Tuhuma dhidi ya Membe: Bashiru hajakurupuka, kuna ukweli

Tuhuma dhidi ya Membe: Bashiru hajakurupuka, kuna ukweli

Upinzani upi? Hao walipokea ruzuku kwa zaidi ya miaka 20 lakini wamshindwa kujenga hata banda la kuku? CCM wana mapungufu sawa, lakini upinzani wamefanya nini tofauti na CCM kama sio zaidi yao? 20 YEARS hata banda, mmeshia kukopeshwa FUSO CHAKAVU?
CCM ilichofanya kwa miaka 41 Ni kupora Mali za wote kuwa zake.Bado haikutosheka, ikaamua kugawa rasilimali za nchi kwa Wazungu na Wachina. Upinzani umejijenga na kuwa na wanachama wanaoizidi CCM na kuisambaratisha kwenye medani ya siasa, mwisho ikaiachia polisi siasa!!!
 
Mie nitakuwa mtu wa mwisho kumtetea Jiwe lakini ukweli shurti usemwe hata kama kusema ukweli huko kutamnufaisha Jiwe.

Background kidogo: unajua nani alimtambulisha Kipilimba kwa Jiwe? Membe. Why this matters? Hiyo ni mada ya siku nyingine ila conduit ya kinachoendelea kwa Jiwe kumfikia Membe ni Kipilimba.

Na hizo tuhuma alizotoa Bashiru jana sio za kutunga. Na hazikutokana na tuhuma za awali kutoka kwa Musiba. Katika hili, Musiba (anayenichafua kila anapojiskia) aliandika tu kile ambacho akina sie tunaojua yanayoendelea chini ya kapeti tunakifahamu kitambo.

Tatizo la Membe ni lile lile lilomfelisha kwenye mapambano wake dhidi ya Lowassa kuwania urais kwa tiketi ya CCM. Ni hivi, Membe alikuwa Mtanzania PEKEE aliyeonekana kuwa mbadala wa dhati wa Lowassa. He had support ya familia ya JK na Mwinyi na Mkapa hawakuwa na tatizo nae.

But he messed up big time. Kwa sie alumni wa kitengo, he did let us down. Not that kufanikiwa kwake kungekuwa na manufaa kwetu bali alishindwa kabisa kutumia intelijensia kuendesha mkakati wa urais, huku akiwa na advantage hiyo kubwa ya "real alternative" ya Lowassa.

Na sasa, pilika zake anazofanya huko nje kama mmoja wa challengers wa Jiwe 2020 ndio hizo zinamwagika hadharani.

Ni hivi, Bashiru ana solid evidence ya harakati za Membe ndani na nje ya Tanzania. Ni evidence hiyo - not tuhuma za Musiba - iliyompa ujasiri wa kumvaa Membe hadharani.

How did Jiwe know kuhusu pilika za Membe? One thing for sure sio umahiri wa Kitengo (there is none) bali mapungufu ya Membe. Huwezi kuwa na mkakati wa siri wa kumng'oa Kiongozi aliyepo madarakani lakini ukazembea kwenye usiri, licha ya kuwa shushushu mzoefu.

Finally, kuna mbinu moja kwenye surveillance ambayo japo sio maarufu sana lakini ina ufanisi mkubwa: overt surveillance, yaani kumfuatilia subject bila kufanya jitihada za kujificha asijue anafuatiliwa. Mara nyingi mbinu hii hutumika kwa minajili ya kumvuruga subject, ajue kuwa "upo kwenye rada zetu" na alazimike mwenyewe kunyoosha mikono.

One last thing, kuna vita kubwa inaendelea chinichini ndani ya CCM katika harakati za kumpata "mrithi wa Jiwe" 2020.

Angalizo: SITREP hii kama zilivyo sitrep nyingine haina lengo la kumshawishi mtu aamini.

Mimi niulize swali dogo

Hiyo strong evidence dhidi ya BM ni kuhusu nini kwani?

Je, unamaanisha kuwa anajiandaa kugombea Urais mwaka 2020?

Kama ndivyo, want's wrong with that? Kwani imetangazwa kuwa "fulani" ni mgombea pekee ktk uchaguzi mkuu wa 2020 na yeyote aoneshaye nia kugombea kupingana na huyo "fulani" atakuwa anavunja sheria?

