TUJIKUMBUSHE: Kifo cha Rais wa Malawi wahaini sita usiku wa manane" The Midnight Six" na Njama za kutaka kumpora Urithi wa Urais Joyce Banda

Pythagoras

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
17,313
2,000
Habari za leo ndugu wasomaji wa JamiiForums.

Kisa hiki cha Rais wa Malawi Pres Bingu wa Mutharika na Makau wake Joyce Banda chaweza kuwa na funzo namna taasisi za nchini humo zilivyokuwa na maadili kwa maslahi ya wana Malawi.

Twende pamoja.

Ni usiku wa kuamkia tare 5 aprili 2012, Rais Bingu wa mutharika akiwa na kikao cha siri akiwa na wabunge wawili Mh Patricia na Mh Agnes ndipo Rais Mutharika alipata shambulio la Moyo (Heart attack) na kupelekwa hospitali ya jirani akagundulika kuwa ameshapoteza uhai.

Hata hivyo serikali ya Malawi ikishirikiana pamoja na Daktari wa Rais hawakutaka kutangaza kifo cha Mutharika ili kutoa mwanya wa kugeuza mambo kinyume cha Katiba.

Ikumbukwe kwa Muda Mrefu Rais Mutharika alikuwa amemwandaa Mdogo wake Peter Mutharika kuja kuwa mrithi wake wa urais hapo baadaye. Ndipo makuwadi na wapiga makofi wa Chama cha DPP cha Rais walipata fursa ya kugeuza mambo watakavyo.

Mwili wa Mh Rais Bingu wa Mutharika ulilazimika kubebwa ukiwa na mipira mdomoni na puani ili kuhadaa umma na wananchi kuwa Rais bado yuko hai ispokuwa yuko mahututi. Ulikimbizwa Nchini Afrika kusini.

Huku akiwa kaka yake amefariki na uvumi nchi nzima na nje ya nchi kupitia mitandao ya kijamii redio na tv Peter Mutharika hakusindikiza (kaka yake mgonjwa) akabaki nchini na mbinu za kupindua katiba ili Joyce Banda asiapishwe kuwa Rais.

TAR 6 APRILI

Mwili wa marehemu ukiwa nchini Afrika Kusini huku viongozi waandamizi wakisambaza taarifa kuwa Rais huyo hali yake ni mbaya sana na yuko mahututi.

Peter Mutharika alimwita haraka sana Mkuu wa Majeshi General Henry Odillo, lengo la wito huo ni kumuomba Kachero huyo asaidie namna ya kuhamisha madaraka na kumruka Joyce Banda. CDF huyo alitupilia mbali ombi haramu la Peter Mutharika na kumwambia kuwa siwezi kufanya hivyo na ni muhimu katiba ya nchi iheshimiwe "the constitution must be respected". Hapo Peter wa Mutharika aligonga mwamba na hakutarajia kama ingekuwa hivyo. Bado hakuridhika akatafuta ushauri haraka ndani ya masaa machache kutoka kwa Mwanasheria mkuu wa Serikali ambaye naye alimweleza bayana kuwa jambo hilo haliwezekani.

Peter mutharika alitamani muda ule CDF atangaze kuwa serikali ya malawi iko mikononi mwa Jeshi huku akijipanga namna ya kupata nafasi ya umakamu wa Rais na hatimaye aapishwe yeye kulinda maslahi ya kaka yake na MATAGA wa malawi.

TAREHE 7 APRILI 2012

Ikiwa ni usiku wa manane huku maharamia wa kidemokrasia nchini Malawi wakiwa hawajui la kufanya na muda ukizidi kuyoyoma na uvumi ukiwa unazidishamiri kila mtaa yakuwa Rais kafariki waliitisha kikao cha kupindua Umakamu wa Joyce Banda na wakakaa usiku ule bila Joyce banda kushirikishwa.

