisonoko (Cinderela).

mkuu hicho kitabu ninacho, niliikiiba library ya magamba sekondari. nilikuwa na tabia mbaya sana ya kuiba vitabu,
 
safari za gulva (sijui kama nipo sahihi na jina) yule jamaa dr. wa kwenye meli alienda nchi yenye vijitu vifupi vya saiz ya nchi 6 tu, halafu badae akakutana na kisa kingine cha kwenda kwenye nchi yenye mijitu mirefu km minazi.

vingine ni kama TAFRIJA YA DAMU, SIMU YA KIFO, MPENZI JUZUU YA 1 na 2,
 
duh...hivi vitabu bwana usipime....wakati huo kipindi cha mama na mwana kilikuwa kinasimulia hadithi zake zikirushwa na RTD, mida ya saa nane, nakumbuka hadhithi chache kama ua jekundu, binti chura, akajasembamba, kina bibi aga, na kuna kitabu kingine kilikuwa kinaitwa 'adili na nduguze' mambo ya mji wa mawe n.k.....kweli watoto wa siku hizi hawafaidi kabisa

Kipindi kile, enzi za utoto wetu tukisoma: Robinson Crusoe, Kisiwa cha Hazina (Treasure Island - by Robert Louis Stevenson), Unyonge wa Mwafrika - umo utawakuta Kaombwe na makapu ya karanga, pia kitabu kimoja jina nimesahau, lakini nakumbuka the main character in Sindbad wa Baghadad. Mzee wangu akipenda kusoma gazeti kubwa sana la Mzalendo na Africa Now. LOL, Old is Gold!
 
Ni wazi mkuu kuwa wakati Someni.jpg ule wa utoto wetu tulibahatika kusoma vitabu hivi: SOMENI KWA FURAHA (ktk series mbali mbali), na baadae SOMENI KWA FURAHA ikawa : SOMENI BILA SHIDA. Ni vitabu vyenye hadithi, visa na mikasa ya kusisimua sana! Mtunzi wa vitabu hivi, mzungu akiitwa Padre Alfons Loogman (RIP - 2011); akitumia uzoefu wake wa kukaa muda mrefu hapa East Africa kwa takribani miaka 37, alikuwa na uwezo mkubwa wa kusoma saikolojia ya watoto ndiyo maana vitabu vyake vilipendwa sana na watoto enzi zile.

Ninamkumbuka Makari Hodari, Pauli Mchafu, Bulicheka na wife wake Lizabeta, King Huihui, Kalumekenge, Wagagagigikoko, bibi Tarbushi n.k.
Nakumbika Mfalme Huihui alivyojaa mapovu siku moja baada ya Bulicheka kujenga nyumba bila ruhusa ya mfalme, akitumia meza ya pembe nne ambayo iligeuzwa upside down na kufungwa ktk minazi minne pwani ya bahari.
 
safari za gulva (sijui kama nipo sahihi na jina) yule jamaa dr. wa kwenye meli alienda nchi yenye vijitu vifupi vya saiz ya nchi 6 tu, halafu badae akakutana na kisa kingine cha kwenda kwenye nchi yenye mijitu mirefu km minazi.

vingine ni kama TAFRIJA YA DAMU, SIMU YA KIFO, MPENZI JUZUU YA 1 na 2,

Yeah Gulliver's Travels by Jonathan Swift - nakumbuka yale majina magumu ya miji aliyotembelea huyu Lemuel Gulliver kama: Lilliput, Brobdingnag, Luggnagg, Balnibarbi nk. Umenikumbusha mbali mkuu!
 
Nakumbuka vitabu vya zamani vya Hesabu: 'HESABU ZA KIKWETU'. Ktk vitabu vile ilikuwa nadra kukuta Metric System! Sana sana utakutana na vipimo kama: wakia, ounce, ratili, pound, mile, foot, inchi n.k. Hiki kizazi cha Lulu hakijaona mambo haya.
 
mkuu patience96 unanikumbusha mbali sana, asaiv watoto ni video tu, ndo maana hawajisumbui kujisomea.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu unakumbuka vitabu vya zamani, English Oxford, walikuwepo akina : Abdul, Mr. Mutabingwa, Kokogonza n.k. Unavikumbuka?
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom