Tujiandae na Vita ya Tatu ya Dunia

Killing machine

JF-Expert Member
Jul 24, 2022
1,424
1,637
Habari wakuu zangu,

Kuna msemo unasema "Jela hakuna mateso ila wanao leta mateso jela ni wajelajela wenyewe."

Hivyo hivyo duniani ni mahala salama, pana maji, vyakula ardhi nzuri, na vyote Mungu alitoa bure. Yaani ule bure, unywe bure, ujenge popote bure, uwinde bure, uvue samaki was baharini bure nk.

Vyoote Mungu alitoa bure kabisa kusudi maisha yawe rahisi na yenye fraha duniani kote, lakini kuna watu wachache walio barikiwa roho za kibinafsi, makatiri, wasiyoipenda katu furaha wala amani wasio iwazia mema dunia yetu nzuri, wala uzao wake wa asili.

Wakajimilikisha mito na maziwa ili wauze maji na kuwalipisha ushuru wavua samaki na wapita na meli juu ya bahari mito na maziwa.

Wakajimilikisha aldhi ili wawalipishe ushuru wakulima walimao juu ya nchi na kuwauzia ardhi wale watakao kujenga na kuishi na wale wafugaji na hata wale wachimbaji wa madini ardhini kama dhahabu, chuma, nk.

Wakajimilikisha anga ili walipwe ushuru kwa wale wapitao na vyombo vya angani. Hawakuishia hapo, wakafikia hatua mpaka ya kutaka ushuru kwa wale walitangazao neno la Mungu, Mungu muumba mbingu na nchi!

Kwa matendo yao wakaipandisha pesa thamani, pesa ikawa na nguvu kuliko utu, pesa ikatawala ikazisimamisha na kuziangusha tawala, ikawasimamisha na kuwaangusha wafalme.

Pesa ikaharibu kabisa nguvu ya upendo kwa dunia yetu pendwa. Wasio na pesa wakakosa ardhi, wasio napesa wakakosa Uhuru, wasio na pesa wakakosa maji, wasio na pesa wakakosa chakula, paku lala, elimu, mavazi, nk, watu wakaitambua thamani ya pesa, wakapania kuitafuta kwa njia yoyote ili wapate heshima, makazi, chakula, maji, mavazi nk.

Kadri watu walivyotafuta pesa kwa nguvu na kwa akili zao zote, wale walioumiliki utajiri wote wa dunia pesa zote za inchi wakapata hofu wakaanza kuwaita; majambazi, matapeli, wakabaji, ombaomba, maskini, mafukara, wadangaji, ma bar maid, wapasua mbao, makapuku wanuka kwapa.

Hawakuishia hapo wakawaita magaidi wakawaua kwa risasi, mabomu, visu, mafuta, magonjwa ya zinaa, nyuklia nk, hawakujipa muda kujiuliza kwanini ujambazi umeshamili, kwanini ngono zimeshamili, kwanini wa watu wanauwana, kwanini migogoro ya ardhi imeshamili!

Hawa kuwa na muda huo, walichojari ni kuongeza ulinzi juu ya mali zao, familia zao, pesa zao, na kuongeza ufanisi katika kutengeneza silaha nzito kwa ajili ya kulinda maslahi yao na utajiri wao.

Leo hii dunia imekuwa uwanja wa vita, magonjwa, visasi, shida, dhiki, ukame, japo maji yapo, kwani hawako tayari kuhakikisha maji yanapatikana kila mahari kwa kuhofia watashindwa kuuza maji ya chupa, wala hawako taya rikuhakikisha kila mmoja ana nyumba ya kulala kwa kuhofia watapoteza mapato kwenye nyumba za kupanga.

Wala hawako tayari kuzalisha umeme wa kutosha kwa kuhofia watashindwa kuuza magenerator, pesa imetufikisha pabaya tumekuwa wanyama! Natokwa na machozi nikiitazama Sudan, Congo, Ukraine, leo hii Palestina na Israel.

