Tulia, spika wa Bunge la JMT, amekuwa mstari wa mbele katika kutetea na kulinda utekaji na mauaji ya wakosoaji.
Mara mbili, wabunge waliomba Bunge lijadili utekaji na mauaji ya wakosoaji, lakini Tulia, kama spika wa Bunge la JMT, alizizima hoja za wabunge hao, na kuzuia kabisa zisijadiliwe bungeni, akidai kuwa siyo kila anayepotea, ametekwa.
Lakini Tulia akiwa nje ya Bunge, aliwaagiza UVCCM kushughulika na yeyote atakayemkosoa Samia, na hiyo inatafsiriwa ni kubariki na kuhamasisha utrkaji na mauaji zaidi kwa wakosoaji wa Samia.
Mdude, kabla ya kutekwa na kupotezwa, alisema kuwa amepewa taarifa kuwa Tulia amewatuma watu wamwue. Tuhuma hizo hazikuwahi kuchunguzwa na polisi, wala Tulia mwenyewe hakuwahi kuzikanusha.
Hivi karibuni, wabunge kadhaa wa bunge linaloongozwa na Tulia wametoa kauli za kuunga mkono ushetani waliofanyiwa wakenya na mganda, waliokuwa wanakuja kufuatilia kesi ya Lisu, na kuwataka watekaji na watesaji waongeze nguvu zaidi.
Umoja wa Mabunge Duniani ni taasisi inayosimama kwenye misingi ya haki na demokrasia. Taasisi hiyo kuongozwa na mtu ambaye ni adui wa haki na demokrasia, ni aibu kwa Dunia nzima.
Ni vema taasisi mbalimbali za ndani na nje ya nchi ziandike barua kwenda Umoja wa mabunge Duniani kutaka Tulia aondolewe haraka na mara moja kwenye uongozi wa umoja huo, kwa sababu amekuwa doa baya kwa taasisi hiyo inayoheshimika.