Walioshirikia walioonekana kwenye tv usiku wa manane (The Midnight Six) ni pamoja na

1. Peter Mutharika - Waziri wa Mambo ya nje wakati huo na mdogo wake Marehemu Bingu wa Mutharika

2. Patricia Kaliati- Waziri wa Habari na Elimu ya Uraia (huyu ndiye alikuwa na Raia kikao vha siri siku ya kifo chake)

3. Henry Mussa - Waziri wa serikali na mamlaka za mitaa

4. Dr Jean Kalilani - Waziri wa Afya

5. Simon Vuwa Kaunda - waziri wa michezo

6. Nicholas Dausi - Naibu waziri Ofisi ya Rais

Ikiwa giza nene linazidi kusonga huku kunakaribia kucha usiku wa kuamkia tar 7, zilisikika habari za kiintelijensia zilizomfikia Rais wa A. Kusini Jacob Zuma kuwa kuna mkakati wa hovyo na ovu unaoratibiwa na baadhi ya wanachama wa baraza la mawaziri wanataka kumpora Joyce Banda haki ya kuapishwa kupitia mbinu za kuchelewesha kutangaza kifo cha raia kupisha mwanya wao kujipanga.

Ndipo Jacob Zuma akalipua taarifa kuwa endapo ikifika mchana wa tar 7 serikali ya Malawi haitatangaza kifo cha Bingu basi yeye atachukua jukumu la Kutangaza na kuusafirisha mwili (repatriation) wa Bingu nchini Malawi.

The midnight six wakaona saaa mpango umeshakwama wakakubali yaishe na wakatangaza kuwa Rais amefariki hapo hapo wakamwapisha Joyce Banda kuwa rais.

Nini kilitokea hapo baadae.

The midnight Six wote walishtakiwa ka kosa la uhaini na kufungwa Jela.

Nini umejifunza kutokana na kisa hiki?
 

Mayor Quimby

Member
Mar 13, 2021
72
150
Unasikiliza sana ngonjera za Chahali, mtu ambae aelewi hata serikali inavyoondeshwa.

Diwani Athumani hana nguvu hizo ndani ya Tanzania.

Katibu mkuu Kiongozi (Dr Bashiru) ndio mkuu wa taasisi na Idara zote za serikali, huyo ndio king maker ikitokea miujiza raisi katutoka.
 

blackstarline

JF-Expert Member
Sep 19, 2016
2,750
2,000
EvIfWxcXEAA_Dko.jpg
 

Shadow7

JF-Expert Member
Sep 28, 2020
6,501
2,000

Peter Mutharika: Kutoka mshtakiwa wa uhaini hadi rais​

Peter Mutharika, ambaye alitangazwa mshindi wa uchaguzi wa Malawi siku ya Ijumaa, anajiandaa kuchukuwa hatamu ya uongozi wa taifa hilo maskini la kusini mwa Afrika chini ya kivuli cha mashtaka ya uhaini.

Mshindi wa kinyanganyiro cha urais wa Malawi Peter Mutharika (katikati) akisalimiana na wafuasi wake.
Mshindi wa kinyanganyiro cha urais wa Malawi Peter Mutharika (katikati) akisalimiana na wafuasi wake.

Mutharika mwenye umri wa miaka 74 na nduguye rais wa zamani Bingu wa Mutharika alishinda kwa asilimia 36.4 ya kura dhidi ya asilimia 20.2 ya rais wa wasa Joyce Banda. Matokeo hayo yalitangazwa dakika chache baada ya mahakama ya juu kutupilia mbali jaribio la dakika za mwisho kuzuwia kutolewa kwake, ili kuruhusu kura zihesabiwe upya.

Mkuu wa tume ya uchaguzi Maxon Mbendera alimtangaza Mutharika kuwa "rais mteule" baada ya uchaguzi huo uliyofanyika wiki iliyopita, ambao rais Banda alidai ulikumbwa na kasoro nyingi na kuutangaza kuwa batili. Matokeo hayo yalionyesha kuwa Banda alitupwa katika nafasi ya tatu, akishindwa pia na Lazurus Chakwera wa chama cha Malawi Congress MCP, aliejipatia asilimia 27.8 ya kura.

Rais wa sasa Joyce Banda alipopiga kura yake.
Rais wa sasa Joyce Banda alipopiga kura yake.

Katika kivuli cha mashtaka ya uhaini
Mutharika sasa anajiandaa kuchukua hatamu ya uongozi chini ya kivuli cha mashtaka ya uhaini. Anatuhumiwa kujaribu kuficha kifo cha kaka yake akiwa ofisini miaka miwili iliyopita kwa lengo la kumzuwia Banda - ambaye wakati huo akiwa makamu wa rais, kuchukuwa madaraka.

Banda aliibuka kidedea na kuapishwa kuwa rais kama katiba inavyoagiza, akimuondoa serikalini waziri huyo wa zamani wa mambo ya kigeni, lakini Mutharika alimchachafya vibaya katika uchaguzi wa Mei 20.