Naona kuna mama, watoto, na wazee, wakati wanaoupitia ni mgumu sana na hauelezeki. Yote haya yanatokea kwa sababu ya ubinafsi wa watu wachache ili wauze silaha zao na kuzitangaza biashara zao. Mambo haya yanatupeleka kuelekea Vita ya Tatu ya Dunia kwani nvita zote msingi wake ni ubinafsi.

Vita hii itaanzia pale Irani itakapoingilia kati, bila shaka Mmisri hatasita na vipi nchi nyingine za kiislamu kama Saudi Arabia, nk, na huku pembeni Muingereza na Mjerumani na washirika wengine hawatakaa kimya.

Kwahiyo tujiandae gharama za maisha kupanda zaidi.
 
Wataishia hivyo hivyo wao wenyewe...mlisema hivyo hata kwa Urusi na Ukraine...
Hata ukisema nchi za kiislamu zipigane na za kikristo mzani utawaelemea watanyukwa vibaya...
 
Hakuna vita ya tatu watu walijifunza kwenye vita ya pili, ambapo Hadi leo athari zake zinaonekana, sasahivi watu hawawezi Kuingia kichwa kichwa kupigana, HAMAS kalikoroga sasahivi wapslestina ndiyo wanaumia wakina Misri na Jordan na Lebanon ambao ni majirani tayari wameshafunga na mipaka hawataki maneno wakina Saudi Arabia wao wametoa ahadi tu yakusaidia mahitaji ya kibinadamu, huko Kwa Putin anaugulia taratibu Irani mshirika wake ataki kujiingiza Moja Kwa Moja, anatoa vidrones tu Tena kwakujificha kama alivyo wapa HAMAS
 
Habari wakuu zangu,?

Kuna msemo unasema "jera hakuna mateso Ila wanao let's mateso jera ni wajera jera wenyewe"

Hivyo hivyo duniani nimahara sarama Pana maji,vyakura ardhi nzuri, na vyote mungu alitoa Bure Yani ule bure,unywe bure,ujenge popote bure, uwinde bure,uvue samaki was baharini bure nk

vyoote mungu alitoa buure kabisa kusudi maisha yawe rahisi na yenye fraha duniani kote

Lakini Kuna watu wachache walio barikiwa roho za kibinafsi,makatiri,wasiyo ipenda katu fraha wara amani wasio iwazia mema dunia yetu nzuri, Wala uzao wake wa asiri

Wakaji milikisha mito na maziwa ili wauze maji nakuwalipisha ushuru wavua samaki na wapita na Meri juu ya bahari mito na maziwa.

Wakaji milikisha aldhi ili wawalipishe ushuru wakulima walimao juu ya inchi nakuwauzia aldhi wale watakao kujenga na kuishi na wale wafugaji nahata wale wachimbaji was madini aldhini Kama dhahabu,chuma,nk

Wakaji milikisha anga ili walipwe ushuru kwa wale wapitao na vyombo vya angani hawakuishia hapo wakafikia hatua mpaka ya kutaka ushuru kwa wale wali tangazao neno la mungu mungu muumba mbingu na inchi.

Kwa matendo yao wakaipandisha pesa thamani pesa ikawa na nguvu kuliko utu pesa ikatawala ikazi simamisha na kuziangusha tawara ikawa simamisha na kuwa angusha wafalme.

Pesa ikaharibu kabisa nguvu ya upendo kwa dunia yetu pendwa wasio na pesa wakakosa aldhi, wasio napesa Waka kosa Uhuru, wasio na pesa wakakosa maji wasio na pesa wakakosa chakula,paku lala, elimu, mavazi, nk
watu wakaitambua thamani ya pesa wakapania kuitafuta kwanjia yoyoteili wapate heshima, makazi, chakula, maji, mavazi nk.

Kadri watu walivyo tafuta pesa kwanguvu na kwa hakilizao zote wale walio umiliki utajiri wote wa dunia pesa zote zainchi wakapata hofu wakaanza kuwaita. Majambazi, matapeli, wakabaji, ombaomba, maskini ,mafukara, wadangaji, ma bar maid wapasua mbao, makapuku wanuka kwapa, hawakuishia hapo wakawaita magaidi wakawauwa kwa risasi, mabomu, visu, mafuta, magonjwa ya zinaa, nyukria nk hawakujipa mda kujiuliza kwanini ujambazi umeshamili?

