TUJIKUMBUSHE: Kifo cha Rais wa Malawi wahaini sita usiku wa manane" The Midnight Six" na Njama za kutaka kumpora Urithi wa Urais Joyce Banda

kwa mazingira ya kwetu ya kutangaza kifo cha mh mama kawaacha mbali wengi sana, maana ukiangalia vizuri tangazo kalitoa bila wakuu wa vyombo na ulinzi na usalama kuwepo, na pia amelitoleo nje ya mjii mkuu dodoma/dar
Una hisi kuna link?
 
Habari za leo ndugu wasomaji wa JamiiForums.

Kisa hiki cha Rais wa Malawi Pres Bingu wa Mutharika na Makau wake Joyce Banda chaweza kuwa na funzo namna taasisi za nchini humo zilivyokuwa na maadili kwa maslahi ya wana Malawi.

Twende pamoja.

Ni usiku wa kuamkia tare 5 aprili 2012, Rais Bingu wa mutharika akiwa na kikao cha siri akiwa na wabunge wawili Mh Patricia na Mh Agnes ndipo Rais Mutharika alipata shambulio la Moyo (Heart attack) na kupelekwa hospitali ya jirani akagundulika kuwa ameshapoteza uhai.

Hata hivyo serikali ya Malawi ikishirikiana pamoja na Daktari wa Rais hawakutaka kutangaza kifo cha Mutharika ili kutoa mwanya wa kugeuza mambo kinyume cha Katiba.

Ikumbukwe kwa Muda Mrefu Rais Mutharika alikuwa amemwandaa Mdogo wake Peter Mutharika kuja kuwa mrithi wake wa urais hapo baadaye. Ndipo makuwadi na wapiga makofi wa Chama cha DPP cha Rais walipata fursa ya kugeuza mambo watakavyo.

Mwili wa Mh Rais Bingu wa Mutharika ulilazimika kubebwa ukiwa na mipira mdomoni na puani ili kuhadaa umma na wananchi kuwa Rais bado yuko hai ispokuwa yuko mahututi. Ulikimbizwa Nchini Afrika kusini.

Huku akiwa kaka yake amefariki na uvumi nchi nzima na nje ya nchi kupitia mitandao ya kijamii redio na tv Peter Mutharika hakusindikiza (kaka yake mgonjwa) akabaki nchini na mbinu za kupindua katiba ili Joyce Banda asiapishwe kuwa Rais.

TAR 6 APRILI
Mwili wa marehemu ukiwa nchini Afrika Kusini huku viongozi waandamizi wakisambaza taarifa kuwa Rais huyo hali yake ni mbaya sana na yuko mahututi.

Peter Mutharika alimwita haraka sana Mkuu wa Majeshi General Henry Odillo, lengo la wito huo ni kumuomba Kachero huyo asaidie namna ya kuhamisha madaraka na kumruka Joyce Banda. CDF huyo alitupilia mbali ombi haramu la Peter Mutharika na kumwambia kuwa siwezi kufanya hivyo na ni muhimu katiba ya nchi iheshimiwe "the constitution must be respected". Hapo Peter wa Mutharika aligonga mwamba na hakutarajia kama ingekuwa hivyo. Bado hakuridhika akatafuta ushauri haraka ndani ya masaa machache kutoka kwa Mwanasheria mkuu wa Serikali ambaye naye alimweleza bayana kuwa jambo hilo haliwezekani.

Peter mutharika alitamani muda ule CDF atangaze kuwa serikali ya malawi iko mikononi mwa Jeshi huku akijipanga namna ya kupata nafasi ya umakamu wa Rais na hatimaye aapishwe yeye kulinda maslahi ya kaka yake na MATAGA wa malawi.

TAREHE 7 APRILI 2012
Ikiwa ni usiku wa manane huku maharamia wa kidemokrasia nchini Malawi wakiwa hawajui la kufanya na muda ukizidi kuyoyoma na uvumi ukiwa unazidishamiri kila mtaa yakuwa Rais kafariki waliitisha kikao cha kupindua Umakamu wa Joyce Banda na wakakaa usiku ule bila Joyce banda kushirikishwa.