Na si inajulikana muhula wa Rais kuongoza ni miaka mi5 na baada ya hapo uchaguzi mwingine unafanyika?
 
mbona mna discuss kama mmetoka mars vile!!!hivi ni nani angeamini kwamba lowasa siyo raisi leo hii?kolimba aliishia wap na mabadiliko yake??hivi tulitegemea mpaka leo nkurunzinza awepo madarakani bado??nchi za kiafrika bado kwenye demokrasia kutumia faulo kwenye chaguzi ni kawaida tu hata akifa mtu watu awajali hali mradi wamepata walichotaka.

Siyo kila siku ni Jumapili mjumbe, usikariri tu...!!

Not this time, not this years.

Zama za akina Kolimba na Lowassa zilishapita...
 
Niamini unachuki binafsi na Membe. Kama unajua huo ukweli kwa watanzania wengi kwanini useme? Kweli lazima usemwe,ulazimaunatoka wapi kama huo ukweli hauna faida. Kama watu wa kitengo husema ukweli mbona hawawalokuwepo hawasemi ukweli?

Mkuu nakuheshimu sana ila naomba nikuulize wewe ni Chahali pamoja na wale wa Ifakara? Niwe mkweli kama wewe unavyopenda ukweli, sijawahi kuwaamini wandamba japo ni ndugu zangu, hata hayo unayoongea 100% itakuwa kwa maslahi binafsi.
 
2020 Jiwe is out, haijalishi atatolewa na nani....... Huwezi kuja na liroho lako la kishetani uharibu ndoto za mamilioni ya watu kwa miaka kumi...... Khaaa we ni nani by the way!!!!!!!!!!!
Ahahaha,,mkuu tunae huyu hadi 2025..ila lol,,mzee kavuruga mambo
 
kwa katiba gani?? Mpya au

Kwani serikali hii inatawala nchi hii kwa kutumia katiba gani?

Kama ipo na unaijua, then, jibu unalo basi...

Kwamba ni kwa hii hii unayoijua....

Amini usiamini, Bwana Mungu muumba wa mbingu na nchi atafanya njia pasipo na njia!!

Narudia tena, usikariri tu.

Siyo kila siku ilikuwa Jumapili iliyopita.

Ipo Juma2 nyingine inakuja na ni mpya kabisa...!!
 
Magu hafai hivyo yoyote anaempinga anastahili kuungwa mkono iwe ndani ya CCM au nje ya CCM.Hata hivyo, Raisi bora hawezi kutoka CCM.

Note: Raisi bora anaweza kutoka CCM lakini kwa kofia ya upinani na si awe Raisi kwa ticket ya CCM.

Raisi anaeweza kubadili hii nchi ni lazima apate wasaidi kutoka nje ya CCM kwa maana ya watu kutoka upinzani ambao watakuwa na fikra na mitazamo tofauti.

Huwezi kufukua makaburi au kurekebisha mambo ukiwa umezungukwa na watu wale wale waliotufukisha hapa tulipo leo hii na ambao teyari wana masilahi au waliwahi kuwa na masilahi katika maeneo mengi.Unahitaji watu clean na hawa utawapata zaidi kutoka upinzani.
Chukueni huyo Membe atawasaidia sana 2020!! Yaani nimeamini kweli upinzani nchi hii hauwezi ongoza nchi hii labda baada ya miaka 100 na pawepo wapinzani wa kweli siyo hawa wakina Salary Slip
 
Kwa akili yako unaona kabisa kwamba hilo ni kundi la kutawala binadamu? Mbona tumeshawajadili kwenye uzi mwingine? Hao ni kundi la vimtu vipuuzi fulani vile! Kama mtu unakuwa waziri na cha kwanza ni kutafuta mwanamke mzuri awe msaidizi wako, kesho ukiwa rais utafanya nini? Mwingine alishasema wamarekani wanamtaka awe rais, wa-TZ je wansemaje?

Tutulize akili tunapokuwa tunabanwa kisheria. Tusipende kusifiwa kwa urafiki au kuwa maarufu kwa urafiki na rais. Aliyebanwa jamani, awe mpole, afuate sheria, basi!