Kwanini ngono zimeshamili? Kwanini wa watu wanauwana? Kwanini migogoro ya ardhi imeshamili? Hawa kuwa na mda huo walicho jari nikuongeza ulinzi juu ya Mari zao, familia zao, pesa zao, nakuongeza ufanisi katika kutengeneza siraha nzito kwa ajiri ya kulinda masrahi yao na utajiri wao.

Leo hii dunia imekuwa uwanja wa Vita, magonjwa, visasi, shida, dhiki, ukame, japo maji yapo kwani hawako tayali kuhakikisha maji Yana patikana Kila mahari kwa kuhofia watashindwa kuuza maji ya chupa wala hawako taya rikuhakikisha Kila mmoja Ana nyumba ya kulala kwa kuhofia watapoteza mapato kwenye nyumba za kupanga.

Wala hawako tayari kuzalisha umeme wa kutosha kwa kuhofia watashindwa kuuza magenerator, pesa imetufikisha pabaya tumekuwa wanyama natokwa na machozi nikii tazama Sudan, Congo, ucraine,leo hii parestina na Israel

Naona Kuna mama, watoto, na wazee, wakati wanao upitia nimgum sana na hau elezeki. Yote haya yana tokea kwa sababu ya ubinafsi wa watu wachache ili wauze sraha zao nakuzitangaza biashara zao. Mambo haya yana tupeleka kuelekea Vita ya tatu ya dunia kwaninvita zote msingi wake ni ubinafsi.

Vita hii itaanzia pale Irani itakapo ingilia kati bira Shaka mmisri hata sita na vipi inchinyingine za kiisramu Kama Saudi Arabia nk na huku pembeni mwingereza na mjerumani na washilika wengine hawata kaa kimya.

Kwahiyo tujiandae gharama za maisha kupanda zaidi
ok sawa
 
Picha unayoiona hapo chini Ni msikiti wa dhahabu maarufu Sana duniani kwa jina la AQSA, ambao uko katika viunga vya mji wa Jerusalemu.

Msikiti huo ulijengwa baada ya Vita ya jihadi iliyopiganwa Kati ya uislam na uyahudi na kupelekea kubomolewa kwa hekalu la Sulemani na kujengwa msikiti huo. Vita hii ilifanya mji wa Jerusalem kuangukia mikononi mwa utawala wa kiislamu (islamc empire).

Waislamu duniani wanaheshimu na kuthamini eneo hili na kila Mwaka wanaenda kuhiji au kulitembelea eneo Hilo wanaloamini Ni takatifu katika dini yao.

Wayahudi na Wakristo wanaliheshimu na kulithamini eneo hili na kuamini ndipo lilipokuwepo hekalu lililojengwa na mfalme Sulemani.

Vita na migogoro mingi unayoishuhudia mashariki ya Kati chanzo Chake Ni msikiti huu wa dhahabu. Kila dini linadai Ni mahali pake patakatifu.

Vita ya tatu ya kidunia ambayo itahusisha slaha za nyuklia , chanzo Chake kinaaminika kusababishwa na mgogoro wa msikiti huu wa AQSA.

Wayahudi wanampango wa kuubomoa msikiti huu ili kujenga hekalu jipya, na hapa ndipo chanzo Cha Vita ya kidini Kati ya mataifa ya kiislamu na mataifa yanayounga mkono Israel.

Vita hivi vitaitwa Vita vya AMAGEDON.

Mataifa ya GUGO yatapigana na mataifa ya MAGUGO. Mamilioni ya watu watakufa na dunia itakuwa katika eneo isiyo salama kuishi.

Nchi nyingi duniani zitakumbwa na mtikisiko wa kiuchumi, njaa, mafuriko na matetemeko ya ardhi.

Vita hivi vitaisha kwa makubaliano ya mkataba wa amani, ambao utaunganisha dini tatu za ukristo, uislam na uyahudi kuwa dini moja ya kishetani ambayo Ni ya mpinga Kristo, na dunia itaanza rasm matumizi ya no 666.

Dunia itakuwa na dini moja, serikali moja na fedha moja.