Kiongozi huyo wa chama cha DPP Mutharika na maafisa wengine waandamizi wanakabiliwa na mashtaka mengine ya kuchochea uasi na kula njama za kufanya mauaji. Kesi hiyo bado haijaanza kusikilizwa, lakini wachambuzi wanasema kuna uwezekano mkubwa kwa kesi hiyo kuwekwa kando kwa sababu marais wa Malawi wanakuwa na kinga muda wote wanapokuwa madakarani.

Kibao cha "Cashgate" kumgeukia Banda?
Kuna fununu kuwa Mutharika atakapokuwa ofisini, anaweza akamgeuzia kibao Banda na kumshtaki kwa rushwa, kuhusiana na kashfa ya wizi wa dola za Marekani milioni 30 uliopewa jina la "Cashgate." Banda amedai sifa kwa kufichua kashfa hiyo, ambayo ilishuhudia fedha za msaada zikifujwa na wajanja serikalini. Lakini wakosoaji akiwemo Mutharika, wanasema fedha hizo zilienda kwenye kampeni ya chama chake.

Rais wa Zamani Hayati Bingu wa Mutharika.
Rais wa Zamani Hayati Bingu wa Mutharika.

Mutharika, profesa wa sheria ambaye aliishi kwa sehemu kubwa nje ya nchi, aliingia katika medani ya siasa ya Malawi mwaka 2009 alipochaguliwa kuwa mbunge na kuteuliwa waziri wa sheria. Baadaye alishikilia nyadhifa mbalimbali zikiwemo za elimu na masuala ya kigeni.

Amesema kuwa hatozingatia sera za uchumi wa kutoka juu kwenda chini, bali atakumbatia sera za uchumi wa kuanzia chini kwenda juu, zinazonuwia kuwaondoa watu kwenye umaskini na kuwaletea mafanikio. Msomi huyo aliegeuka kuwa mwanasiasa ana kibarua kigumu cha kujenga upya uchumi dhaifu wa taifa hilo, na kuwavutia wafadhili wa kigeni waliositisha sehemu ya msaada wao kufuatia sakata la "Cashgate."

Kitendawili cha uongozi wake
Mfumo wa uongozi wake serikalini, nje ya kivuli cha kaka yake mkubwa, bado ni kitendawili, wanasema wachambuzi. " Ni mtu mwenye maneno machache --- kwake hatuwezi kujua nini cha kutarajia," alisema Boniface Dulani kutoka chuo kikuu cha Malawi. "Hakuwa na ushawishi mkubwa wakati alipokuwa bungeni. Alikuwa akiongea kwa nadra."

Wakati Mutharika akiwa waziri wa elimu Chuo Kikuu cha Malawi kilikabiliwa na mgogoro, na kusababisha kufungwa kwa muda mrefu, baada ya wahadhiri watatu kufutwa kazi kufuatia matamshi waliyoyatoa darasani.

Ramani inayoonyesha mipaka ya kimataifa ya Malawi na mji mkuu wake Lilongwe.
Ramani inayoonyesha mipaka ya kimataifa ya Malawi na mji mkuu wake Lilongwe.

Mmoja alisema kuwa "Machipuko ya mataifa ya kiarabu" huenda yakaikumba Malawi. "Wakati wa kipindi hicho tete kilichohatarisha uhuru wa taaluma, Mutharika alishindwa kuonyesha uongozi," alisema Dulani. Baadaye alihamishiwa kwenye wizara ya mambo ya kigeni.

Peter Mutharika ni nani hasa?
Akiwa na shahada za sheria kutoka vyuo vikuu vya London na Yale, Mutharika aliondoka nchini Malawi katika miaka ya 1960 na kuweka makazi nchini Marekani. Alirejea nchini Malawi mwaka 1993 kusaidia kuandaa katiba ya kwanza ya kidemokrasia baada ya kuanguka kwa utawala wa dikteta Kamuzu Banda. Alirudi nchini Marekani lakini akarudi tena nyumbani mwaka 2004 baada ya kaka yake kuingia madarakani.

Akiwa mjane kwa miaka 30, Mutharika ana watoto watatu ambao wote wanaishi nchini Marekani. Kuchaguliwa kwake kunamfanya kuwa rais wa tano wa Malawi tangu nchi hiyo ilipopata uhuru wake kutoka kwa Uingereza mwaka 1964.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom