Majanga Hanang majibu ya kebehi ya wataalam TANESCO kuhusu suala la umeme

Steven Joel Ntamusano

JF-Expert Member
Jun 17, 2023
2,948
1,988
Mungu hamfichi mnafiki.Msemo maarufu wenye miaka mingi. Wataalam wa shirika la ugavi wa umeme TANESCO wamejibiwa na Mungu mwenyewe pale walipojibu shutuma kwanini umeme haupatikani huku mvua zikinyesha. Wakasikika wakisema zinanyesha katika mikoa mingine mbali kabisa na kule Mtera ambapo kuna mitambo ya kuzalisha umeme kwa njia ya maji.

Haikupita hata wiki moja mvua kubwa ikanyesha kule Hanang na kuleta uharibifu mkubwa pamoja na kuondoka na uhai wa watanzania wenzetu kadhaa. Yale ni majibu kutoka kwa Mungu asiyeonekana kwenda kwa wataalam wetu wanaolewa ile jeuri ya usomi na utaalam wao wakisahau kuwa kauli huwa inaumba.

TANESCO kuiamini kuwa ni suluhisho la tatizo la umeme katika Tanzania hii ambayo ina serikali yenye utayari wa kubinafsisha bandari ili iendeshwe kisasa, kwa kweli ni kujidanganya. Umefika muda wa kuwa na wazalishaji wengi wa umeme wanaoipa changamoto TANESCO. Pia mlaji wa mwisho anakuwa na chaguo la wapi apate huduma kulingana na pato lake na mahitaji yake.

Wapo wengi ambao hawajaelewa ni kwanini TPA anapelekewa ushindani wa DP World, huwezi kuwalaumu ni akili zile zile za kijamaa kwa maana ya mawazo ya serikali kuu kuhodhi utendaji wa mamlaka zenye kugusa umma moja kwa moja.

TANESCO kuhodhi utoaji huduma za usambazaji wa umeme ni uendelezaji wa ukiritimba ule ule ambao umejaa mianya ya wizi na ufisadi mwingi wa kimya kimya. Wanajua hata wakiharibu na kuwapa hasara wafanyabiashara wengi wenye mitaji midogo bado ipo serikali kuu itakayotetea uozo huo.

Huu ni muda wa kumpa ushindani TANESCO kwa kuruhusu makampuni mengine kufanya shughuli ya kuzalisha nishati hii muhimu sawa sawa na kule bandarini ambapo DPW na mwendeshaji mwingine anayetafutwa wanakwenda kumchangamsha TPA.
 
Back
Top Bottom