Kwa hiyo hakuna mtu kuuza Wala kununua, Wala kutibiwa asipokuwa na chapa ya kishetani ya no 666.

Myaonapo Mambo hayo yakitokea tambueni ya kwamba Siku za mwisho zimekaribia.

Mwenye kudhurumu azidi kudhurumu.

Mwenye uchafu azidi kuwa mchafu.

Mtakatifu azidi kujitakasa.

Mwana wa Adamu yupo mlangoni kulichukua kanisa lake.

Mungu akubariki.

1699070136736.jpg
 
Kwanza umepotosha hakuna jihadi iliyovunja hekalu,hekalu lilivunjwa mara nyingi sana na ya mwisho ni miaka 70 baada ya kristo,walilivunja warumi.

Huo mskiti wa alqsa ulijengwa kwenye eneo lilipikuwepo hekalu.

Israel ikimalizana na wapalestina itauvunja na kujenga hekalu lao na hakuna kitu waarabu watafanya zaidi ya porojo mana eneo hilo sio lao walilivamia tu
 
Well israel ni mbabe
 
Unastahili kupokea Maua
 
Katika historia ya dunia Vita ya pili ndio ilikua yenye mafanikio kwa kuunda mifumo ya kulinda amani kama UN, na sheria Nyingine za kimataifa ambazo zimefanya Dunia isiingie kwenye vita nyingine ya Tatu.

VITA YA TATU YA DUNIA
Scholar wengi wamejaribu kutabiri au kuchambua juu ya uwezekano wa vita ya dunia lakini theory zote zimeonekana hazina mashiko kasoro moja !!

NINI KITAFANYA KUANZA KWA VITA YA DUNIA
Ili kuwepo na vita ya dunia lazima mataifa makubwa duniani yawe kwene pande mbili tofauti zinazokinzana na kusiwe na suruhu kisha mataifa mengine vibaraka vya mataifa makubwa yatafuatisha kile mabwana zao wakuu watachosema!

Hapa kuna kupangiana adui na kupigana vita ambayo nchi nyingine hazikua na uadui!

KITOVU CHA VITA YA DUNIA
1.Ukraine
Wengi wanadhani au walidhani Ukraine itakua ni kitovu cha vita ya tatu ya dunia hasa ukizingatia Nchi kubwa zenye nyuklia zilihusika

Nadhalia hii haijaonekana kua na mashiko kwan mataifa mengine makubwa kama India, China na Africa kwa ujumla imeonekana kujiweka mbali na vita hii.

Pia USA kamwe asingepeleka jeshi la marekanai ( siongelei mercenaries) kwenye vita ambayo lengo lake ni kuidhoofisha russia

Russia haina uchumi mkubwa wa kuendelea na vita kwaiyo ingefika sehemu wangeachana na vita na kurudi zao Russia kama walivo fanya miaka ya 79 Afghastan

2.Taiwan China war
Hii pia inaonekana kama ndio itakua vita kubwa tangu USA ianze kupigana vita.
USA economy (24T) Vs China (17T)
Itakua ni vita itayoidhuru dunia kwa kiasi kikubwa na ndo yenye uwezo wa kusababisha Mataifa mengi yakapigana.
Ingawa kwa sasa china haiko tayari lakini Iko serious sana kwenye swala la Taiwan

3.Israel VS Arabs
Hiki ni kitovu haswaa cha vita ya dunia.
Sababu ni kua hapa ndipo sehemu kubwa ya dunia inagongana.

Israel /USA/Western hawa wote watasimama upande wa Israel achana na makelele wanayopiga mapinzani wa israel kwenye hizi nchi ikishafika wakati watazimwa kama kibatari gizani

Upande wa pili ambao taratibu unajitengeneza utakua ni
Arabs include North Africa/Iran/Russia/China na nchi nyingine kama pakistan,Bangladeshi ,indonesia na malaysia

NB: Vita itahusisha nyuklia,,, hivo madhara yatakua makubwa kulikoa inavodhaniwa
 
rekebisha neno ''suruhu iwe suluhu'' ili tuendelee kuchangia
 
Back
Top Bottom