Tujifunze kidogo kuhusu ndege (airplane)

Tujifunze kidogo kuhusu ndege (airplane)

Hapana, japo zote zinafanya kazi katika kanuni moja. Helicopter yenyewe lift force (Kani-mnyanyuo) inazalishwa na rotor blade (lile panga la juu). Haina mabawa. Helicopter inaweza kujongea pande zote, yaani mbele, nyuma, kushoto na kulia. Rubani anacheza na tilt angle tu. Kitu ambacho airplane haiwezi
Naona kama mfumo wa helcopta ni simple kuliko hayo madege....ni kwann wasitumie mfumo huo huo kutengeneza ndege kubwa kama boing?
 
Shebbydo Asante kwa somo zuri.Kule kwenye cockpit kuna mzani rubani kufahamu kwamba ndege yake ina uzito fulani?
 
Kuna watanzania watundu sana watengeneza vitu kama helicopter je kuna aliyefanikiwa ikapaa bila ya shida yeyote?
 
Mkuu zile jet ndio injini au kuna injini ambayo inazalisha nguvu ya kuzisukuma!!
 
Hizi bomberdia zetu pendwa pia zina mfumo kama hizo ndege zingine? manake sizisikii siku za hivi karibuni
 
Kuna watanzania watundu sana watengeneza vitu kama helicopter je kuna aliyefanikiwa ikapaa bila ya shida yeyote?

Hapana mkuu haijawahi kutokea. Kuunda ndege hasa helicopter iweze kupaa ni gumzo. Zaidi tutaishia kutengeneza midoli.

Kama stori ya yule jamaa sikumbuki alikuwa wa wapi waliyedai katengeneza helikopta kwa kutumia vifaa vya gari, mimi nilibaki kucheka.

Jambo kama hulijui ni sawa na usiku wa giza. Sifa ya kwanza ya vifaa vinavyounda ndege ni imara lakini vyepesi. Suala la injini ya gari kurusha helikopta ni ndoto za mchana kwa sababu hata kama utaunga unga shaft zako pamoja na mapangaboyi yako, haiwezi kuwa na power ya kutosha.

Ndege kila kifaa kilichopo kipo kwa hesabu maalum. TCAA walivyopiga marufuku watu wakalalamika eti tunaua vipaji, mimi niliona ni kwa sababu watu hawaelewi tu. Laiti wangeelewa hata kidogo kuhusu airworthness wangeandamana kwenda kumzuia yule jamaa asilete majanga ya majariribio ya kitu asichokuwa na ufahamu nacho.
 
Asante kwa somo zuri.Kule kwenye cockpit kuna mzani rubani kufahamu kwamba ndege yake ina uzito fulani?
Hakuna mzani kwenye cockipit ila ndege ipo equiped na vifaa vingi sana (INSTRUMENTS) za kitoa taarifa mbalimbali. Ndege ikiwa ardhini inajua, ikiwa angani inajua pia sasa uzito haupo kwenye matairi.
 
Ni kwa sababu jibu lako limenichanganya na nilichokuwa nakijua kama kishikilishi cha injini. Kama unaona nakuudhi samahani sana bwana mdogo.
Sina imani kama kweli unafahamu umri wangu ukiachilia mbali kunifahamu mimi. Unamaanisha nacelle ni kishirikishi cha injini? Labda mimi nikuulize tu, injini ya ndege inakaa wapi?
 
Hizi bomberdia zetu pendwa pia zina mfumo kama hizo ndege zingine? manake sizisikii siku za hivi karibuni
Bombardier zipo kama ndege zingine tofauti ni power plant. Kwa mfano Q400 na Q300 zinatumia propeller kuzalisha thrust, power plant yake ni turboprop.
Huzisikii kivipi mkuu?
 
Ok! Bahati mbaya sina uzoefu na ndege za kijeshi ila milango yote ya ndege inaendeshwa na actuators. Nadhani itakua ni mfumo tu ambao pilot akicommand basi actuator inafungua ama kufunga mlango.
Na mimi nilitaka niulize kuhusu masuala ya ndege za kijeshi bahati nzuri umesema huyajui
 
Nashukuru kwa somo hili ndugu. Mimi napenda sana kuwa ruban ttzo sijui gharama halisi za koz hucka na kama hapa nchini kuna chuo hucka. Msaada tafadhali
 
Ahsante sana ndugu Shebbydo kwa kutupatia/kutuongezea ufahamu ya usafiri wa anga ambao tunautumia mara kadhaa bila hata kuwa na ABC yake.

Labda ningekuomba utujuze juu ya mifumo/classifications za ndege maana tunasikia majina kama JET Engines na kuna hizi zenye mapangaboi mengine yako kwenye pua ya ndege na mengine yameshikizwa kwenye mabawa nk. Natanguliza shukrani
 
Mleta uzi you look like a microburst![emoji30][emoji30][emoji30]
 
Unajibu vzuri sana mkuu. Nataka kujua wakati watu wapo ndani ya ndege je? Wanatumia oxygen inayotoka wapi? Na kwann ndege ikitaka ku crush vile vidude vinavyo toka automatically vnakuwa toa wapi hewa? Asante
 
Nashukuru kwa somo hili ndugu. Mimi napenda sana kuwa ruban ttzo sijui gharama halisi za koz hucka na kama hapa nchini kuna chuo hucka. Msaada tafadhali
Asante sana ndugu.

Kukipenda kitu ni hatua ya kwanza ya kwenda mbele hata kama hicho ulichokipenda kinachangamoto zake.
Mambo haya ya elimu ya ndege hasa kwa urubani na uhandisi yanachangamoto katika kumudu gharama zake. Gharama zake ni kubwa sana.

Fani ya urubani inagawanyika katika leseni zifuatazo;
1: Private Pilot Licence (PPL); hii ni leseni ya chini katika urubani. Ili upate leseni hii lazima uwe na masaa ya kuwa angani 40 (flying hours). Leseni hii inakuruhusu kuongoza ndege ambayo si abiria. Yaani ni wewe na familia yako na jamaa zako ndani ya ndege. Kwa hapa Tanzania, pale airport kuna mzungu anafundisha leseni hii kwa mli. 35 Tsh. Nilisikia NIT walitaka kuanzisha course ya urubani sijui waliishia wapi.

2:Commrcial Pilot Licence (CPL); Hii ni leseni inayokuruhusu kuongoza ndege za kukodiwa lakini si abiri. Lakini pia ukiwa na leseni unaweza kuajiliwa kwenye kampuni ya ndege kama Co-pilot wakati ukifukuzia masaa. Chuo cha Soroti flying school kinatoa mafunzo ya leseni hii kwa 62_000 USD. Hii leseni ni lazima uwe na masaa ya angani 200. Kwa mfano yule mzungu pale airport JNIA anatoza saa moja 200 USD.

3: Airline Transport Pilot Licence (ATPL); Hii ndo leseni inayokuruhusu kuongoza ndege za abiria. Na ili upate leseni lazima uwe na masaa yasiyopungua 1000.Lakini uzuri wa leseni utafikisha hayo masaa ukiwa ni Co-pilot ilimradi upate sehemu ya kujishikisha. Ukishafikisha masaa 100 mwanga unaanza kuonekana.
 
Back
Top Bottom