Rais Chakwera apiga marufuku Safari za Nje za Viongozi pamoja na yeye mwenyewe

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,121
1700126024951.png
Rais Lazarus Chakwera amesitisha mara moja safari zote za Kimataifa zinazomhusisha yeye na maafisa wote wa Serikali huku akiwaagiza Mawaziri wote walioko nje ya nchi kwa sasa kurejea haraka Nchini humo.

Pia, Chakwera ameweka vikwazo vya Safari za ndani ya Nchi na kupunguza kwa nusu ya mgawo wa Mafuta kwa Mawaziri na Maafisa Wakuu wa Serikali, uamuzi ambao utatumika hadi mwisho wa mwaka wa Fedha ujao, (Machi 2024).

Aidha, Rais amemtaka Waziri wa Fedha kuweka masharti ya nyongeza ya Mishahara kwa watumishi wote wa Umma katika mapitio ya Bajeti ya mwaka 2024/25 pamoja na kupunguzwa kwa Kodi ya Kipato (PAYE) kwa Wafanyakazi akieleza kuwa Mapato yao yamepoteza thamani kutokana na Mfumuko wa Bei.

Hatua ya Rais inafuatia Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) kuidhinisha mkopo wa miaka 4 wa Tsh. Bilioni 435.5 siku chache baada Benki Kuu kutangaza thamani ya Sarafu ya Malawi imeshuka kwa 44%.

=========

Malawi’s President Lazarus Chakwera has suspended with immediate effect all international travel involving himself and all government officials.

He has also ordered all ministers currently outside the country to return home.

Speaking in a televised address on Wednesday night, he also announced restrictions on local travel and a reduction by half of the fuel allocation to cabinet ministers and senior government officials.

The measures will be in place until the end of the financial year next March.

Some similar austerity measures were also announced during the Covid pandemic but had limited impact as they were not strictly enforced.

The president asked the minister of finance to make provisions for a reasonable wage increase for all civil servants in the next budget review.

He also directed a reduction of income tax in the new budget so as to help workers whose pay has lost value as result of inflation.

The president’s move comes as the International Monetary Fund (IMF) approved a four-year credit facility for Malawi worth $174m (£140m), just days after the country devalued its local currency.

Last week, the central bank announced a 44% drop in the value of the local currency, the kwacha.

Analysts suggest the devaluation may have been a condition for securing the IMF credit facility.

BBC
 
Hivi mfano nimechukua mkopo wa Million 100 bank, hela ikashuka thamani kama hiyo 44%, je Bank watapandisha interest rate yangu au itakua imekula kwao ??
 
Nilitaka kushangaa Chakwera huyuhuyu aliyechaguliwa mwezi huohuo mkewe, watoto na shemeji wakaenda nje ziara ya kikazi kuzurula. Baadae kidogo Waziri wake wa Mambo ya Nje akaenda Uingereza kuhudhuria kikao cha online baadae akajitetea kwao mtandao ulikuwa unasumbua.

Nikajua yeye ndio kazuia kumbe kibano cha IMF na WB. Kama kuna marais wapumbavu hata Chakwera yupo, since day one namkataa. We uliona wapi Askofu akaongoza nchi kwa ufanisi. Alafu huyu alikuwa mpinzani mkubwa.

Kwanza nyadhifa za juu kajaza mashemeji na kabila lake. Hopeless
 
Rais Lazarus Chakwera amesitisha mara moja safari zote za Kimataifa zinazomhusisha yeye na maafisa wote wa Serikali huku akiwaagiza Mawaziri wote walioko nje ya nchi kwa sasa kurejea haraka Nchini humo...
Huyu Rais aliwahi kuja hapa nchini halafu siku anaondoka akaniachia upweke utadhani alikuwa amenitembelea mimi. Sikupenda kabisa aondoke. Ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kusikia hali hiyo; sijui ni kwa nini!
 
Rais wa Malawi Lazarus Chakwera amesitisha safari zote za Kimataifa zinazomhusisha yeye na Maafisa wote wa Serikali pia amewaagiza Mawaziri wote walioko nje ya Nchi kwa sasa kurejea nyumbani.

Akilihutubia Taifa kupitia Televisheni usiku wa kuamkia leo pia ametangaza kupunguza asilimia 50 ya pesa ya mafuta kwa Mawaziri na Maafisa Wakuu wa Serikali kama njia za kubana matumizi.

Hatua hiyo inafuatia kushuka kwa thamani kubwa ya sarafu ya Kwacha huku Malawi ikitegemea mkopo kutoka kwa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) ili kukuza uchumi wake unaodorora, hatua hizo zitaendelea hadi mwisho wa mwaka wa fedha mnamo March 2024.

Rais amemtaka pia Waziri wa Fedha kuweka masharti ya nyongeza ya mishahara kwa Watumishi wote wa umma katika mapitio yajayo ya bajeti pia ameagiza kupunguzwa kwa ushuru wa mapato kwa Watu binafsi katika bajeti ijayo ili kusaidia Wafanyakazi ambao kipato cha kimepoteza thamani.
 
Rais Lazarus Chakwera amesitisha mara moja safari zote za Kimataifa zinazomhusisha yeye na maafisa wote wa Serikali huku akiwaagiza Mawaziri wote walioko nje ya nchi kwa sasa kurejea haraka Nchini humo.

Pia, Chakwera ameweka vikwazo vya Safari za ndani ya Nchi na kupunguza kwa nusu ya mgawo wa Mafuta kwa Mawaziri na Maafisa Wakuu wa Serikali, uamuzi ambao utatumika hadi mwisho wa mwaka wa Fedha ujao, (Machi 2024).

Aidha, Rais amemtaka Waziri wa Fedha kuweka masharti ya nyongeza ya Mishahara kwa watumishi wote wa Umma katika mapitio ya Bajeti ya mwaka 2024/25 pamoja na kupunguzwa kwa Kodi ya Kipato (PAYE) kwa Wafanyakazi akieleza kuwa Mapato yao yamepoteza thamani kutokana na Mfumuko wa Bei.

Hatua ya Rais inafuatia Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) kuidhinisha mkopo wa miaka 4 wa Tsh. Bilioni 435.5 siku chache baada Benki Kuu kutangaza thamani ya Sarafu ya Malawi imeshuka kwa 44%.

=========

Malawi’s President Lazarus Chakwera has suspended with immediate effect all international travel involving himself and all government officials.

He has also ordered all ministers currently outside the country to return home.

Speaking in a televised address on Wednesday night, he also announced restrictions on local travel and a reduction by half of the fuel allocation to cabinet ministers and senior government officials.

The measures will be in place until the end of the financial year next March.

Some similar austerity measures were also announced during the Covid pandemic but had limited impact as they were not strictly enforced.

The president asked the minister of finance to make provisions for a reasonable wage increase for all civil servants in the next budget review.

He also directed a reduction of income tax in the new budget so as to help workers whose pay has lost value as result of inflation.

The president’s move comes as the International Monetary Fund (IMF) approved a four-year credit facility for Malawi worth $174m (£140m), just days after the country devalued its local currency.

Last week, the central bank announced a 44% drop in the value of the local currency, the kwacha.

Analysts suggest the devaluation may have been a condition for securing the IMF credit facility.

BBC
Nchi imefilisika
 
Hivi mfano nimechukua mkopo wa Million 100 bank, hela ikashuka thamani kama hiyo 44%, je Bank watapandisha interest rate yangu au itakua imekula kwao ??
Kwa nmb inapanda, na niliwahi kuhoji Hilo,kwny fomu yao ya vigezo na masharti ya mikopo, icho kipengele kipo
 
Back
Top Bottom