Soma vizuri mchango wangu mimi nimejikita ktk kariba na ‘exposure’ pia umri ili kupata mtazamo mpya na nikasema ukitoa hao ambao nimewataja tunaweza kuwajadili pia na watakao jitokeza hapo baadae kwa kariba hiyo na umri huo na ‘exposure ‘

Pia hivi mtu kama Membe ( sijabeza uzoefu na exposure yake) ambae kahusika kwa karibu na na matokeo yoyote chanya au hasi ktk nchi hii ni kweli bado tunaweza rudi kumuona kama ni ‘best candidate’ ktk zama na wakati huu

Kwa Membe tunatengeneza ‘cycle’ ya visasi, ujuaji,kutambiana,umjini, na mambo kama hayo

Badala tuweke nguvu kwa watu watakao ‘liponya’ Taifa na mipasuko na pia kuja na mustakabali mpya sidhani Membe kama atakuwa mtu sahihi kwa nyakati hizi na narudia tena sijabeza ubobezi , uzoefu na taaluma yake lkn kumchagua ni kurudi nyuma na huu ni mtizamo wangu tu mkuu

Kina Membe na wengine wa kariba hiyo wabaki kama washauri tu kwa mambo ya Kitaifa
 
Wanaweza wakawa siyo wapya kwa dhana hiyo lakini kwa kariba na umri huo at least tungeanza hata kuwafikiria na kuwachuja na mfano Membe isingekuwa yaliyotokea labda leo ndo angekuwa Rais sasa naona imetosha na jua alikuwa karibu sana wa utawala uliopita either kwa mema au mabaya tuliyopitia

Hao kina January , Nape na wote wa kariba yao kwa uongozi na umri at least wanaweza jua mahitaji halisi ya kizazi hiki na kijacho na lengo sio wateuliwe ndo maana nimeorodhesha wengi tu na wa upinzani lkn tungeanza kuwamulika hao kuliko majina sijui Membe mara sijui nani na tunaona tulionae anavyotunyoosha kwa mitizamo yake ana ndoto labda nzuri kuhusu nchi yetu hii nzuri na inapotakiwa kuwepo lkn ona namna ya kutufikisha huko kwenye maziwa na asali tunavyoburuzwa
Kumbuka kuongoza nchi sio sawa na kubeba Zege, la msingi ni kuwa Na vision and being capable to pursue the vision. Uongozi ni karama, akili, busara,maono na exposure umri sio kigezo cha uongozi kama ilivyo kuwa umri sio kigezo cha busara. Kuna mijitu mizima haina busara na kuna wengine wanabusara pia kuna vijana wenye busara na pia wapo wasio na busara. Kiongozi anatakiwa awe na full parkage
 
Kwani serikali hii inatawala nchi hii kwa kutumia katiba gani?

Kama ipo na unaijua, then, jibu unalo basi...

Kwamba ni kwa hii hii unayoijua....

Amini usiamini, Bwana Mungu muumba wa mbingu na nchi atafanya njia pasipo na njia!!

Narudia tena, usikariri tu.

Siyo kila siku ilikuwa Jumapili iliyopita.

Ipo Juma2 nyingine inakuja na ni mpya kabisa...!!
Kwahiyo wewe katiba iko sawa
mungu wako atakupa ushindi
Kwa mipango hiyo kila la kheri boss
 
Huyu jamaa ana issue zake personal na Membe usimuamini sana
Na mkumbuke huyu jamaa alikimbia Nchini kipindi cha kikwete na Membe akiwa kiongozi mwandamizi wa Serikali inawezekana Membe alichangia huyu jamaa kukimbia so analipa kisasi kwa kumchafua.
Na sitoshangaa ikitokea wakabaki wagombea wawili let say Membe na Jiwe huyu jamaa yupo radhi kumkampenia Jiwe kama alivyofanya 2015 zidi ya Lowassa. Jamaa ana chuki sana na wote waliokuwa kwenye Utawala wa Kikwete.
 
Kumbuka kuongoza nchi sio sawa na kubeba Zege, la msingi ni kuwa Na vision and being capable to pursue the vision. Uongozi ni karama, akili, busara,maono na exposure umri sio kigezo cha uongozi kama ilivyo kuwa umri sio kigezo cha busara. Kuna mijitu mizima haina busara na kuna wengine wanabusara pia kuna vijana wenye busara na pia wapo wasio na busara. Kiongozi anatakiwa awe na full parkage

Ni kweli mkuu unachosema lkn sijasema umri peke yake ndo uwe kigezo kikubwa nimeweka na vingine na umri pia kwa maana ya kubeba dhana mpya ktk changamoto za kisasa
 
M4P
IMG-20181201-WA0015.jpeg
 
Back
Top Bottom