Walioshirikia walioonekana kwenye tv usiku wa manane (The Midnight Six) ni pamoja na

1. Peter Mutharika - Waziri wa Mambo ya nje wakati huo na mdogo wake Marehemu Bingu wa Mutharika

2. Patricia Kaliati- Waziri wa Habari na Elimu ya Uraia (huyu ndiye alikuwa na Raia kikao vha siri siku ya kifo chake)

3. Henry Mussa - Waziri wa serikali na mamlaka za mitaa

4. Dr Jean Kalilani - Waziri wa Afya

5. Simon Vuwa Kaunda - waziri wa michezo

6. Nicholas Dausi - Naibu waziri Ofisi ya Rais

Ikiwa giza nene linazidi kusonga huku kunakaribia kucha usiku wa kuamkia tar 7, zilisikika habari za kiintelijensia zilizomfikia Rais wa A. Kusini Jacob Zuma kuwa kuna mkakati wa hovyo na ovu unaoratibiwa na baadhi ya wanachama wa baraza la mawaziri wanataka kumpora Joyce Banda haki ya kuapishwa kupitia mbinu za kuchelewesha kutangaza kifo cha raia kupisha mwanya wao kujipanga.

Ndipo Jacob Zuma akalipua taarifa kuwa endapo ikifika mchana wa tar 7 serikali ya Malawi haitatangaza kifo cha Bingu basi yeye atachukua jukumu la Kutangaza na kuusafirisha mwili (repatriation) wa Bingu nchini Malawi.

The midnight six wakaona saaa mpango umeshakwama wakakubali yaishe na wakatangaza kuwa Rais amefariki hapo hapo wakamwapisha Joyce Banda kuwa rais.

Nini kilitokea hapo baadae.

The midnight Six wote walishtakiwa ka kosa la uhaini na kufungwa Jela.

Nini umejifunza kutokana na kisa hiki?
The midnight six ndo akina Sukuma Gang wa nchi moja hivi.

Naona kabisa kuna ufanano kati ya Joyce Banda na Bi Vasco kwa maana katika njia ya kuingia madarakani lakini pia ufanano katika njia ya kutoka madarakani.
 
Unasikiliza sana ngonjera za Chahali, mtu ambae aelewi hata serikali inavyoondeshwa.

Diwani Athumani hana nguvu hizo ndani ya Tanzania.

Katibu mkuu Kiongozi (Dr Bashiru) ndio mkuu wa taasisi na Idara zote za serikali, huyo ndio king maker ikitokea miujiza raisi katutoka.
Usalama wa taifa ndo kila kitu bro
 
The midnight six ndo akina Sukuma Gang wa nchi moja hivi.

Naona kabisa kuna ufanano kati ya Joyce Banda na Bi Vasco kwa maana katika njia ya kuingia madarakani lakini pia ufanano katika njia ya kutoka madarakani.
hahaa Bi Vasco Da Gamma
 
Vp na uyu bibie atakuja kutoka madarakani kama Joyce Banda manaa naye aliangukia pua pakubwa sana baada ya uchaguzi
 
Vp na uyu bibie atakuja kutoka madarakani kama Joyce Banda manaa naye aliangukia pua pakubwa sana baada ya uchaguzi
Kama hana Leadership Traits Kwa katiba na Katiba inatoa uhuru na haki basi anaweza kutoka.
 
The midnight six ndo akina Sukuma Gang wa nchi moja hivi.

Naona kabisa kuna ufanano kati ya Joyce Banda na Bi Vasco kwa maana katika njia ya kuingia madarakani lakini pia ufanano katika njia ya kutoka madarakani.
Ooh kumbe
 
Vp na uyu bibie atakuja kutoka madarakani kama Joyce Banda manaa naye aliangukia pua pakubwa sana baada ya uchaguzi
Kwa katiba Ipi? Huko Malawi iliwezekana kwa kuwa katiba yao ilikuqa relatively independent
 
Back
Top Bottom